JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Rafiki wa karibu wa kijana huyo amesema Salvador pia alichekwa kwa kutovaa nguo nzuri, kutokana na hali hiyo alianza kukwepa kuingia darasani. Siku alipokuwa akitimiza umri wa miaka 18, alinunua bunduki mbili siku chache kabla ya tukio la mauaji.
Alipiga picha silaha alizonunua na kuzituma kwa rafiki yake licha ya kutomwambia sababu ya kuzinunua. Jirani wa kijana Ramos amenukuliwa akisema: “Alimjeruhi bibi yake kwa risasi baada ya majibizano, akaondoka na kwenda kufanya mauaji hayo.”
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea siku moja baada ya wenzake aliokuwa akisoma nao kuhitimu masomo.