Marekani anatoa misaada kiduchu hataki Ukraine ashindwe wala kushinda sana, anataka vita iwe ndefu ili kumfanyia utafiti Urusi na Ukraine awe mdaiwa

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Ndicho nachokiona, Marekani anatumia misaada kidogo kidogo lengo ni Ukraine asishinde wala asipigwe, yani vita iwe neutral wawe wanatwangana na mrusi, Nipe nikupe, Marekani akiona Ukraine anazidiwa anamtumia silaha , akiona anakaribia kupata ahueni anazima data rais wa Ukraine anaanza kulalamika, Marekani anatuma misaada kidogo kidogo kwa maksudi kabisa, mpaka sasa imefikia dola bilioni 60 ambazo tunaweza kuzioma nyingi ila kwa marekani ambaye bajeti yake pekee ni dola bilioni elf 4 hii misaada ni KIDUCHU.

lengo kuu la mmarekani kutuma misaada kidogo kidogo ni kuirefusha vita iwe ndefu ili akusanye intelejensia , Mmarekani saizi yupo na daftari lake anamfanyia urusi utafiti anakusanya intelejensia kuhusu mabadiliko ya mbinu za kivita za kisasa anazotumia urusi, kumlazimisha urusi atumie teknolojia alizoficha ili azichunguze, kupima loyalty ya wanajeshi, kujua mbinu anazotumia urusi anapobanwa na vikwazo, reaction za Putin, n.k. kwa sasa kaenda mbali zaidi hata katika tafiti zake anawapa silaha Ukraine ila yeye ndie anaeminya rimoti ya kumtungua urusi huku wakifatilia kwa makini urusi huwa anajibu vipi mapigo.

Hii vita hadi iishe ni mpaka Marekan awe kachukua notes za kutosha kajaza counter books za quire 4 za intelejensia kumhusu Urusi. kiufupi Urusi anatumika, asahau kabisa kuhusu ushindi.

Pesa ikigoma kununua kitu tumia currency nyingine, wengine hutumia zawadi, wengine hutumia urafiki, wengine hutumia connection, n.k. Marekani inanunua utiifu kutoka Ukraine kwa njia ya kuilimbikizia madeni, vita ikiisha tutarajie Ukraine ikiwa moja ya ally mpya za Marekani katika kiwango cha juu cha utiifu.

Kuhusu Putin aliingia vitani kibabe sana na ni aibu kwake kuondoka hata akipigwa ataendelea hivyo hivyo na haitakiwa kitu cha ajabu kwa Putin kuanza kuwakamua wananchi wa nchi yake ili kuilipia vita na ndipo hapa warusi watachafukwa kutakuwa na maandamano kibao na majaribio ya kumpindua Putin, na muda huo ndipo Marekani nae ataongeza zaidi misaada kwa Ukraine, sasa sijui itakuwaje hapo, ukiweka nguvu ya kuzima maandamano na mapinduzi kule Ukraine anapeleka moto sio mchezo, ikiwekwa nguvu zaidi vitani basi humo nchini maandamano na majaribio ya mapinduzi yanashika kasi, Chagua moja
 
Naweza kukubaliana na wewe. URUSI inabidi awe makini.
hizi mbinu anazotumia za kumtumia Ukraine misaada kidogo kidogo ni janja janja ya kumfanya urusi asishinde haraka maana bado kuna vitu wanamsoma Urusi kwa hio hawatak vita iishe haraka, Ukraine ndio inatumika kama uwanja wa Majaribio ya kumu observe Russia, Hata hizi silaha wanazowatumia Ukraine nyingine huwa zinapachikwa ukraine wao wanaminya rimoti Marekani... Lengo ni kuona vipi Uurusi ana respond wao wananakili.
 
Kama sisi Tanzania 🇹🇿 tumelijua hilo, iweje liwe jambo geni kwa Russia 🇷🇺?
Hao Urusi wameyakanyaga, hata kama wanajua, hawana namna !! Mmarekani saizi yupo na daftari lake anakusanya intelejensia kuhusu mbinu za vita za urusi, udhaifu wake, Loyalty ya wanajeshi, uvumilivu, anavyokabiliana na vikwazo n.k. Hii vita kwa mmarekani kaamua kuitumia Ukraine kama darasa la kumsoma Urusi, wala hana haraka kabisa, Hii vita hadi iishe ni mpaka Marekan awe kachukua notes za kutosha kajaza counte books za quire 4 za intelejensia,
 
Kama sisi Tanzania 🇹🇿 tumelijua hilo, iweje liwe jambo geni kwa Russia 🇷🇺?
Unaweza kujua na usijue namna ya kujinasua kwasababu uliingia vitani kibabe na sasa unaona aibu kutangaza umeshindwa. Hilo la kwanza.

Jambo la pili urusi atakomaa hata kama anapata hasara ilimradi adui yake USA asimsogelew karibu. Maana yake akitangaza kushindwa tu.. Mmarwkani atakuwa karibu yake kama NMB.
 
Eti kama NMB, vijana mna maneno sana..
 
Putin ana nyuklia na huwa tunaambiwa hapa anatumia mgambo tu yale majeshi yake halisi hajayagusa. Yaani na yeye anacheza cheza na NATO kupitia Ukraine. Au ni uongo?
 
Sijui mmekatwa vichwa?

Makanali 100 wa Urusi wameteketea na Misiba na mazishi Yao tunaoneshwa kwenye TV halafu unaropoka eti Russia hajatumia Majeshi Yake? Majeshi ya Urusi + Chechen Soldiers + Wagner fighters + DPR Fighters + LPR Fighters wote kwa Pamoja wako bega kwa bega wanapambana na Majeshi ya Comedian ambaye anapewa Silaha kiduchu Tena za Mgao na bado anawajambisha. Mpaka Sasa,Russia haijateka Donbass yote (Luhansk + Dotnensk). Wamefanikiwa Kuitena Luhansk TU. Kila wakisogea Mji mkuu was Jimbo la Dotnensk wa Krymatonsk wanafekwa Nyuma. Tangu HIMMARS ziingie nchini Ukraine siku 30 zilizopita,Urusi imeteka 10km Kule Dotnensk na 3km Kule Izyum na Kupoteza 38Km Kule Kherson.

Ukweli wa hii vita Ni kwamba,Mwanzoni mwa Vita,Urusi alifanikiwa kuyateka maeneo mengi ya Ukraine kwa haraka kwasababu Ukraine haikuwa na Silaha hata za kupiga 50km. Sasa tunajionea baada ya Ukraine Kupewa Silaha kiduchu kutoka nchi za Magharibi,Russia ameshindwa Kuteka maeneo mapya kwa Uharaka zaidi Kama ilivyokuwa mwanzo. Hii inaonesha Licha ya mpaka Sasa Urusi kuwa na Silaha Nyingi na Wanajeshi wengi kuliko Ukraine,lakini Silaha alizopewa Ukraine zimeonesha ufanisi mkubwa Sana. Mpaka Sasa Urusi ingelikuwa imeshateka miji yote ya Ukraine ikiwemo Kyiv. Lakini Mambo Ni tofauti kabisa. Hata Donbass (Russian Speaking Provinces) ambazo zipo 45Km kutoka mpaka wa Urusi bado Urusi imeshindwa kuziteka.
 
Hii ripot umitoa wapi bwana andunje maripol ilichukuliwa kipindi silaha nyingi zimeshafika tyri Ukrein kuanzia jevelin, howitzer na vifaru vingi mkasifia sana Ila mwisho eneo likabebwa wakaja donest wakabeba saivi wanamalizia donbase yote na kharvik mashambulizi yashaanza kuurejesha uwoo mjii nyie bwabwajeni haitabadilisha chochote
 
Mambo ya kukatwa vichwa achana nayo we tuhabarishe kuhusu hali ya Urusi kijeshi, Urusi ipo katika hali gani kijeshi? Bado ina nguvu au ina hali mbaya? Maana kavita nako kana muda sasa hakaishi wala hakavuki mipaka.
 
Hii ripot umitoa wapi bwana andunje maripol ilichukuliwa kipindi silaha nyingi zimeshafika tyri Ukrein kuanzia jevelin, howitzer na vifaru vingi mkasifia sana Ila mwisho eneo likabebwa wakaja donest wakabeba saivi wanamalizia donbase yote na kharvik mashambulizi yashaanza kuurejesha uwoo mjii nyie bwabwajeni haitabadilisha chochote
Wagner group wamefyekwa huko Ukraine ss hivi wanahangaika kwenye majela ya Urusi kusaka wapiganaji

Ndicho nachokiona, Marekani anatumia misaada kidogo kidogo lengo ni Ukraine asishinde wala asipigwe knock out, akiona anazama anamuibua akiona anapata hewa anamuacha.

lengo kuu la mmarekani kutuma misaada kidogo kidogo ni kuirefusha vita iwe ndefu ili akusanye intelejensia , Mmarekani saizi yupo na daftari lake anakusanya intelejensia kuhusu mbinu za vita za urusi, udhaifu wake, Loyalty ya wanajeshi, uvumilivu, anavyokabiliana na vikwazo, reaction za Putin, n.k. kwa sasa kaenda mbali zaidi hata silaha anazowatumia Ukraine yeye ndie anaeminya rimoti ya kuzivyatua huku akifatilia kwa makini response ya Urusi.

Hii vita kwa mmarekani kaamua kuitumia Ukraine kama darasa la kumsoma Urusi, wala hana haraka kabisa, Hii vita hadi iishe ni mpaka Marekan awe kachukua notes za kutosha kajaza counter books za quire 4 za intelejensia kumhusu Urusi.

Kiufupi Urusi anatumika, asahau kabisa kuhusu ushindi,

Mbaya zaidi mrusi aliingia vitani kibabe na sasa anaona aibu kufunga virago maana itaonekana ameshindwa, atakomaa kibishi hata kama anapata hasara ili asichekwe, muda huu ukifika maisha yatakuwa magumu sana kwa warusi na yatakuwa yamewafika shingoni na hapa kitachotokea ni majaribio ya mapinduzi huku nako Ukraine wakijaziwa misaada tofauti na sasa,.

Ila mwisho wa vita hii nae Ukraine atakuwa kashajilimbikizia madeni kibao na hapa ndipo marekani anakuwa amenunua utiifu kutoka Ukraine katika kutekeleza mikakati yake, misaada hii ndio hela ya kuununua utiifu (loyalty) ya Ukraine.
Siyo kweli mkabisa! Hii vita si kwamba ukraine imeshindwa bali Marekani imeshindwa vibaya!! Mahesabu ya vMarekani ni kwamba Urusi isingehimili vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na hivyo isingeweza kuendelea na vita!! Kinyume na matarajio ni kwamba vikwazo havikuiathiri sana kiuchumi urusi na hivyo kuweza kuendelea na vita!! Pia Marekani na nchi za ulaya magharibi zimeumia sana kiuchumi kutokana na vikwazo vyao wenyewe na hazina hamu tena na vita hii. Vyombo vya habari vya magharibi vimeshaacha kushabikia na kuandika habari za vita hii maana hazina "habari nzuri" za kuandika!! Ni kwamba Marekani anashindwa hii vita na taratibu wanamtafutia kona Zelensky wamtwike zigo lote la lawama!! Ujue kuwa Marekani amejiandaa na hii vita kwa kuiandaa ukraine kwa miaka 8 ikiwa inapewa silaha na mafunzo lakini haijafua kitu!!
 
Ndicho nachokiona, Marekani anatumia misaada kidogo kidogo lengo ni Ukraine asishinde wala asipigwe knock out, akiona anazama anamuibua akiona anapata hewa anamuacha.

lengo kuu la mmarekani kutuma misaada kidogo kidogo ni kuirefusha vita iwe ndefu ili akusanye intelejensia , Mmarekani saizi yupo na daftari lake anakusanya intelejensia kuhusu mbinu za vita za urusi, udhaifu wake, Loyalty ya wanajeshi, uvumilivu, anavyokabiliana na vikwazo, reaction za Putin, n.k. kwa sasa kaenda mbali zaidi hata silaha anazowatumia Ukraine yeye ndie anaeminya rimoti ya kuzivyatua huku akifatilia kwa makini response ya Urusi.

Hii vita kwa mmarekani kaamua kuitumia Ukraine kama darasa la kumsoma Urusi, wala hana haraka kabisa, Hii vita hadi iishe ni mpaka Marekan awe kachukua notes za kutosha kajaza counter books za quire 4 za intelejensia kumhusu Urusi.

Kiufupi Urusi anatumika, asahau kabisa kuhusu ushindi,

Mbaya zaidi mrusi aliingia vitani kibabe na sasa anaona aibu kufunga virago maana itaonekana ameshindwa, atakomaa kibishi hata kama anapata hasara ili asichekwe, muda huu ukifika maisha yatakuwa magumu sana kwa warusi na yatakuwa yamewafika shingoni na hapa kitachotokea ni majaribio ya mapinduzi huku nako Ukraine wakijaziwa misaada tofauti na sasa,.

Ila mwisho wa vita hii nae Ukraine atakuwa kashajilimbikizia madeni kibao na hapa ndipo marekani anakuwa amenunua utiifu kutoka Ukraine katika kutekeleza mikakati yake, misaada hii ndio hela ya kuununua utiifu (loyalty) ya Ukraine.
Huwezi kusema marekani inatoa msaada kiduchu!! Mpaka sasa marekani imeshatoa zaidi ya dola bilioni 60!! Huo ni msaada kiduchu!!! Ni zaidi ya bajeti ya Tanzania kwa miaka mitatu!! Halafu bila aibu unasema ni msaada kiduchu!!!
 
Back
Top Bottom