Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Baadhi ya benki za Marekani ambazo hazitaki tena wateja kuweka akiba
Benki zaomba wateja wake kuweka akiba zao kwingineko.
Baadhi ya benki tayari zimeanza kukataza wateja wake kuweka pesa zao benki.
Wateja wa moja ya benki ya kubwa Marekani ya JPMorgan ndio wa hivi karibuni kukumbana na tukio hili ambalo sio nla kawaida.
Benki hiyo iliwaomba wateja wake kuweka akiba zao kwingineko.
Kama anavyoelezea mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Jamie Dimon, benki hiyo imeomba baadhi ya kampuni zenye kiasi kikubwa cha pesa ilizoweka katika benki hiyo kuzihamisha kwingineko, na kupunguza pesa inazowekea wateja kwa dola bilioni 200.
Kampuni ya JPMorgan ikiwa miongoni mwa benki kubwa Marekani haikusazwa katika jinamizi hili.
"Benki kubwa nchini humo zinapesa nyingi kiasi kwamba baadhi zimeanza kukataza wateja kuweka pesa zao na pia kuna uwezekano mkubwa benki au mashirika mengine ya kifedha yakaanza kuchukua hatua hiyo," amesema Nathan Stovall, mtaalamu wa mifumo ya fedha Marekani, alipozungumza na BBC Mundo.
Ilifikaji hatua ya benki kukataa pesa?
"Hakujawahi kutokea hali kama hii kabla. Hatujawahi kupitia kitu kama hicho," amesema Stovall."Tunachopitia sasa hivi ni kinyume na wakati kuna pesa kidogo katika mzunguko wa fedha. Kawaida, uchumi unapoporomoka sana, pesa taslim inakuwa adimu kupatikana na benki hufanya kila namna kupata pesa. Lakini wakati wa janga, kinyume chake ndicho kinachotokea. Benki zina pesa nyingi ambazo hazina faida kwao. "
Kawaida, benki huwa na shauku ya kupokea pesa, kwasababu wakiwa na hizo pesa wanaweza kutoa mikopo na kupata riba. Na riba ni sehemu ya biashara.
Lakini sasa faida ambayo benki zilikuwa zinapata kwasababu ya riba imepotea kutokana na janga.
Sasa hivi watu hawataki mikopo na hatua hiyo inaumiza sana benki.
Riba iliyowekwa na benki kuu Marekani imekuwa sufuri tangu mwezi Machi, hatua ambayo ililenga kuhamasisha watu kutumia pesa na kuendeleza mzunguko wa fedha lakini pia ni hatua ambayo imeumiza sana wakopeshaji.
Na matokeo ya janga la corona ni kwamba hitaji la mikopo limepungua sana.
Wasiwasi wa kutojua janga hili litaisha lini na uchumi kuimarika ni jambo ambalo wengi wanaliangazia kwa tahadhari sana na matokeo yake ni kwamba wanaotaka kukopa wamekuwa wachache.
Riba iliyowekwa na benki kuu Marekani imekuwa sufuri tangu mwezi Machi.
Matokeo yake, benki ya JPMorgan na Benki kuu ya Marekani na Citigroup zimepokea pesa nyingi kutoka kwa wateja zaidi ya dola trilioni 1 mwaka 2020 ambazo wateja waliziweka huku wanaochukua mkopo benki wakipungua sana.
Sasa basi kilichotokea, akiba inayowekwa benki imeongezeka. "Watu wameshikilia madola yao benki yaani hakuna anayetaka kutumia pesa zake," Stovall amesema.
Athari yake kwa benki na watu ni gani?
Stovall anaamini kwamba "mfumo wa fedha uko imara" na wala haupo hatarini. "Suala la kuangaziwa hapa ni kiwango cha faida kinachoweza kupatikana"Wataalamu wanaamini kwamba "benki kubwa zina njia nyingi tu za kufanya biashara" na haziamini kwamba serikali mpya inayoongozwa na Joe Biden itachangia kufikiwa kwa makubaliano fulani katika suala la udhibiti.
"Usalama wa mfumo uliopo ndio kipaumbele kwa serikali, ambayo inataka benki kuwa katika nafasi ya kutoa mikopo na kuimarisha uchumi na bila shaka benki pia ziko radhi katika hilo.
Lakini je vipi kwa wateja iwapo itafika mahali waone hawana sehemu ya kuweka pesa zao?
"Baadhi ya benki zinaweza kuwaambia wateja watafute sehemu nyingine ya kuhifadhi pesa zao, lakini lazima kutakuwa na mtu ambaye yuko tayari kupokea pesa," Stovall amebashiri.
Riba ya chini inapunguza faida kwa watu wanaoweka akiba yao benki.
Riba ya chini inapunguza faida kwa watu wanaoweka akiba yao benki.
Ukweli ni kwamba wale wanaoathirika na hatua hii zaidi ni wateja ambao wameweka akiba zao benki kwasababu hakuna faida wanayopata na kulingana na utabiri hili halina uwezekano wa kubadilika hivi karibuni.
Na pia ameonya kwamba wanaoweka akiba zao kidogo kidogo benki huenda wakaanza kutafuta sehemu zingine ambako pesa zao zinaweza kuzaana na kujikuta wamejiingiza katika pesa za mtandaoni kama vile bitcoin kwasababu inaonekana kuwa na faida.
Hivi punde tutawasiliana na ripota wetu waishio Marekani ndugu Kiranga na Nyani Ngabu kujua zaidi hali halisi