Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Ukraine na Ulaya wamejifunza kwa uchungu sana, Marekani yawakataa

Marekani sio mshirika wa kutegemewa kama anapata kidogo kuliko anachotoa kwako ila ikiwa anapata kikubwa marekani hata ruhusu hara Inzi watue kwako..

Case study ni israel na marekani.. hata israel akitukanwa tu Marekani kuanzia Rais hadi maseneta watatoa matamko maana yake Israel ni moyo wa pili wa marekani kwani anafaidika pakubwa direct and in direct

Ikirushwa hata roket moja Israel marekani atapeleka manowari za kivita israel

Sasa hao Euro na ukraine marekani anafaidika padogo sana na wao wanafaidika pakubwa kutoka marekani ndo maana unaona trump kawaambia kuwa wao wanauza bidhaa zao marekani ila hawataki kununua bidhaa za marekani wananunua china so maana yake marekani hafaidiki na ushirika wao.. ndo maana anachimba mkwara ..
 
Mkuu Xi Jinping, keep it up kwa
Uchambuzi wq Medani za Kimataifa.
 
Hivi mbona sijawahi kusikia shirika la misaada la Urusi? Lakini pia mbona sijawahi kusikia shirika la misaada la China? Walau Japan kuna JICA na Sweden kuna SIDA, ila hao giants Urusi na China wao ni maneno tu, misaada aaaah!
Hayo mashirika ni kwa maslahi mapana kwa hizo nchi za Magharibi na usije kufikiri kuwa wanawapenda sana na kuwaonea huruma, LA HASHA, hiyo ni ndoana ya kukuvua wewe na pia fimbo ya kukuchapia inapobidi. Nadhani wenye D 2 wamenielewa
 
Rudi kijiweni wakakuongezee ujinga
 
Mbona kama unaleta porojo!? Ukriane anapambana na wavamizi waliovamia nchi yake, na si kinyume chake!
 
Very well said
 
Falme gani zimeijaribu Urusi zikapotea? Ukraine iliivamia Urusi??
 
Umesema vyema

Urusi ni lidude fulani hivi ambalo NATO wamekubali kusanda

Kama mkuu wao Marekani kakiri Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Poland n.k wao ni nani
Urusi inayotumia hadi wanajeshi wa Korea Kaskazini ya Kim Kiduku na kuchukua silaha kutoka China??
 
Dunia ya balance of power ya USSR babu zako walikuwa wanavaa suruali zenye matobo na viraka kwenye makalio, ilikuwa dunia ya hovyo sana ndio maana USSR ilianguka na Western order ikachukua ushawishi wa dunia.
Dunia yenye ushawishi mkubwa wa China itakuwa mbaya sana pia.
 
Huu ni uongo mkubwa na propaganda zinazoipunguza historia yote ya Marekani kuwa Historia ya Trump tu.
 
Amekuwa mshirika wao mzuri kwa miaka 80 iliyopita. Ulaya na nchi kama Korea na Japan wanatakiwa kuwa na shukrani sana.
 
Hayo mashirika ni kwa maslahi mapana kwa hizo nchi za Magharibi na usije kufikiri kuwa wanawapenda sana na kuwaonea huruma, LA HASHA, hiyo ni ndoana ya kukuvua wewe na pia fimbo ya kukuchapia inapobidi. Nadhani wenye D 2 wamenielewa
Hao wa Magharibi huwa wanatulazimisha kupokea misaada au huwa tunawafuata kuwaomba?
 
Sera ya mambo ya nje ya marekani imekaa kinyonyaji zaidi kwa mataifa mengine. Ulaya na ujanja wao wote nao wametekwa na ujinga wa Marekani.

Ni vile Afrika hatuna malengo na uzalendo ila kipindi hiki ambapo dunia imechangamka, tulitakiwa kujitathmini na tuchukue hatua kujitoa kwenye makucha ya huyu mnyonyaji.

Traore anajaribu, ngoja tuone kama atafanikiwa au naye atawindwa kumzimisha.
 
Africa tuna shida sana. Ujinga na kusalitiana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ