State Propaganda
JF-Expert Member
- Apr 25, 2024
- 542
- 1,286
The Europeans are now experiencing what it truly means to be friends and allies of the United States😂😂😂
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Marekani sio mshirika wa kutegemewa kama anapata kidogo kuliko anachotoa kwako ila ikiwa anapata kikubwa marekani hata ruhusu hara Inzi watue kwako..Mwaka 1968 aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje ya Marekani Henry Kissinger alisema:
"Inaweza kuwa hatari kuwa adui wa Marekani, lakini kuwa rafiki wa Marekani ni majanga."
– Henry Kissinger
Na Marekani imethibitisha kuwa Kissinger alikuwa sahihi. Mara kwa mara, Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Zamu hii Ukraine na Ulaya wamejifunza.
Akizungumza na washirika wa NATO mjini Brussel, Belgium, Waziri wa Ulinzi wa Marekani alitoa matamshi ambayo naamini mpaka sasa Zelensky na viongozi wa Ulaya hawaamini macho yao.
"Hakuna uanachama wa NATO kwa Ukraine"
"Hakuna vikosi vya Marekani kwenda nchini Ukraine"
"Hakuna askari wa NATO kwenda nchini Ukraine. Lakini nchi za Ulaya zinaweza kutuma wanajeshi wao wenyewe.”
"Lazima tuanze kwa kutambua kwamba kurudishwa kwa mipaka ya Ukraine ya kabla ya 2014 ni lengo lisilowezekana, kufuatia lengo hili lisilowezekana kutaongeza muda wa vita na kusababisha mateso zaidi."
"Wanajeshi wowote wa Uingereza au Ulaya ambao walitumwa nchini Ukraine hawatakuwa chini ya misheni ya NATO au na dhamana ya kifungu cha 5 cha muungano huo, watategemea usaidizi kutoka kwa mataifa yanayoshiriki."
– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)
Na kama haitoshi naye Trump alifanya mazungumzo na Putin kwa saa 1:30 wakiafikiana kuwa watakutana Saudi Arabia mada kuu itakuwa suala la vita ya Ukraine.
Lakini wakati huohuo Trump alitumia dakika 10 tu kuongea kwenye simu na Zelensky.
Ukraine imepoteza mamia ya maelfu ya askari, mamilioni ya Waukraine wamekimbia nchi yao, wamepoteza karibu 20% ya ardhi yao na uchumi na miundombinu mingi kuharibiwa na Urusi.
Mkuu Xi Jinping, keep it up kwaKwa sasa taifa pekee ambalo Marekani analihofia duniani ni China.
"Pia tunakabiliwa na mshindani China anayeweza kutishia Marekani na maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacific. Marekani imekuwa ikibadilisha vipaumbele vyake vya kijeshi kwa kulinda nchi yake na kuizuia China."
– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)
Hapo kwa China wasipoteze muda na pesa Trump mwenyewe anajua hilo alijaribu 2018-2021 akafeli vibaya mno.
Hayo mashirika ni kwa maslahi mapana kwa hizo nchi za Magharibi na usije kufikiri kuwa wanawapenda sana na kuwaonea huruma, LA HASHA, hiyo ni ndoana ya kukuvua wewe na pia fimbo ya kukuchapia inapobidi. Nadhani wenye D 2 wamenielewaHivi mbona sijawahi kusikia shirika la misaada la Urusi? Lakini pia mbona sijawahi kusikia shirika la misaada la China? Walau Japan kuna JICA na Sweden kuna SIDA, ila hao giants Urusi na China wao ni maneno tu, misaada aaaah!
Rudi kijiweni wakakuongezee ujingahv unajuwa hali ya Urusi sas hv ? Urusi wamefikia hatua ya kusema liwalo na liwe ika sio kwamba ukimya wao unamaanisha wapo vzr , Trump katumia busara , Hii vita imempa fursa nying China na lzn wafanye maamuz kama haya ili China asiwapige gap kubwa , kipind cha hii vita ndo China kapata ushawishi mkubwa baran kwake Asia ambako wengi walikiwa hawamtaki pia Ndo kipind China kawatoa rasmi wazungu huku Afrika , pia ndo kipind China kaanza tawala soko la Ulaya , pia ndo kipind China amepanya option ya kuiangusha USA kwa kuitumia Urusi , so ni lzm Trump arud nyuma aweke sw ila bila uwepo wa China kama superpower bas USA angemvagaa Urusi na kumdunda vzr maana hata kama angerud nyuma bas bado angekuwa kileleni maana kutoka yeye hadi mtu wa tatu anamzid krb mara 2 ila huyu wa pili yake yupo makalion , USA akidelay kdg China anakaa Mbele zaid , so uwepo wa China km mshindani wa USA ndo umefanya Trump afanye hayo maamuz
Mbona kama unaleta porojo!? Ukriane anapambana na wavamizi waliovamia nchi yake, na si kinyume chake!Wamempiga nyuki busu wakajua maumivu yake alafu wewe unashauri waendelee na huu mchezo?
Tangu 2014 nawaambia wajinga kama wewe kuingia vitani na Urusi ni sawa na kudumbukia kwenye tanuru la kuyeyusha vyuma.
Falme nyingi zimeijaribu urusi zikapotea usije kufikiri marekani ni mjinga
Very well saidMarekani sio mshirika wa kutegemewa kama anapata kidogo kuliko anachotoa kwako ila ikiwa anapata kikubwa marekani hata ruhusu hara Inzi watue kwako..
Case study ni israel na marekani.. hata israel akitukanwa tu Marekani kuanzia Rais hadi maseneta watatoa matamko maana yake Israel ni moyo wa pili wa marekani kwani anafaidika pakubwa direct and in direct
Ikirushwa hata roket moja Israel marekani atapeleka manowari za kivita israel
Sasa hao Euro na ukraine marekani anafaidika padogo sana na wao wanafaidika pakubwa kutoka marekani ndo maana unaona trump kawaambia kuwa wao wanauza bidhaa zao marekani ila hawataki kununua bidhaa za marekani wananunua china so maana yake marekani hafaidiki na ushirika wao.. ndo maana anachimba mkwara ..
Yeah, Trump na Putin sasa wanaungana dhidi yake.Maskini Zele kwisha habari yake!
Falme gani zimeijaribu Urusi zikapotea? Ukraine iliivamia Urusi??Wamempiga nyuki busu wakajua maumivu yake alafu wewe unashauri waendelee na huu mchezo?
Tangu 2014 nawaambia wajinga kama wewe kuingia vitani na Urusi ni sawa na kudumbukia kwenye tanuru la kuyeyusha vyuma.
Falme nyingi zimeijaribu urusi zikapotea usije kufikiri marekani ni mjinga
Mlimshauri afanyaje?Zelensky tulimshauri mapema akagoma, wacha tu apewe za uso
Urusi inayotumia hadi wanajeshi wa Korea Kaskazini ya Kim Kiduku na kuchukua silaha kutoka China??Umesema vyema
Urusi ni lidude fulani hivi ambalo NATO wamekubali kusanda
Kama mkuu wao Marekani kakiri Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Poland n.k wao ni nani
Dunia ya balance of power ya USSR babu zako walikuwa wanavaa suruali zenye matobo na viraka kwenye makalio, ilikuwa dunia ya hovyo sana ndio maana USSR ilianguka na Western order ikachukua ushawishi wa dunia.Tunaposema dunia inahitaji balance of power watu wawe wanatuelewa kuwa kuifanya dunia iendeshwe na taifa moja matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona tangu Trump aapishwe
Watu huwa wanakuwa wajinga kuisifu sifu Marekani sijui superpower ni kosa kubwa sana. Umeona wamesitisha misaada kama dawa za ARV waathirika ambao walikuwa wanaisifu Marekani superpower wameanza kutoa vilio
Ndio mana tunataka mataifa mengine ya kuichallenge kiuchumi, kiteknolojia, nguvu za kijeshi na misaada ili Marekani isijione bila yeye mambo hayaendi
Tayari Mrusi kashaonyesha hilo hapo Ukraine, Marekani katulizwa kakaa. Na China inafanya hivyo kiuchumi, kiteknolojia na kupitia foreign aids
Hiki ndicho tunaita balance of power tunaihitaji sana hii kitu duniani, ilipotea tangu kuanguka kwa Soviet Union miaka ya mwanzoni mwa 1990
Huu ni uongo mkubwa na propaganda zinazoipunguza historia yote ya Marekani kuwa Historia ya Trump tu.Ni wakati wa nchi za Ulaya kuwa na ushirikiano na China na Russia dunia ya sasa inahitaji win-win cooperation sio sera za Marekani za win-lose cooperation
Tatizo la nchi za Ulaya zimekubali kuwa U.S vassal states, wamekubali internal na foreign policies zao zitegemee sera za Marekani wanaumia sana, ndicho anachopitia Japan, South Korea, Canada, Australia na U.S vassal states nyingine.
Leo uchumi wa Ujerumani unaotegemea viwanda, uzalishaji viwandani umeporomoka kwa sababu ya kupanda kwa gharama za nishati ambazo awali walikuwa wananunua Urusi kwa bei rahisi, Marekani akalipua Nord Stream pipeline ili awauzie LNG kwa bei kubwa
Mafuta wanauziwa na India ambayo nayo inanunua Urusi na kuwauzia kama third party kwa gharama kubwa
Na bado Marekani inawatisha kwa kuwapandishia tariffs bidhaa zao.
Mchina aliona mbali kafanya juu chini kuhakikisha kuwa soko lake kubwa la bidhaa lisitegemee Marekani, kwa sasa soko kubwa la China ni Global South countries.
Ukiwa trade partner mkubwa wa Marekani lazima akutese sana kama Canada, Mexico na Japan zinavyoteswa na tariffs.
Siku hizi Mchina anafanya tit for tat Marekani akitia tariffs na yeye anampandishia tariffs kwa sababu soko la Marekani sio kipaumbele kwake.
Marekani ni kwenda naye kibabe kama Urusi na China zinavyofanya
Hao wa Magharibi huwa wanatulazimisha kupokea misaada au huwa tunawafuata kuwaomba?Hayo mashirika ni kwa maslahi mapana kwa hizo nchi za Magharibi na usije kufikiri kuwa wanawapenda sana na kuwaonea huruma, LA HASHA, hiyo ni ndoana ya kukuvua wewe na pia fimbo ya kukuchapia inapobidi. Nadhani wenye D 2 wamenielewa
Zaidi ya 30% ya bajeti yetu inaihitajiMisaada ya Nini wewe,nyie ccm bn
Hawajatulazimisha na wala hatujawaomba. Ukishakuwa Masikini halafu mtu anakuletea msaada nadhani utatamani aendelee kukupa msaada huo.Hao wa Magharibi huwa wanatulazimisha kupokea misaada au huwa tunawafuata kuwaomba?
Africa tuna shida sana. Ujinga na kusalitianaSera ya mambo ya nje ya marekani imekaa kinyonyaji zaidi kwa mataifa mengine. Ulaya na ujanja wao wote nao wametekwa na ujinga wa Marekani.
Ni vile Afrika hatuna malengo na uzalendo ila kipindi hiki ambapo dunia imechangamka, tulitakiwa kujitathmini na tuchukue hatua kujitoa kwenye makucha ya huyu mnyonyaji.
Traore anajaribu, ngoja tuone kama atafanikiwa au naye atawindwa kumzimisha.