Marekani imetangaza kuanza kufuta viza za wanafunzi wa China

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Marekani imetangaza kuwa itaanza kufuta viza za wanafunzi kutoka China, hususan wale wanaohusishwa na Chama cha Kikomunisti cha China au wanaosomea fani zinazotajwa kuwa nyeti kwa usalama wa taifa.

Marekani imetangaza kuwa itaanza kufuta viza za wanafunzi kutoka China,hususan wale wanaohusishwa na Chama cha Kikomunisti cha China au wanaosomea fani zinazotajwa kuwa nyeti kwa usalama wa taifa.

Tangazo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio siku ya Jumatano, ambaye pia amesema kuwa masharti ya viza yatapitiwa upya ili kuongeza uchunguzi kwa maombi kutoka China na Hong Kong.

Tangazo hilo linakuja siku moja baada ya kuripotiwa kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesitisha kwa muda miadi mipya kwa wanafunzi na waombaji wa viza za kubadilishana.

Mpango huo unatajwa kuwa sehemu yajuhudi za utawala wa Rais Donald Trump za kuimarisha udhibiti wa uhamiaji, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uchunguzi wa mitandao ya kijamii kwa wanafunzi wa kimataifa, kufuta viza, na kuharakisha hatua za kuwarejesha makwao.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Elimu ya Kimataifa (IIE), China ilikuwa na idadi ya pili kwa ukubwa ya wanafunzi wa kimataifa waliokuwa wakisomea Marekani mwaka 2023/2024, wakiwa 277,398.

Hadi sasa, ubalozi wa China mjini Washington haujatoa kauli rasmi kuhusiana na tangazo hilo. Wachambuzi wanasema hatua hii huenda ikaathiri uhusiano wa kielimu na kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili yenye mvutano wa muda mrefu.
 
Unakuwaje na wanafunzi 277,398 at a time ndani ya nchi nyingine moja? That's too much hao wachina nao wawe japo na aibu kidogo!
Ata Ulaya kupo ivyo ivyo Mkuu Mchina anasaka Elimu Ulaya yote kila Chuo Wachina wamejaa kinoma noma!!!

Vijana wa Kizungu wapo Baaa wanapata moja mbili !!!

wamelewa na ukubwa wao na propaganda zao !!

wkt wenzao wanakuja kwa Kasi ya umeme. Na wingi wao .
 
Unakuwaje na wanafunzi 277,398 at a time ndani ya nchi nyingine moja? That's too much hao wachina nao wawe japo na aibu kidogo!
Wachina wanagombania visa vya kwenda nchi za magharibi
 
Mmarekani akasome nini China wakati wachina wenyewe ni wapiga chabo tu kisha wanatengeneza bidhaa feki.
Shida ni kuwa wazungu wamebweteka sana wakati wachina ndo wapo mchakamchaka. Wanabaki kulalamika ya kuwa wachina wanawaibia teknolojia.
 
Unakuwaje na wanafunzi 277,398 at a time ndani ya nchi nyingine moja? That's too much hao wachina nao wawe japo na aibu kidogo!
Kwamba hawataki elimu bora?
 
Unakuwaje na wanafunzi 277,398 at a time ndani ya nchi nyingine moja? That's too much hao wachina nao wawe japo na aibu kidogo!
Aibu utaona wewe lkn sio Mchina..... yaaaaniiiii ni shidaaa
 
Marekani imetangaza kuwa itaanza kufuta viza za wanafunzi kutoka China, hususan wale wanaohusishwa na Chama cha Kikomunisti cha China au wanaosomea fani zinazotajwa kuwa nyeti kwa usalama wa taifa.

Marekani imetangaza kuwa itaanza kufuta viza za wanafunzi kutoka China,hususan wale wanaohusishwa na Chama cha Kikomunisti cha China au wanaosomea fani zinazotajwa kuwa nyeti kwa usalama wa taifa.

Tangazo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio siku ya Jumatano, ambaye pia amesema kuwa masharti ya viza yatapitiwa upya ili kuongeza uchunguzi kwa maombi kutoka China na Hong Kong.

Tangazo hilo linakuja siku moja baada ya kuripotiwa kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesitisha kwa muda miadi mipya kwa wanafunzi na waombaji wa viza za kubadilishana.

Mpango huo unatajwa kuwa sehemu yajuhudi za utawala wa Rais Donald Trump za kuimarisha udhibiti wa uhamiaji, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uchunguzi wa mitandao ya kijamii kwa wanafunzi wa kimataifa, kufuta viza, na kuharakisha hatua za kuwarejesha makwao.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Elimu ya Kimataifa (IIE), China ilikuwa na idadi ya pili kwa ukubwa ya wanafunzi wa kimataifa waliokuwa wakisomea Marekani mwaka 2023/2024, wakiwa 277,398.

Hadi sasa, ubalozi wa China mjini Washington haujatoa kauli rasmi kuhusiana na tangazo hilo. Wachambuzi wanasema hatua hii huenda ikaathiri uhusiano wa kielimu na kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili yenye mvutano wa muda mrefu.
Cabinet ya trump naona imekaa shaghala baghala kila mtu anayoyake
 
Back
Top Bottom