Ndio maana nasema NAONGEA NA TUTUSA WA STORI ZA VIJIWENI.
-Malaysia na Indonesia uwekezaji wao mkubwa ni ushirika wa China na Qatar.Nimezifuatilia vema hizi nchi.
Wachina na Qatar pale wamefanya massive investments tena sio mchezo.
-China uchumi wake ni closed economy nikimaanisha sekta nyingi za uchumi zinamilikiwa na serikali.
90% ya viwanda vya China ni government owned ama government subsidies.Mwaka 1992 China inafanya mageuzi ya uchumi ilijenga viwanda takriban elfu 45 vyote ni state owned industries.Ndio maana HAKUNA kitu USA atafanya cha kumuangusha China.Refer trade war ya 2018,hivi unajua malipizo ya US kui ban Google isitumike na Huawei kuliiletea sana madhara USA ya kiuchumi!?
Rare earth metals 80% zinazalishwa China,China alipiga ban zisiingie USA,vipuli na ghafi nyingi za boti na vyuma USA anatoa China kwa cheap price,China alipiga ban visiende USA.Viwanda vingi vilipunguza uzalishaji hapo USA kwa kukosa malighafi kutoka China.
Na USA amewekeza China kwasababu China kuna soko kubwa kulingana na population ya China pia kubwa zaidi China kuna highly skilled labours ambao ni cheap in salary.
USA akijifanya afunge uwekezaji wake China hivyo viwanda na uwekezaji mwingine vyote vitahodhiwa na serikali ya China na kumletea yeye ushindani zaidi.
Mbona hatukuwaona hao Rothschild family kuiokoa USA na Kuikandamiza China!?
Hivi unajua kama China ana deni kwa USA la zaidi ya $3.6 trillions la treasury bill!??
Unajua hiyo ina nguvu gani kiuchumi kwa China na hasara gani kiuchumi kwa USA!!??
Mbona hiyo Rothschild family haikuja na kuiokoa USA dhidi ya hilo deni na kuiacha salama!?
Muda mwingine ndugu zanguni mukae muchunguze mambo kabla hamjamezeshana vichekesho huko vijiweni.