Marekani ina shida gani na Iran na Korea Kaskazini ?

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
6,406
Reaction score
12,736
Ningependa kujuzwa na wajuvi wa mambo na wataalam wa siasa za kimataifa katika hili swali langu.

Je, nchi ya Marekani ina shida gani na haya mataifa mawili Iran na Korea Kaskazini ? Kwa nini tawala mbalimbali za Marekani zinayatendea haya mataifa kama tishio kwa marekani ?

Maoni yangu binafsi:
Mimi binafsi sioni hilo tishio kama linavyo elezwa kwa haya mataifa mawili kwa marekani tofauti kidogo na China na Russia.

N.b:
Ningependa watakao changia wawe na utimamu wa akili. kebehi,kejeri na lugha yoyote isiyofaa hapa sio mahala pake.

Moderator uangalizi wako nauhitaji katika huu uzi.
 
Marekani ina mvutano na Iran na Korea Kaskazini kwa sababu ya masuala ya nyuklia, usalama, na siasa za kimataifa:

Sababu kuu
• Iran: Marekani inahofia mpango wake wa nyuklia, ufadhili wa makundi kama Hezbollah, ushawishi wake Mashariki ya Kati, na udhibiti wake wa Mlango wa Hormuz.

• Korea Kaskazini: Ina silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu, utawala wake unakiuka haki za binadamu, na ina mvutano na Korea Kusini, mshirika wa Marekani.
 
Hujapata kusikia the so referred to as Axis of Evils? Mihimili ya uovu ni hatari sana kwa dunia ya kistaarabu.
 
Fafanua mkuu kuhusu hiyo Axis of Evils
 
Tukianza na Iran, USA imekuwa iki-intefare masala ya ndani ya Iran hata kabila ya utawala WA sasa WA ayatollah(1979)

Makampuni ya magharibi (mfano BP) yalikuwa yanachimba mafuta katika njia ambayo hazikuwa Sawa.

Ufalme ulikuwa ni kama puppet

Iran iliwahi kufanya uchaguzi WA kidemokrasia na Mohammed Mosadeggh alichagukiwa kuwa waziri mkuu.

Huyu kama alikuwa ni tatizo kwao akaja kupinduliwa kazi ikiwa imefanywa na CIA na MI6 KAZI ikiwa imeongezwa na Kermit Roosevelt Jr, ufalme ukalejeshewa nguvu na serikali ya kidemokrasia ikapinduliwa na mafuta yakaendelea kutonufaisha wa-Iran

Baadae ya kuanguka serikali ya kidemokrasia kukaanza kuibuka harakati zinazoambatana na itikadi za dini kulingana na Hali nzima ya kimaisha na chuki iliyoambatana exploitation ya mafuta inayofanywa na UK na USA

Kwenye miaka 1970s uchumi ulikuwa ni mbaya na ufalme ulikuwa Una ubadilivu, na watu wengi walikuwa wanachukizwa pia nchi kuwa na karibu na nchi za magharibi.

Kwa uongozi lazima uwe kinyume na lazima kungekuwa UTAIFISHAJI WA kampuni za mafuta pasipo ku-serve interest za mataifa ya kigeni.

Baadae ya mapinduzi 1979 mataifa ya magharibi yakaanza kumuunga mkono Saddam Hussein kwenye vita vya Iran-Iraq, Kwa lengo pia ya kuondoa utawala mpya ya ayatollah

Kwa mantiki hiyo USA ilikuwa inatamani kuondoa utawala WA Iran maana hakuwai tena na control ya mafuta, lakini mapinduzi Yale yangeweza hari Kwa nchi zingine za Middle east maana ya mapinduzi ayatollah aliwahizima wananchi kwenye nchi za kiislamu kufanya mapinduzi na kuondoa tawala za zote za kifalme kwani ni puppet govs.

Na hapa ndipo tawala kama za Saudi Arabia, Iraq, Kuwait, Qatar, UAE zikaanza kuichukulia Iran kama ni tishio lakini pia Israel Kwa sababu Iran ilikuwa ni supporter WA PLO ya Yasser Arafat

Ili kujilinda na USA na hasa kutokana vita vya miaka minane lakini pia historia ya serikali ya kidemokrasia iliyopindiliwa 1953, Iran ilianza projects za space hasa za uundaji WA makombora na urutunishaji WA uranium (Iran wanadai ni Kwa matumizi ya kiraia)
 
Ningependa kujuzwa na wajuvi wa mambo na wataalam wa siasa za kimataifa katika hili swali langu.

Je, nchi ya Marekani ina shida gani na haya mataifa mawili Iran na Korea Kaskazini ? Kwa nini tawala mbalimbali za Marekani zinayatendea haya mataifa kama tishio kwa marekani ?

Maoni yangu binafsi:
Mimi binafsi sioni hilo tishio kama linavyo elezwa kwa haya mataifa mawili kwa marekani tofauti kidogo na China na Russia.

N.b:
Ningependa watakao changia wawe na utimamu wa akili. kebehi,kejeri na lugha yoyote isiyofaa hapa sio mahala pake.

Moderator uangalizi wako nauhitaji katika huu uzi.
No too late wameshindwa
 
Ugomvi wa iran na usa sio kingine bali ni hilo taifa la mchongo la israel
 
Sababu hata hazina kaana ,nchi iko America ila inapigania mambo ya nchi za Asia ,kamq sio umbea ni nn?

Marekani ni ambayo wananchi wake hawana akili wanapelekwa tu na Mayahudi ,wao wengi wamebaki kujipa uhru wa kijinga ; Pale Iran anahofia jamaa ana nyunklia anahatarisha usalama wa Israel ,huku korea ni hivyo hivyo.

Iran amekosa ushawishi wa awali kwenye makampuni yake tangu uingie huu utawala a kidini.
 
Tukianza na Iran, USA imekuwa iki-intefare masala ya ndani ya Iran hata kabila ya utawala WA sasa WA ayatollah(1979)

Makampuni ya magharibi (mfano BP) yalikuwa yanachimba mafuta katika njia ambayo hazikuwa Sawa.

Ufalme ulikuwa ni kama puppet

Iran iliwahi kufanya uchaguzi WA kidemokrasia na Mohammed Mosadeggh alichagukiwa kuwa waziri mkuu.

Huyu kama alikuwa ni tatizo kwao akaja kupinduliwa kazi ikiwa imefanywa na CIA na MI6 KAZI ikiwa imeongezwa na Kermit Roosevelt Jr, ufalme ukalejeshewa nguvu na serikali ya kidemokrasia ikapinduliwa na mafuta yakaendelea kutonufaisha wa-Iran

Baadae ya kuanguka serikali ya kidemokrasia kukaanza kuibuka harakati zinazoambatana na itikadi za dini kulingana na Hali nzima ya kimaisha na chuki iliyoambatana exploitation ya mafuta inayofanywa na UK na USA

Kwenye miaka 1970s uchumi ulikuwa ni mbaya na ufalme ulikuwa Una ubadilivu, na watu wengi walikuwa wanachukizwa pia nchi kuwa na karibu na nchi za magharibi.

Kwa uongozi lazima uwe kinyume na lazima kungekuwa UTAIFISHAJI WA kampuni za mafuta pasipo ku-serve interest za mataifa ya kigeni.

Baadae ya mapinduzi 1979 mataifa ya magharibi yakaanza kumuunga mkono Saddam Hussein kwenye vita vya Iran-Iraq, Kwa lengo pia ya kuondoa utawala mpya ya ayatollah

Kwa mantiki hiyo USA ilikuwa inatamani kuondoa utawala WA Iran maana hakuwai tena na control ya mafuta, lakini mapinduzi Yale yangeweza hari Kwa nchi zingine za Middle east maana ya mapinduzi ayatollah aliwahizima wananchi kwenye nchi za kiislamu kufanya mapinduzi na kuondoa tawala za zote za kifalme kwani ni puppet govs.

Na hapa ndipo tawala kama za Saudi Arabia, Iraq, Kuwait, Qatar, UAE zikaanza kuichukulia Iran kama ni tishio lakini pia Israel Kwa sababu Iran ilikuwa ni supporter WA PLO ya Yasser Arafat

Ili kujilinda na USA na hasa kutokana vita vya miaka minane lakini pia historia ya serikali ya kidemokrasia iliyopindiliwa 1953, Iran ilianza projects za space hasa za uundaji WA makombora na urutunishaji WA uranium (Iran wanadai ni Kwa matumizi ya kiraia)
Umechanganya mno mambo,suala ni shah kuwataka BP(uingereza),SHELL(Ufaransa) na kampuni la marekani kulipa mirabaha stahiki kwenye uchimbaji mafuta Iran,kwa ulafi wao wakaona Iran itanufaika,wakamsaidia ayatollah khomeini kupindua nchi waliingia nae mkataba wa kuchamba mafuta wa kihuni, ayatollah akasaini,akaingia ikulu,aka-apply taqiya(yaani kubali jambo hata kama baya kwako ukiwa dhaifu na ukipata nguvu kataa), ndiyo mwanzo wa uadui wa magharibi na Iran, ndiyo maana 1979 mapinduzi na vikwazo havikukawia
Kwa kiduku kunataka kufanana na Cuba, ujamaa na ubepari
Kwa Iran limeongezeka la uadui na israel na geopolitics za mashariki ya kati
 
Tukija Korea Kaskazini.

Kwa kipindi kirefu kwenye kipindi cha vita baridi USA ilifanya kitu kinaitwa operation condor ambayo ilifanya mapinduzi serikali nyingi za America kusini hasa zile zilizokuwa tishio Kwa maslahi ya US (nyingi nchi za kijamaa na ki-comunist).

Oparesheni za namna hii pia zilikuwa zinaendelea pia kwenye nchi za Asia.

Baadae ya Japan kusarenda Korea Kaskazini na Korea Kusini ziligawanywa na USSR (Kaskazini) na USA(kusini)

USA alitaka kuzuia kusambaa Kwa ukomunist asia hivyo akawahi upande WA kusini, kumbuka hata kusini ukomunist ulikuwa unaungwa mkono na wengi ndio maana hata USA ilisapoti viongozi madikteta kama Park Chung Hee

Hizi nchi zikaangia kwenye vita 1950-1953 amavyo viliisha Kwa kusitisha mapigano hapakuwa na mkataba WA Amani hivyo Korea zote bado zipo vitani.

Kwenye vita ya Korea, jeshi la us lilipiga mabomu mengi kuliko mabomu aliyodondosha kwenye WWII

Kama ilivyo kawaida rain wengi ndio waathirika, hapa ndipo Kim Il Sung (babu yake Kim Jung Un) alipoona kuna haha ya kuanzia kuwekeza kwenye kuwa na silaha za nyuklia kama njia za kujilinda.

Kwa maana hiyo ukomunist Kwa sasa sio ishu kabisa maana Vietnam ina serikali ya chama kimoja Ila inafanya biashara kubwa Tu makampuni ya USA na ni washirika sasa hivi.

North korea Kwanza hajaisujudia USA hivyo ni rahisi kuwa karibu na maadui WA USA kama China, Urusi na Iran, kumbuka Korea Kaskazini imepakana na China na Urusi

Wakati huo pia Korea Kaskazini inamiliki silaha za nyuklia na pia mara Kwa mara hujaribu makombora ya Masafa marefu ambayo USA inadai ni tishio Kwa washirika wake(Japan na S.korea) na Korea Kaskazini inasema inajilinda dhidi ya US
 
Marekani ina mvutano na Iran na Korea Kaskazini kwa sababu ya masuala ya nyuklia, usalama, na siasa za kimataifa:

Sababu kuu
• Iran: Marekani inahofia mpango wake wa nyuklia, ufadhili wa makundi kama Hezbollah, ushawishi wake Mashariki ya Kati, na udhibiti wake wa Mlango wa Hormuz.

• Korea Kaskazini: Ina silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu, utawala wake unakiuka haki za binadamu, na ina mvutano na Korea Kusini, mshirika wa Marekani.
Hoja ya kukiuka haki za binadamu ni hoja ya kipuuzi.
 
Marekani usipo endana na masilahi yake atakupa jina baya na mbaya zaidi kuna wapumbavu huwa wanaamini propaganda zake.
 
Ningependa kujuzwa na wajuvi wa mambo na wataalam wa siasa za kimataifa katika hili swali langu.

Je, nchi ya Marekani ina shida gani na haya mataifa mawili Iran na Korea Kaskazini ? Kwa nini tawala mbalimbali za Marekani zinayatendea haya mataifa kama tishio kwa marekani ?

Maoni yangu binafsi:
Mimi binafsi sioni hilo tishio kama linavyo elezwa kwa haya mataifa mawili kwa marekani tofauti kidogo na China na Russia.

N.b:
Ningependa watakao changia wawe na utimamu wa akili. kebehi,kejeri na lugha yoyote isiyofaa hapa sio mahala pake.

Moderator uangalizi wako nauhitaji katika huu uzi.
Korea Kaskazini na Iran siyo tishio kwa Marekani. Iran ni tishio kwa Israel Korea Kaskazini ilikuwa tishio kwa Korea Kusini.
 
Sina hakika na umri wako lakini utakua labda una miaka 50+ utakubaliana na mimi (unaweza pia kuuliza watu wazima kuhusu hili, just in case ) hadi miaka ya katikati ya 80, kulikuaga hakuna Islamic fundamentalist, hawa watu wameanza hasa baada ya Iran kua na amani, machafuko nchi mbalimbali duniani yakihusisha na dini hi yalianza, Iran akiwa kama chief financer wa haya mambo; mwendawazimu kama huyu sasa ndio eti amiliki silaha za nuclear, just imagine. Or put this way, una duka lako la vioo halafu kuna mwendawazimu ana kirungu karibu na duka lako, utakua na amani kweli? Wamiliki wa silaha za nuclear wapo wengi duniani nadhani hata Africa kusini wanazo but jumuia ya kimataifa wala haina time nao except hawa wendawazimu 2. India na Pakistan mara nyingi wakigombanaga, jumuia ya kimataifa huaga fasta inawapatanisha, Pakistan kuna mwendawazimu, hawachelewi kubonyeza button za nuclear, Iran utaishauri?
 
Ningependa kujuzwa na wajuvi wa mambo na wataalam wa siasa za kimataifa katika hili swali langu.

Je, nchi ya Marekani ina shida gani na haya mataifa mawili Iran na Korea Kaskazini ? Kwa nini tawala mbalimbali za Marekani zinayatendea haya mataifa kama tishio kwa marekani ?

Maoni yangu binafsi:
Mimi binafsi sioni hilo tishio kama linavyo elezwa kwa haya mataifa mawili kwa marekani tofauti kidogo na China na Russia.

N.b:
Ningependa watakao changia wawe na utimamu wa akili. kebehi,kejeri na lugha yoyote isiyofaa hapa sio mahala pake.

Moderator uangalizi wako nauhitaji katika huu uzi.
Iran akiwapa Hezbollah au Houthi missile yenye nyukilia unategemea nani atabaki salama? Wenzio wakishatamka "Allahu Akbar" akili zote zinahamia kwa wale bikira72 kinachofata nazani unakijiua
 
Back
Top Bottom