Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Hivi misaada huwa wanatoa kwa viongozi au sie wananchi? haya mambo ya vikwazo ni vitu ambavyo haviingii akilini kabisa.
Jaribu kuwauliza maafisa wa Iran watakupa habari yake, hata Makonda anajua vizuri hii kitu
 
Wajinga tu ndio mnababaika ila dunia ya sasa hivi hakuna nchi ina babaishwa na vikwazo vya wamarekani, yeye mwenyewe anapumulia mashine sasa hivi, akizubaa mchina huyu hapa kwa nyuma yake.

Hao Irani unafikiri wana hali mbaya kama mnavyotangazowa?
Pole sana mkuu, huko ni taasisi ndio inadeal na wewe wala sio pompeo au Trump yaan ni sawa uwe na kesi ya mauaji na hapa katikati majaji wote wakafa unadhani ndio mwisho wa kesi yako
 
Washughulikie Uchaguzi wao, wasitusumbue wao wameshindwa kufanya uchaguzi mpaka aibu, wanyamaze kabisa
 
Jaribu kuwauliza maafisa wa Iran watakupa habari yake, hata Makonda anajua vizuri hii kitu
Ndio nimeuliza misaada wanayotupa ni kwa ajili ya watu kama akina Makonda au ni kwa ajili ya wananchi? kwa sababu wanapositisha misaada au kuweka vikwazo wanaothirika zaidi ni mimi na wewe sio Makonda. Sasa sijui hapo wewe mwenzangu unafurahia vp na hivi vikwazo.

Hebu tizama hizo nchi zilizopigwa vikwazo unakuta viongozi wao wanaendelea kula maisha huku bado wameshikilia misimamo yao vilevile,sasa anayekomoka nani kama sio wananchi?
 
Upuuuuzi mtupu.

Wanahamasisha uhuru wa kujieleza, huku wameifungia acc ya twitter ya Trump.

Wanacho kihamasisha wao hawakiishi, wadeal na hali yao wanaiyoipitia sasa baada ya uchaguzi.
Wajinga sana hawa wasitusumbue, wameshindwa yakwao wanaleta usumbufu kwa wengine
 
Nikiziangalia sura zilizojazana NEC na kwa msajili wa vyama vya siasa kwa hakika wamejaa wazalendo watupu na wengi wao hata huko Marekani hawakujui...
The action is not simple as you see it. It has far reaching consequences. The European Union and UK will soon join the move.
 
Mbona Rais Trump amelalamika sana kuibiwa kura, wamefunga account zake ili asiwasiliane na watu wake, na hakuna mahakama, wala Vyombo vya uchunguzi vilivyochukua hatua yeyote hata kumsikiliza kama mwananchi wa kawaida licha yeye kua ni Raisi.

Watanzania wanaweza kumaliza changamoto zao wenyewe, washughulike Madai ya Rais Trump na watoe matokeo ya uchunguzi hazarani ili Dunia ijifunze kutoka kwao, kwa sasa Marekani haina uhalali wa kushauri wala kukemea nchi nyingene.waje wajifunze namna ya kufanya uchaguzi na kuheshimu viongozi.
 
Back
Top Bottom