Marekani kuipuuza Afrika kunatoa msukumo wa ushirikiano na umoja zaidi

Marekani kuipuuza Afrika kunatoa msukumo wa ushirikiano na umoja zaidi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
1747031697158.png

Wakati Marekani ikiendelea na mashambulizi dhidi ya biashara huria duniani, Afrika iko ni mmoja wa wahanga. Na sasa Rais Donald Trump wa Marekani amefungua medani ya kidiplomasia tena ambapo serikali yake inalenga balozi mbalimbali duniani kwa kile alichokiita Donald Trump kuitikisa sera ya mambo ya nje ya Marekani.

Hivi karibuni vyombo vya habari vya Marekani vilitangaza kuwa Bw. Donald Trump anapanga kufanya marekebisho makubwa zaidi kwenye sera ya mambo ya nje ya Marekani tangu mwaka 1789, hatua ambayo italeta mabadiliko makubwa kwenye mpangilio wa mkakati wa kidiplomasia wa kimataifa wa Marekani. Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Ulinzi ni nguzo mbili za sera ya mambo ya nje ya Marekani, na mageuzi makubwa yanayofanywa na Bw. Trump bila shaka yatatikisa diplomasia duniani.

Rasimu ya amri ya rais itakayosainiwa na Rais Trump ikilenga maeneo hayo inaripotiwa kuwa tayari kusainiwa, ikiwa na hatua mbalimbali, lakini mabadiliko muhimu zaidi ni pamoja na yale yanayoilenga Afrika. Serikali ya Trump imeamua kuondoa shughuli nyingi za Wizara ya Mambo ya Nje barani Afrika, na kupendekeza kufungwa kwa balozi zilizotajwa kuwa "zisizo muhimu" katika nchi mbalimbali za Afrika. Kati ya mabadiliko mengine ofisi ya Masuala ya Afrika, ambayo inasimamia sera za Afrika kusini mwa Sahara, nafasi yake itachukuliwa na "Ofisi ndogo zaidi ya Mjumbe Maalum wa Masuala ya Afrika."

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa Trump anafikiria kufunga balozi 10 na balozi ndogo 17. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani itaundwa upya na kuwa na ofisi nne za kikanda, zikilenga maeneo ya Indo-Pacific, Amerika Kusini, Mashariki ya Kati, na Eurasia. Katika mpango huu inaonesha kabisa kuwa Afrika haipo akili au hata kwenye mipango ya serikali ta Trump.

Mabadiliko haya hata kama yakipitishwa si jambo jipya kwenye duru za kidiplomasia za Afrika na hata duniani, kwani jambo sawa na hilo lilifanywa na serikali ya Rais Trump katika awamu yake ya kwanza ya urais, lakini sasa hivi inaonekana kivitendo zaidi.

Hata hivyo ni lazima tukubaliane na ukweli kuwa, inawezekana mabadiliko anayotaka kufanya Trump yanatokana na Marekani kutambua ukweli kwamba dunia sasa imebadilika. Cha kushangaza ni kwamba Bw. Trump mwenyewe hatambui kuwa mabadiliko hayo duniani pia yamefanya Afrika iwe na machaguo mengi zaidi ya kukabiliana na dharau na vitendo vyake vya uhasama.

Kwanza Afrika sio bara sawa na lililokuwepo kabla ya mwaka 1950. Kwa sasa Umoja wa Afrika umekuwa na mwelekeo wa kuimarika, na umoja huo haupo kwenye eneo la siasa tu, bali pia sasa una mwelekeo wa kiuchumi zaidi. Kuna uwezekano kuwa hatua za Bw. Trump badala ya kuleta masikitiko zinatakiwa ni kichocheo kwa umoja zaidi wa nchi za Afrika.

Ikumbukwe pia kuwa kwa sasa dunia sio eneo la nchi moja tena. Inawezekana kuwa Marekani ina nguvu kubwa kijeshi, lakini kiuchumi kuna nchi mbalimbali duniani zenye uwezo wa kuziba ombwe linaloachwa na Marekani. Baadhi ya wachambuzi wa Marekani walidiriki hata kusema kuwa baada ya Marekani kuondoa misaada yake barani Afrika, janga linaweza kutokea. Ni karibu miezi mitano sasa baada ya Marekani kufanya hivyo, hakuna kubwa baya lililotokea. Bila shaka hivyo ndivyo itakavyokuwa hata baada ya Marekani kufunga balozi zake katika nchi mbalimbali za Afrika.
 
Athari si za muda mfupi kama mnavyofikiri,marekani imejipambanua na kuwa tegemewa karibu bara lote la afrika,lazima athari ziwepo.
 
Back
Top Bottom