Marekani kulipa fidia kama njia ya kuizuia Israel kuishambulia Iran! Iran yasema ipo tayari kwa lolote!

enzo1988

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2018
Posts
1,838
Reaction score
7,346
Katika hali inayoonekana kama njia ya kupunguza na kuondoa taharuki huko mashariki ya kati, serikali ya Marekani imesema ipo tayari kulipa fidia kutokana na madhara ya mashambulizi ya makombora kutoka Iran wiki iliyopita!

On Sunday, Israeli TV channel Kan11 claimed that Washington had offered West Jerusalem a “compensation package” for not striking Iranian nuclear sites or oil facilities






Wakati hayo yakijri, serikali ya Iran yenyewe wanasema wana mipango mikakati zaidi ya kumi (10) kwa shamabulizi lolote kutoka Israel na imesisitiza kuwa Israel kwao ni taifa dogo sana!


The Iranian military has prepared at least ten” scenarios for a possible Israeli strike, according to the news agency run by the Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC).



Nb: Muda utaamua!
 
Ila watu wengi wanaipa kura za juu sana israel lkn watambue iran nao wanajua na huenda walijitayarisha toka zamani kwa harakati kama hizi

Muda utaongea
 
Israel na Marekani lao ni moja, hapo wanabuy time tu lakini Iran lazime idhoofishwe kabisa ndio target.
 
Mtoto ukimdekeza ndio madhara yake haya. Aachwe afunzwe na Dunia.
 
kutoka Israel na imesisitiza kuwa Israel kwao ni taifa dogo sana!
Hii ni jeuri ya mnyama ajulikanaye kama nyegere.
Taifa dogo huku limemdungua mgeni wako akiwa amekutembelea
kati kati ya mji mkuu wa nchi yako?

Kweli kenge ili ajitambue amepigwa lazima atoke damu puani.
 
nchi za kiarabu zina mikwara sana
tunamkumbuka Sadam na irak yake. ila ni wepesi kama unyoya
 
Ila watu wengi wanaipa kura za juu sana israel lkn watambue iran nao wanajua na huenda walijitayarisha toka zamani kwa harakati kama hizi

Muda utaongea
Mapungufu Makubwa ya Iran ni poor intelligence, jeshi la anga very poor na kuwa kitisho kwa majirani zake ambao ni Wasunni hapa ndipo amepoteza timing zote, badala yake anawatumia magaidi wa Kisunni Hamas ili ionekane Iran inathamini watu wa Palestina kumbe ina Agenda zake binafsi kupitia makundi ya kigaidi.
 
Lengo la USA ni kuidhoofisha Iran katika mpango wa kuilinda Israeli na kuzifanya nchi zote za middle east kuwa allies au puppet wa west against Russia.

Russia and Iran kuna mahala wana ukaribu wa border na hapo ndio unaileta Russia middle east kupitia Iran na kuleta influence.

Vita kati ya Iran na Israeli kwa sasa inaweza kuleta athari kubwa kwa USA maana watajikita sana kuelekeza nguvu mashariki ya kati huku home work ya Ukraine haijaisha, tafsiri yake Ukraine itatekwa kirahisi na kumfanya Russia arelax na kuelekeza nguvu kwa allies wake wa mashariki ya kati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…