Asiyekuelewa atakuwa ni mpumbavu mno. Hata ktk hii vita, niliwahi kuzungumza kuwa, Russia alikosea kuingia Ukraine, alikosea sababu anashutuku serikal ya Ukraine ina mkono wa magharibi. Sasa nikauliza swali, ikiwa shutuma hizo ni za kweli, yeye Russia alishindwa nini kuweka mtu wao hapo ili kuhakikisha usalama wake?
Leo tutengane na Zanzibar, kisha Rwanda aje aweke pandikizi serikali ya mpya ya Zanzibar. Je sisi Tanganyika tulikuwa wapi kuweka mtu wetu ili kulinda maslahi ya Taifa letu ambapo sana sana ni usalama wa nchi yetu?
Hapa ndipo unapoona licha ya uovu wote wa US, na kila mtu anafahamu hili, ila jamaa wana akili nyingi mno, wakati ambao sisi tunawaza miaka 10 mpaka 20 au 30 mbelez wao wapo 50 na zaidi. Na wana confidence ya ajabu ktk kutimiza matakwa yao. Hawayumbishwi kirahisi au kukata tamaa kirahisi.
Sent using
Jamii Forums mobile app