Marekani kupeleka Ulaya Cubic meters 15 bil za gesi asilia kufidia ile waliyokuwa wananunua Urusi

Kuupanda mchongoma kushuka ndio ngoma

Rais Biden wa Marekani anajadiliana na kufikia makubaliano namna USA itavyowapelekea Ulaya cubic meters 15 bil za gesi asilia kufidia pengo lililojitokeza baada ya kuiwekea vikwazo Russia.

Source: BBC
Anataka kuwapelekea gesi kutoka mbali kote huko wakati iko huku kwetu ya kumwaga,hii fursa inabidi tuichangamkie ili tuuage umasikini...
 
Uko sahihi somo la long term planning linafundishwa kila chuo hata kama cha kata Tanazania kiwe cha diploma au degree.Mimi huwa nashangaa mtu akisema elimu yetu iko chini sidhani.Kaulize hata mtu aliyesoma chuo cha kata na aliyepata low class anajua long term planning ni kitu gani atakueleza vizuri kwa ufasaha hasa!!

Cha ajabu ni USA pekee ndio huwa serious kwenye issue ya long term plans na implementation.Sisi kila siku long term plans hubadilika inategemea Raisi gani au bosi gani yuko madarakani kwa wakati huo!! Kuna succession plan ya kupokezana uongozi sio long term plans za nchi.Marekani wana zote succession plan za uongozi na long term plans na wako serious nazo
 
Unafkiri US na Europe wakiamua wanashindwa kuhusu hilo bomba kuliweka?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ingekua rahisi wangeweka toka mwaka 1960, Pengo aliloliacha Russia unafikiri US anaweza kuliziba, kumbuka Russia alikuwa ana supply 40%, US anatarajia kupeleka only 10 per given time kwa gas aliyokuwa anapeleka Russia, na hapo US unaambiwa wamefika mwisho kabisa wa uzalishaji, yaani kama unakula wali basi unaokoteza mpaka na punje za chini ili kusudi tu ushibe.

Norway, Algeria n.k ni moja ya nchi zinazopeleka gas Ulaya.


US haiwezi kuziba pengo aliloacha Russia, ni kauli za kibingwa tu za kisiasa.
 
Umeongea kifupi ila umeeleweka, umeongea kisomi. Kwa hoja hiyo, basi tusiilaumu ulaya kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asiyekuelewa atakuwa ni mpumbavu mno. Hata ktk hii vita, niliwahi kuzungumza kuwa, Russia alikosea kuingia Ukraine, alikosea sababu anashutuku serikal ya Ukraine ina mkono wa magharibi. Sasa nikauliza swali, ikiwa shutuma hizo ni za kweli, yeye Russia alishindwa nini kuweka mtu wao hapo ili kuhakikisha usalama wake?

Leo tutengane na Zanzibar, kisha Rwanda aje aweke pandikizi serikali ya mpya ya Zanzibar. Je sisi Tanganyika tulikuwa wapi kuweka mtu wetu ili kulinda maslahi ya Taifa letu ambapo sana sana ni usalama wa nchi yetu?

Hapa ndipo unapoona licha ya uovu wote wa US, na kila mtu anafahamu hili, ila jamaa wana akili nyingi mno, wakati ambao sisi tunawaza miaka 10 mpaka 20 au 30 mbelez wao wapo 50 na zaidi. Na wana confidence ya ajabu ktk kutimiza matakwa yao. Hawayumbishwi kirahisi au kukata tamaa kirahisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenzio anapeleka maji kwa bomba wewe kwa boza tutaona mwisho wake
 
Hiyo gesi USA ataitoa popote duniani

Hata Kwa kumwaga damu
 
Nimeupenda mfano wa Rwanda!
 
Hiyo reserve ya US kwisha ni baada si chini ya Miaka 400 ijayo kwa kupiga current production ya sasa ikihusisha na hiyo wanayouzia Ulaya

Kwa hiyo waweza fidia hiyo gap ya Russia kwa Miaka 400 ijayo labda useme baada ya hiyo miaka 400
Russia anagesi mpaka ya kugawa bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…