Marekani kutoza rai wa Malawi na Zambia takriban dola 5,000 hadi 15,000 kuingia Marekani

Marekani kutoza rai wa Malawi na Zambia takriban dola 5,000 hadi 15,000 kuingia Marekani

Joined
Jun 26, 2024
Posts
41
Reaction score
57
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kwamba raia wa Zambia na Malawi watatakiwa kulipia dhamana ya dola za Kimarekani 5000 hadi 15,000 (USD5,000 - 15,000) ili kuruhusiwa kuingia nchini Marekani kwa vibali (VISA) vya biashara au utalii.

Utekelezaji wa Uamuzi huo utaanza rasmi Agosti 20, 2025 kama sehemu ya zoezi la majaribio ya kupunguza idadi ya wageni wanaoamua kubakia Marekani hata baada ya vibali vyao kuisha muda.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Tammy Bruce, ameeleza kuwa dhamana hiyo itarejeshwa kwa muombaji, pale atakapokuwa ametimiza masharti ya kibali chake cha kuingia Marekani.

Aidha, imeelezwa kuwa raia watakaoingia nchini humo watatakiwa kupitia Uwanja wa ndege wa Boston Logan, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy na uwanja wa ndege wa Washighton Dulles. Raia hao pia wametahadharishwa kutokutoka nchini humo kupitia viwanja tofauti na hivyo kwani uondokaji wao hautosajiliwa.

Huu umekua muendelezo wa kampeni kubwa ya kupambana na kile kinachoitwa uhamiaji haramu.
 
Back
Top Bottom