Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .
aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.
Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.
Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
- Tunachokijua
- Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.
Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.
Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.