SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.

IMG-20250306-WA0008.jpg
 
Tunachokijua
Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.

Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.

Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.
Niliwahi kuandika Uzi huu

Nafikiri majibu yamepatikana sasa.

Wanajeshi wa drc ndio walikua wanaua raia ili wazalendo ( wao wanawaita waasi) wa drc waliokua jeshini waliasi wanaotaka kulinda rasilimali za nchi waonekane wao ndio wabaya ...
Mkuu kwani ulithibitisha vipi beyond reasonable doubt kwamba waasi hawaui kabisa raia badala yake wanasingiziwa?

Lakini pia umefikiaje kirahisi tu conclusion ya kumvisha Kagame taji la uzalendo kwa kuvamia na kupambana na majeshi ya nchi nyingine? Kwa tunaoishi na jamii za watutsi tunajua fika tabia zao za roho mbaya, ubaguzi na ubinafsi huwezi katu kutudanganya kuwa Kagame anafadhili M23 kwa sababu ya kuguswa na misoto ya watu wa Congo, na eti haui kabisa anasingiziwa, never.
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
Duh!..
 
Hayo madini anayaiba Kagame kwa muda mrefu sasa, na ndio yanatumika kama fimbo ya kuwapiga wazaire.
Kumpa Marekani ina maana kumkimbiza Kagame kutoka kwenye hayo madini.
Maana nyingine Kagame amenyang'anywa uwezo wa kuuwafadhili M23.
MBOKA NA NGAI ...

Kagame anahitaji vikwazo tu Ili kukomesha vurugu anazofanya huko Kivu..
 
Hiyo inaitwa tukose wote.
DRC watakosa madini.
Rwanda watakosa madini.
Marekani watapata madini, DRC watapata amani pengine na maendeleo kidogo.
WIN WIN SITUATION HAPA ANAYEFAIDIKA NI MMAREKANI.....

BAADAE HUKO UTASIKIA MAREKANI INA HIFADHI KUBWA YA MADINI ADIMU IKIWEMO HAYO YA KUTENGENEZEA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI
 
Back
Top Bottom