SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.

IMG-20250306-WA0008.jpg
 
Tunachokijua
Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.

Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.

Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.
Nakubaliana na wewe kwamba kuna kitu hakipo sawa kwenye ubongo wetu watu weusi. Yule wa Bukinafaso was more worse, walau kajitambua but je ataishi muda mrefu yule kweli? I doubt, watu weusi wanaweza kumsariti afe kama walivo kufa wapigania uhuru kina Kwame Nkuruma, Patrice Lumumba, nk.
Mabeberu hawawezi kumuacha salama aisee, intelijensia yao ipo juu sana na watafanya kila namna kumshusha chini kama ya kipindi kile kwa Gadafi
 
Ndo hitaji lake kwa sasa. Uwwzekano mkubwa kapunjwa.
Alternatively, aorganise achimbe mwenyewe awauzie faida aitumie kuimarisha usalama wake, na hii ndo best alternative but it needs brain to implement. Hiyo brain anayo?
Hapo ndio kipengele mkuu na swala hili linaibua hoja nyingi hasa katika siasa za kimataifa na kama ujuavyo pale Congo ni lango kubwa la kiuchumi kupitia zile rasilimali za madini
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
Kazi ya kuwaondoa waasi si wangepewa JWTZ,wiki tu wangeondolewa wote
 
Hayo madini anayaiba Kagame kwa muda mrefu sasa, na ndio yanatumika kama fimbo ya kuwapiga wazaire.
Kumpa Marekani ina maana kumkimbiza Kagame kutoka kwenye hayo madini.
Maana nyingine Kagame amenyang'anywa uwezo wa kuuwafadhili M23.
Agreed mkuu, kiukweli suluhisho sijui lini litapatikana juu ya mzozo huu
 
Hayo madini anayaiba Kagame kwa muda mrefu sasa, na ndio yanatumika kama fimbo ya kuwapiga wazaire.
Kumpa Marekani ina maana kumkimbiza Kagame kutoka kwenye hayo madini.
Maana nyingine Kagame amenyang'anywa uwezo wa kuuwafadhili M23.
Yes na hako ndio ka akili kidoogo kalikotumika ni kwamba kama Kagame anawapata madini kupitia proxy ni bora wao wawape moja kwa moja ,kwa kifupi Kagame yatamkuta mambo muda si mrefu
 
Unapata amani lakini kiwango kikubwa cha madini kinaenda Marekani

Japo sipuuziii suala la Amani Kongo, ila Marekani ni mastermind anajua kuchanga karata zake vizuri

WIN WIN SITUATION HAPA ANAYEFAIDIKA NI MMAREKANI.....

BAADAE HUKO UTASIKIA MAREKANI INA HIFADHI KUBWA YA MADINI ADIMU IKIWEMO HAYO YA KUTENGENEZEA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI
Unataka raia wa DRC waendelee kufa? Tshekedi kashaona majirani zake wote hawana nguvu za kupambana na M23,bora agawe madini kwa mmarekani apate ulinzi wa watu wake, au mnapenda wakongo waendelee kufa kisa eti uzalendo wasigawe madini yao kwa wazungu(jiwe aliharibu uwezo wenu wa kufikiri,kila kitu mnamuona mzungu hafai)
 
HUU MSTARI HAPO JUU HUJAUONA...''Japo sipuuziii suala la Amani Kongo''
 
Unapata amani lakini kiwango kikubwa cha madini kinaenda Marekani

Japo sipuuziii suala la Amani Kongo, ila Marekani ni mastermind anajua kuchanga karata zake vizuri
Kwani angekaa nayo hivyo ktk hali hii ambayo yanaibiwa na Kagame kwa kejeli na mauaji ya wakongo ingeongeza nini! Bora amani kwanza mengine watajadiliana. Kwani ni congo pekee ktk Afrika au duniani itakayokuwa imefanya jambo la ajabu. Vipi kuhusu Ukraine, south Africa wanufaika ni akina nani, nchi zenye mafuta nk.. bora Kagame afukuzwe kwanza ili kuondoa dharau zake siyo tu kwa Afrika bali pia kwa dunia.
 
Ndio maana humshangaa MTU anaechukia waarabu,adui wa mtu mweusi ni mzungu
Duuuh,sasa hao si walewale tu wote?
unadhani ingekuwa kwenu si wangepewa waarabu mbuzi tu
 
Back
Top Bottom