SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.

Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.

Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.
Back
Top Bottom