SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.

IMG-20250306-WA0008.jpg
 
Tunachokijua
Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.

Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.

Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.
Kagame sasa anaelekeza mirija yake Tanzania, Ndio nimesema Tanzania!
Tunaokaa huku kanda ya ziwa kwa Dotto Biteko tunayaona mengi sana!
 
Yes mkuu! Lkn ile dhamila ya kutaka kutatua mgogoro kwa ujumla huioni
Kinachotafutwa ni suluhisho la muda (Temporary solution) kwa ajili ya kulinda madaraka.
DR Congo Wana Bahati mbaya ya kupata Marais wanaojali madaraka yao kuliko maslahi mapana ya nchi.
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
Masikini kagame 🥹🥹🥹
 
Kagame sasa anaelekeza mirija yake Tanzania, Ndio nimesema Tanzania!
Tunaokaa huku kanda ya ziwa kwa Dotto Biteko tunayaona mengi sana!
Aisee! Sasa mbona mmekaa kimya tuu muda wote huo? Au na ninyi mnataka muone kama kuna fursa?
 
Unampa marekani madini wewe unapewa vifaa vya ulinzi
Yale yale yanajirudia.

Na hivi mmarekani ameyaainisha madini hayo kama "Critical minerals" na kuyahakikishia "usimamizi salama na Udhibiti"
Tutaona na kuyasikia mengi.

Nonetheless, yale waliyayafanya nchi za magharibi miaka ya nyuma kwenye bara letu kwa kibwagizo cha kutetea masilahi yao; waliwagawia silaha mababu zetu kama trade offs na baadae kuleta majeshi kuhakikisha usimamizi salama na udhibiti wa njia zao za usafirishaji n.k-sio mda mrefu wata watawala bakongo kama walivyofanya mabeberu wa Ulaya.

Mambo yanajirudia. Kweli ni Usenge huu.
 
Kama ni hivyo, mbona yana matumizi madogo ukilinganisha na nguvu inayotumika kuyachukua?
Zaidi ya 45% ya madini yote duniani aina ya Cobalt na 75% ya madini yote duniani aina ya coltan yanapatikana dr congo pekee, ni madini adimu sana ndio maana inatumika nguvu kubwa sana kuyapata
 
M23 ni wacongo wenye asili ya kitutsi. Kuwakatalia utaifa wao ndio kutakakofanya waendelee kupigania kilicho chao.
Nenda benaco karagwe pale,na kigoma kwenye kambi za wakimbizi,kuna wakimbizi wapo mle toka miaka ya 70 wamezaliana mle lakini sio wa TZ,siku drc wakiweza kuicontrol east congo ndio utajua m23 kwao halisi ni wapi
 
M23 ni wacongo wenye asili ya kitutsi. Kuwakatalia utaifa wao ndio kutakakofanya waendelee kupigania kilicho chao.
M23 siyo wakongo, uzuri umesema ni watutsi. Asili ya watutsi ni ama Rwanda au Burundi. Watutsi wa kongo waliingia huko kutokea Rwanda kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kikabila kati ya wahutu na watutsi vilivyokuwa vinatokea huko mara kwa mara hasa vile vilivyomuingiza Habyarimana madarakani miaka ya 1959 hadi 1962 pia vile vya kimbari ambapo ktk vipindi vivyo watutsi wengi walikimbia,hata Kagame na wazazi wake waliweza kukimbilia Uganda. Je mbona Kagame leo hakuendelea kudai kuwa yeye ni Mganda ingawa tayari alihudumu ktk jeshi la Uganda. Kwetu Afrika kuzaliwa ktk nchi fulani hakukupi uhalali wa moja kwa moja kuwa wewe ni raia hadi hapo taratibu za nchi husika zitakapo kuruhusu. Kwa sasa hawa watutsi wana agenda yao iliyojificha.
 
Usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili sio wapuuzi mnaochangia humu kwenye jukwaa la international.

You are supposed to anticipate the opponent move and prepare the counter attack.

That rationale is based on various global factors.

99.99% ya wachangiaji wa hili jukwaa ni wajinga watupu.


Ndio ukweli
 
Back
Top Bottom