SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.

IMG-20250306-WA0008.jpg
 
Tunachokijua
Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.

Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.

Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.
Hii ni habari mbaya sana kwa PK, kwa 🇺🇸 kupewa mandate ya kuvuna madini, ina maana Rwanda hana nafasi tena Congo.
 
Wazungu washenzi sana wanacheza huku na huku unakuta USA ndio anafadhili M23 walete chokochoko kisha anakuja upande wa Serikali anataka madini awape ulinzi unashangaa mkikubaliana tu mkaweka saini M23 wanalipwa chao na USA kisha wanyeyuka.
 
Kama ni hivyo, mbona yana matumizi madogo ukilinganisha na nguvu inayotumika kuyachukua?
Mkuu, unasema matumizi madogo???? Hebu tafakari kwa umakini zaidi kama ifuatavyo:
Hayo madini ni hitajio muhimu sana ili kuzalisha hivyo vitu alivyotaja mdau lakini ukiingia kwa undani zaidi sasa hapo utagundua kwamba hiyo computer ndo inatumika pia kuendesha Drones (za kivita au kiraia), lakini pia yale makombora Guided missiles yanahitaji electronic devices ili kuwa more precise to the targets, simu (smart phones) sio tu ya kusikiliza, kupiga picha mnato au mjongeo au kuandika sms n.k. bali pia ni remote control gadget (rejea kulipuka kwa zile paggers huko Lebanon) halafu ujue kwamba AI na maroboti nayo ni vifaa vya kielectronic pia -vinahitaji matumizi ya hayo madini. Tena ndege vita na air defense systems ni silaha zenye kifaa cha kielectronic ndani yake. Satelites zinazorushwa angani (za kivita au kiraia) huwa na vifaa electronic chips vyenye hayo madini pia.
Kwa kifupi hayo madini ni kitu muhimu mno na nyeti sana kwenye ulimwengu huu wa sasa wa kidigitali.
 
Wazungu washenzi sana wanacheza huku na huku unakuta USA ndio anafadhili M23 walete chokochoko kisha anakuja upande wa Serikali anataka madina awape ulinzi unashangaa mkikubaliana tu mkaweka saini M23 wanalipwa chao na USA kisha wanyeyuka.
Hilo nalo neno. Inawezekana pia ikawa hivyo. Those guys are very cunning.
 
Waafrika tukiamua tunaweza ila ndio hivyo sasa
Kuamua kuongea ni rahic lakin ground hakuna mizizi, hatujaandaliwa kushindana na jamii nyingine zaid ya kuongea. Hatuzalish chochote zaid ya kunukuu maandishi ya wanaume tu. Ili ufikie hapo unapotaka tufike peekaboo watoto shule sana na pambana nao kwenye nidhamu.
 
So wanaipa Marekani script ya namna ya kuchukua Madini ya Afrika, once DRC case is closed, wataenda kwa nchi engine tena na wataitumia tena puppets wao, maana from the beginning wanufauka wanaweza kuwa ni walewale
 
Congo kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe, nchi haina umoja sio kama Ukraine ; Tshekedi anapata wapi ujasiri wa kuingia mkataba wa kuwapa marekani haki ya kuchimba madini tena sehemu zinazomilikiwa na M23?
Tshekedi anakuwa kibaraka wa marekani kama Mobutu ; hawezi kudumu atapinduliwa muda si mrefu.
Mkuu; Kumbuka Tshiseked kwa Kisheria za Kimataifa ndo Rais anayetambulika kama mwenye final say juu ya mustakabali wa hatma ya kinachoendelea hapo DRC. Hao M23 bado wanajitafuta. Kwa hiyo mwenye mamlaka (kwa ubunifu wa mbinu) amempangisha (outsoucre au amemkaimisha) huyo kidume eneo hilo kwa Mkataba. Kwa mantiki hiyo, Marekani kama mmiliki/mpangaji (Tenant) halali wa eneo hilo atakuwa na kazi ya kuyalinda maslahi yake mwenyewe ndani ya eneo hilo la Eastern DRC na Tshisekedi atatulia "at room temperature" na kuangalia au kufuatilia tu jinsi ambavyo huyo Kidume anavyotembeza kichapo.
Yatokanayo:-
1. Mmarekani akiulizwa kulikoni; ataonesha Mkataba.
2. Tshisekedi akiulizwa atasema yy ndo Rais, Amiri jeshi mkuu na ndiye Msemaji halali wa DRC Kisheria.
3. M23 endapo wakiulizwa kulikoni; wataishia makelele tu ya tunaka nchi yetu, tumechoka kudhulumiwa, tunataka madini yetu....blablaa...n.k. Hawana nguvu ya kisheria.
4. Tolu akiulizwa atasema yy tangu zamani alishakanusha na kukataa kwamba anahusika huko mashariki ya DRC. Yule jamaa ni mjanja sana.
5. SADC na Mataifa mengine e.g. Africa wakiulizwa watasema "Hapo DRC hapaeleweki" na tukipeleka Walinzi wanauawa na kutekwa kana kwamba wapo kwenye mapambano ilhali walinzi hao iliwekwa baya kwamba ni walinzi wa Amani na hawahusiki na Mapambano.
Mkuu; Mpaka hapo unaweza kuona akili aliyotumia Tshisekedi. He has played it wisely.
Matokeo tarajiwa (Prognosis): Kinachotegemewa hapo ni uwepo walau wa Amani (japo haiyumkiniki ni kwa muda na kiwango gani) (Probability of an event to occur = ? haitabiriki.);
-Majeshi ya Serikali watapewa mafunzo stahiki ya kijeshi na sio kama ilivyo sasa hv eti Afande anaingia baa na AK 47 halafu akishalewa halipi na akiulizwa anakoki silaha na watu wanasambaratika kila mtu kivyake.
  • Hayo madini yatachukuliwa kwa Utaratibu unaoeleweka ndani ya Mkataba uliokubalika.
  • Hao M23 watadhibitiwa (japokuwa haiyumkiniki sana) kwani watakuwa wanapambana na "Adui mpya" na ambaye ana utaalam, vifaa-vita na uzoefu mkubwa wa mbinu za kivita kuliko Jeshi la DRC na lile la Tolu.
 
Ila mzee kwa nchi za Kiafrika uchumi wa kuchimba madini hatuna, hii njia aliyoitumua mie naona iko vyema mfano Saudia mbona walitoa mafuta yao ili walindwe na USA na mambo yanawaendea vyema tu. Muhimu wangie nao mkataba mzuri wenye kuilinda kongo na watu wake
....muhimu waingie mkataba mzuri.....
 
Kwa style hii tusahau mgogoro kuisha
Uishe vp, wao wamepewa zana walinde nchi yao hawana hela ya kurudisha bali kutoa eneo US achimbe madini.
kutoka kwa uonevu wa hao majirani zake waafrika wenzie kabisa Ambao wanagombea hayo hayo madini na wanachimba kibabe.
Wameacha kukaa na rasilimali zao, wanaiba DRC kila siku.
Sioni kosa wakiomba silaha na mafunzo US badala ya mkopo.
Dawa ya moto ni moto
 
Kabisa. Haikubaliki mtu anaingia kibabe kwenye mali zako kana kwamba ni za kwake na hapo zilipo zipo kimakosa. Na ukithubutu kujaribu kuhoji/kuuliza anakuua.
 
Mkuu, unasema matumizi madogo???? Hebu tafakari kwa umakini zaidi kama ifuatavyo:
Hayo madini ni hitajio muhimu sana ili kuzalisha hivyo vitu alivyotaja mdau lakini ukiingia kwa undani zaidi sasa hapo utagundua kwamba hiyo computer ndo inatumika pia kuendesha Drones (za kivita au kiraia), lakini pia yale makombora Guided missiles yanahitaji electronic devices ili kuwa more precise to the targets, simu (smart phones) sio tu ya kusikiliza, kupiga picha mnato au mjongeo au kuandika sms n.k. bali pia ni remote control gadget (rejea kulipuka kwa zile paggers huko Lebanon) halafu ujue kwamba AI na maroboti nayo ni vifaa vya kielectronic pia -vinahitaji matumizi ya hayo madini. Tena ndege vita na air defense systems ni silaha zenye kifaa cha kielectronic ndani yake. Satelites zinazorushwa angani (za kivita au kiraia) huwa na vifaa electronic chips vyenye hayo madini pia.
Kwa kifupi hayo madini ni kitu muhimu mno na nyeti sana kwenye ulimwengu huu wa sasa wa kidigitali.
Kama zina matumizi katika utengenezaji wa mifumo ya kivita/ulinzi hapo nakubaliana na wewe. Lakini hii ya kusema madini yanatumika kwa ajili ya kutengeneza mapambo, inaweza isiwe sababu kuu ya uchimbaji wake.
 
Kabisa. Haikubaliki mtu anaingia kibabe kwenye mali zako kana kwamba ni za kwake na hapo zilipo zipo kimakosa. Na ukithubutu kujaribu kuhoji/kuuliza anakuua.
You are making the assumption that DRC is a United country, it’s not! Ni mkusanyiko wa makabila mengi kila moja linatetea muhogo wake! Tshekedi hakubaliki huko Eastern DRC Ndio maana anashindwa kutawala.
Kuwaita wamerekani waje kumsaidia kutawala kwa kulinda madini is untenable in the long run! Mobutu throughout his reign was propped up by the Americans but he was overthrown; same thing will happen to Tshekedi in no time!!
 
Kwani mbona Tz tunayo makabila zaidi ya 120 na hatuna huo mtafaruku? Ni suala la kujipanga tuu. Haijawahi kutokea Rais wa nchi yeyote hapa Duniani akakubalika na wananchi wake wote. - HAKUNA. Hata hapa Tz ww ni shahidi jinsi rais wetu anavyofanyiwa. Cha msingi ni jinsi Rais na Serikali yake anavyojiweka. Kuna gharama yake ujue lakini.
Ni kweli kuwaita Marekani sio suluhisho la kudumu lakini walau kwa hilo nchi itapumua kwa Amani kidogo.
 
Hebu jiulize Joseph Kabila aliwezaje kuwa na relative peace enzi ya utawala wake?
Halafu jiulize tena jimbo la Katanga linapakana na nchi nyingine na kuna madini pia kwanini hakuna vita kama eastern DRC?
Jibu ni kwamba Huko Katanga makabila yanayoishi mpakani hayabaguliwi na nchi husika!! Kiini cha mgogoro wa DRC ni ubaguzi haya mambo ya madini yamekuja baadae! It’s the land stupid!
 
Back
Top Bottom