SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.

IMG-20250306-WA0008.jpg
 
Tunachokijua
Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.

Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.

Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.
Je ccm wanasemaje kuhusu swala la uchaguzi wazidi kubaka demokrasia waingie mkataba na USA
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
kagame akae mguu sawa hii miaka miwili haiishi yatamkuta ya Sadam,tena kigezo cha kumtoa roho itakuwa ni uroho wa madaraka...ila nitafurahi yakimkuta hayo
 
Tulimwambia tsekekedi akitaka kuwarejesha m23 Rwanda awape wamarekani migodi Kongo mashariki.
Si unaona wale magaidi wa msumbiji walivyopotezwa kwa sababu marekani anachimba madini kule
 
Hayo madini ya Congo yameanza kuibiwa zamani ni kampuni za huko huko marekani (Apple) na M23 ndio waliokuwa wanagawa hayo madini na kupewa silaha kumshambulia Tikshedi DRC kuondoka madarakani. Sasa ni vile madini yao yataendela kuondoka kwa mtindo mwengine ambao utambakisha madarakani Tikishedi.
Nakuunga mkono kabisa kwa hili

iko hivi, Wazungu wakiona inakuwa ngumu kuingia nchi za watu, huwa wanawatumia waasi kwa kuwapa silaha na msaada wa kijeshi ili kupambana na serikali iliyoko madarakani.. nyie mnapambana huku, wao wanabeba madini hao wanasepa
 
Trump akiwaita “ Shithole countries “ mnakasirika ! Yako wapi sasa? Waafrika wameshindwa kutatua matatizo yao wenyewe mpaka marekani aje kusuluhisha kwa ujira wa madini anavyotaka yeye! Halafu anawauzia silaha muuwane wenyewe kwa wenyewe! What a curse!
I pray that M23 should match all the way to Kinshasa and topple Tshekedi na hizo silaha zikija wazichukue .
Wakifanikiwa kufanya hivyo huo mkataba na marekani utakuwa batili
sawa mkuu asante kwa maoni yako
 
Cobalt na cotan ni madini muhimu sana kwa Elon musk kutengenezea magari yake ya umeme Tesla na pia kwenye maroketi na ma satellite yao.
Na musk na Trump ni wafanyabiashara yule mtu mrefu sijui atakimbilia wapi.
Kanali nanga anaenda kuwa nanga safari hii
 
Congo kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe, nchi haina umoja sio kama Ukraine ; Tshekedi anapata wapi ujasiri wa kuingia mkataba wa kuwapa marekani haki ya kuchimba madini tena sehemu zinazomilikiwa na M23?
Tshekedi anakuwa kibaraka wa marekani kama Mobutu ; hawezi kudumu atapinduliwa muda si mrefu.
Ujasiri anaupata kutoka mataifa makubwa yenye ushawishi kisiasa na kiuchumi (USA)
 
Back
Top Bottom