SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.

IMG-20250306-WA0008.jpg
 
Tunachokijua
Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.

Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.

Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.
Congo kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe, nchi haina umoja sio kama Ukraine ; Tshekedi anapata wapi ujasiri wa kuingia mkataba wa kuwapa marekani haki ya kuchimba madini tena sehemu zinazomilikiwa na M23?
Tshekedi anakuwa kibaraka wa marekani kama Mobutu ; hawezi kudumu atapinduliwa muda si mrefu.
M23 ipi au hii ya Rwanda inayoongozwa na viongozi wa jeshi la Rwanda walimweka kibaraka na msaliti wa wakongo Nanga kama walivyo muweka rais kivuli Kabila senior na baadae wakamgeuka na kumuua? Au Hadaa ipi unayo taka kusema.
 
Trump akiwaita “ Shithole countries “ mnakasirika ! Yako wapi sasa? Waafrika wameshindwa kutatua matatizo yao wenyewe mpaka marekani aje kusuluhisha kwa ujira wa madini anavyotaka yeye! Halafu anawauzia silaha muuwane wenyewe kwa wenyewe! What a curse!
I pray that M23 should match all the way to Kinshasa and topple Tshekedi na hizo silaha zikija wazichukue .
Wakifanikiwa kufanya hivyo huo mkataba na marekani utakuwa batili
Acha kulalama M23 ni wanyarwanda walio watangulize vibaraka na wasaliti wa congo akina Nanga na baada ya hapo huyo Nanga atauliwa kama Kabila tu.
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
Yaani Trump lazima ajione mwamba wa dunia hii, kichwa hicho!
 
Hiyo inaitwa tukose wote.
DRC watakosa madini.
Rwanda watakosa madini.
Marekani watapata madini, DRC watapata amani pengine na maendeleo kidogo.
DRC watakosa madini Gani!?
 
Maafisa tu Tshisekedi chalii, je angekutana Rubio!! afu watu wanamchukulia poa zelensky ambaye aliwekwa mtu kati na trump plus makamu wake.
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
Japo USA naye siyo wa kumwamini, angalau hao wahuni waliojazana Mashariki mwa DRC watatulia.
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
Bila shaka hii taarifa kwa Watusi na Joseph Kabila si habari njema kwao.
 
Tena amna ata baruti inayopigwa sembuse huko watu wanauwawa bora amani . Pale Afghanistan alipokuwepo Mmarekani watu walienjoy wasichana wakaenda shule maisha yakawa na ustawi alipoondoka kukawa giza tena sasa bora kipi
Yaan....Mimi nilishasema Nyerere alikosea kuwatoa wazungu mapema Tanganyika
 
Acha kulalama M23 ni wanyarwanda walio watangulize vibaraka na wasaliti wa congo akina Nanga na baada ya hapo huyo Nanga atauliwa kama Kabila tu.
Hiyo ni better option kuliko kuwaleta marekani kuja kutawala uchumi wa Congo! M23 ni wacongo wenye asili ya Kitutsi hivyo they are fighting for their country!
 
Nyie watutsi huwa hamna akili.

Au mnadhani watu ni wajinga sana hawafahamu ukweli halisi?
 
Hayo madini anayaiba Kagame kwa muda mrefu sasa, na ndio yanatumika kama fimbo ya kuwapiga wazaire.
Kumpa Marekani ina maana kumkimbiza Kagame kutoka kwenye hayo madini.
Maana nyingine Kagame amenyang'anywa uwezo wa kuuwafadhili M23.
Kwani huyo kagame hayo madini si alikuwa anawapelekea hao hao wazungu? Inaonekana kagame alikuwa mjanja kwa kuwapunja mgawo wazungu, hivyo wameamua kuyafuata wenyewe mgodini. Na hapa ndio itakuwa mwisho wa kiburi cha kagame kudharau nchi zote za ukanda wake kwa kuwa alikuwa analindwa na wazungu hao
 
Amefanya jambo jema. Sasa Kagame na magenge yake wakatafute nchi nyingine ya kuvamia na kupora madini.
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
Vita na mapigano mengi Africa ni Kwa sababu ya raslimali zilizopo. Kama DRC isingekuwa na hayo madini inawezekana kusingekua na vita. Hivyo vita vinaanzishwa Ili watu wabebe raslimali Kwa gharama nafuu. Cha ajabu wamarekani wanaweza kubeba madini na vita isiishe
 
Amefanya jambo jema. Sasa Kagame na magenge yake wakatafute nchi nyingine ya kuvamia na kupora madini.
Huyo rwanda mwenyewe nyuma yake yupo marekani na ndie kamtuma kuidhoofisha dr congo ili apate mwanya wakuchota madini kiurahisi, UN na mabeberu kama wangeamua kweli kuipiga pin rwanda kiuchumi kagame asingekua nakiburi kile na angeishasarenda kitambo!
 
Unampa marekani madini wewe unapewa vifaa vya ulinzi

ALIETULOGA WAAFRICA AISEE
Hana namna, anatafuta kutawala Congo kwa amani na yeye apate mkate. M23 unawajua ni akina nani? Hadi Ufaransa ni M23, ukiachilia mbali akina Kagame.

Hapo bila kuomba msaada asingefika mbali.
 
Back
Top Bottom