SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

SI KWELI Marekani na DRC wakubaliana katika mikataba ya madini adimu na ulinzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.

IMG-20250306-WA0008.jpg
 
Tunachokijua
Kwa sasa, Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado hawajasaini makubaliano mapya rasmi kuhusu madini. Hata hivyo, kuna mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hizo mbili kuhusu uwezekano wa mpango wa kubadilishana madini kwa msaada wa kiusalama.

Mpango huu uliopendekezwa unahusisha mashirika ya Marekani kupewa haki za uchimbaji na usafirishaji wa madini muhimu, huku Marekani ikitoa msaada wa kiusalama, mafunzo, na vifaa vya kijeshi kwa jeshi la DRC. Hata hivyo, mazungumzo haya bado yapo katika hatua za awali, na hakuna mkataba rasmi uliosainiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa wako wazi kwa kushirikiana na DRC ili kuhakikisha maendeleo ya rasilimali zake za madini kwa njia inayowajibika na yenye uwazi.

Kwa hivyo, ingawa mazungumzo yanaendelea, hakuna mkataba rasmi kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchimbaji wa madini na msaada wa kiusalama kwa sasa.
Siasa za wazungu ukiwa bwege utadhani unawaelewa hao rebels miaka yote UN ikisema warudi nyuma huwa wanarudi but this time wanajitia uziwi. Tshekedi amejifanya mzungu kasoro rangi matokeo yake amekula matapishi yake. Alishakataa kusilikilza AU and the like, mzungu kamwambia azingatie mazungumzo ya AU na EAC kuleta amani congo 🇨🇩. Alivyo mwehu ametoa shukrani kwa watu 2 tuu tena huyo mmoja kinafki. Ngoja tuone upepo unatavuma kwenda wapi
 
Hebu jiulize Joseph Kabila aliwezaje kuwa na relative peace enzi ya utawala wake?
Halafu jiulize tena jimbo la Katanga linapakana na nchi nyingine na kuna madini pia kwanini hakuna vita kama eastern DRC?
Jibu ni kwamba Huko Katanga makabila yanayoishi mpakani hayabaguliwi na nchi husika!! Kiini cha mgogoro wa DRC ni ubaguzi haya mambo ya madini yamekuja baadae! It’s the land stupid!
Sasa Kama ndo hivo; huyo Tshisekedi anakwama au nini kilimfanya hata akaifikisha nchi hapo ilipo?
Most probably, Tshisekedi is the causal agent. Lakini sasa; kwa lengo la kuiarrest situation, bora amuite Marekani japokuwa ni kwa gharama kubwa sana. Na kama kichwa chake huyo Tshiseked kipo vizuri, atumie muda huo marekani anaposomba madini, kuondoa hiyo sumu ya ubaguzi aliyoipanda huko mashariki mwa DRC. Atahitaji wadau (stakeholders) wengi na tofauti kuifanya kazi hiyo.Akibugi tena hapo baas, ni bora akae pembeni ampishe mwenye kuimudu DRC.
 
Wameanza kwanza kumkatia misaada ili apate njaa
Yep. Akipata njaa; akili itafanya kazi ya ziada kutafuta ugali badala ya silaha, umaarufu/ubabe na madini. Akikaza fuvu wanaondoa meza na kiti alichokalia halafu yy wanamhifadhi mahali na maisha yanaendelea.
 
Siasa za wazungu ukiwa bwege utadhani unawaelewa hao rebels miaka yote UN ikisema warudi nyuma huwa wanarudi but this time wanajitia uziwi. Tshekedi amejifanya mzungu kasoro rangi matokeo yake amekula matapishi yake. Alishakataa kusilikilza AU and the like, mzungu kamwambia azingatie mazungumzo ya AU na EAC kuleta amani congo 🇨🇩. Alivyo mwehu ametoa shukrani kwa watu 2 tuu tena huyo mmoja kinafki. Ngoja tuone upepo unatavuma kwenda wapi
Mwelekeo wa upepo unavuma kwa kasi kubwa dhidi yake. Ww huoni anavyotapatapa? Ila mr. Tolu hatokuwa salama pia.
 
Unampa marekani madini wewe unapewa vifaa vya ulinzi

ALIETULOGA WAAFRICA AISEE
Ivyo vifaa vya ulinzi unavyovikashivu vinauzwa trillion za pesa na endapo unakua na vifaa sahihi bas vita kuishinda na kurejesha amani kwa wananchi itakua rahis

Tunapenda sana kuponda na kukandia sabu hatujui reality ya vita na atujawai shuhudia vita
Iv ayo madini yanafaida gan kama huwezi kuyachimba ayo madini yanafaida gan km huwezi kuyatumia kukuletea amani, Amani ni muhimu
Sana na endapo amani itapatikana bas watachimba madini ili kijenga nchi yao

Waswahili wanasema chako ndo kitakacho kuokoa
 
Yep. Akipata njaa; akili itafanya kazi ya ziada kutafuta ugali badala ya silaha, umaarufu/ubabe na madini. Akikaza fuvu wanaondoa meza na kiti alichokalia halafu yy wanamhifadhi mahali na maisha yanaendelea.
Kabisa,atatia akili
 
Serikali ya Marekani na DRC wamekubaliana kwamba marekani itaruhusiwa kuchimba madini adimu maeneo ya mashariki ya DRC wakati huo Marekani itatoa vifaa vya ulinzi, tekinolojia ya kijeshi kwa jeshi la DRC .

aidha pia kulinda maeneo ya kimkakati ndani ya DRC.

Hayo yamejiri baada ya Rais wa DRC Felix Etiene Tshisekedi wa Mulumba kukutana na maafisa wa Marekani na kuwekeana mikataba kadhaa ya ushirikiano sambamba na kuwaondoa waasi wote ndani ya DRC.
Ila MAREKANI bana tayari kashamuingiza Congo geto kiulaini
 
Ivyo vifaa vya ulinzi unavyovikashivu vinauzwa trillion za pesa na endapo unakua na vifaa sahihi bas vita kuishinda na kurejesha amani kwa wananchi itakua rahis

Tunapenda sana kuponda na kukandia sabu hatujui reality ya vita na atujawai shuhudia vita
Iv ayo madini yanafaida gan kama huwezi kuyachimba ayo madini yanafaida gan km huwezi kuyatumia kukuletea amani, Amani ni muhimu
Sana na endapo amani itapatikana bas watachimba madini ili kijenga nchi yao

Waswahili wanasema chako ndo kitakacho kuokoa
Mkuu sikupingi uko sahihi

Kinachotatikana ni amani na ustawi wa jamii ili maendeleo mengine yaendelee

RISASI NA MAENDELEO havijawahi kwenda sambamba
 
Uishe vp, wao wamepewa zana walinde nchi yao hawana hela ya kurudisha bali kutoa eneo US achimbe madini.
kutoka kwa uonevu wa hao majirani zake waafrika wenzie kabisa Ambao wanagombea hayo hayo madini na wanachimba kibabe.
Wameacha kukaa na rasilimali zao, wanaiba DRC kila siku.
Sioni kosa wakiomba silaha na mafunzo US badala ya mkopo.
Dawa ya moto ni moto
KWELI KWELI KAZI KUBWA IPO
 
Trump yupo kazini haswa, hapo DRC ameona Wafaransa wanavuna na wayahudi, wachina yaani ni shamba la kuokoteza tu

Sasa ameona na yeye aje wa mtindo mwingine
Waafrika kuja kujielewa ni ngumu sana
Unashangaa waliouza mababu kwa waarabu na wazungu
Ila bado akili zile zile tu
Sasa hapo ungekuwa wewe ndo Rais wa DRC ungefanya Nini?
 
Kuamua kuongea ni rahic lakin ground hakuna mizizi, hatujaandaliwa kushindana na jamii nyingine zaid ya kuongea. Hatuzalish chochote zaid ya kunukuu maandishi ya wanaume tu. Ili ufikie hapo unapotaka tufike peekaboo watoto shule sana na pambana nao kwenye nidhamu.
inawezekana, hatujaamua tu
 
Wamarekani wamemuhakikishia kwamba watailinda Congo milele? Au alindwe yeye tu kipindi Cha uongozi wake then akitoka ngoma ibaki pale pale? Alichokifanya sio njia ya kutatua mgogoro wa hapo Congo bali ni ujinga mtupu.

Congo haijapata kiongozi mwenye uchungu na nchi yake, That' why sijaona kiongozi mwenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro Kila anae ingia ikulu anatafuta namna ya kujilinda binafsi
Ulinzi binafsi WA madaraka, the same way as Kabila jr did.
 
Back
Top Bottom