Marekani ni nchi moja ya raha sana. Wakiishiwa pesa wanachapisha tu

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Ukisikia nchi ni superpower usichukulie jambo dogo. Kuna faida nyingi sana. Mfano Marekani wakiishiwa pesa wanachapisha tu na kununua vitu kokote. Wanasafiri kutalii nk. Anachofanya ni kuhakikisha anaendelea kuwa superpower na kumdunda yoyote anayeleta fyokofyoko. Ukiwa raia wa nchi kama hiyo unashindwaje kufanikiwa?
 
Tunachapisha, ila kiasi kikizidi mfumuko wa bei unatokea. US wao pesa yao inatumika dunia yote. Wanaweza kuchapa za kutosha na kuja kununua dhahabu. Wewe huwezi chapa madafu ya kutosha na kwenda kununua dreamliner.
Kipengele hichi ulichofafanua hapa ndicho sijawahi kukielewa hata kidogo...

Yaani ndomaana huwa najiaminisha kuwa "pesa" ni mfumo tu na siku wasukuma nao wakiukamata huo mfumo basi hela ya Tanzania itaambiwa ndo yenye thamani zaidi duniani
 
Hakuna tatizo lolote kwa nchi kuchapisha pesa yake kwa namna ambavyo inataka.

Ili mradi tu, hiyo nchi iwe na uwezo wa kiuchumi wa kuzalisha bidhaa muhimu za kutosha katika soko ili kukidhi demand ya pesa itakayoingia kwenye mzunguko.

Kama kiwango cha supply ama uzalishaji wa bidhaa muhimu sokoni hakiongezeki, bidhaa muhimu zilizopo zitapanda bei taratibu ili kulingana na mahitaji (demand). Na hapo ndipo mfumuko wa bei unapotokea huku pesa ikipoteza thamani yake.
 
Hakuna uchumi wa namna hiyo, kumbuka Amin alichapisha pesa kwa wingi na akaharibu uchumi. Dollar haichapishwi ovyo ndio maana Ina thamani.
 
[emoji38][emoji38]
 
Pesa hizi ni usanii sana.
 
Sasa US pesa yao inatumika dunia nzima. Mfumuko kwao hauwezi kutokea. Wanasemwa wanaexport inflation.
 
Hakuna uchumi wa namna hiyo, kumbuka Amin alichapisha pesa kwa wingi na akaharibu uchumi. Dollar haichapishwi ovyo ndio maana Ina thamani.
Dolar inachapwa sana hovyo. Sema kinachoisaidia inatumika dunia nzima. Shida wanapata nchi zingine. Tofauti na Iddi Amin pesa yake ya Uganda tu lazima iwe na matatizo ikipita kiasi. Lakini ukweli ni kuwa serikali zinachapa pesa from thin air
 
Back
Top Bottom