Marekani, unachokifanya juu ya vita ya Russia na Ukraine si kuanzisha vita 3 ya dunia, uko tayari?

Marekani, unachokifanya juu ya vita ya Russia na Ukraine si kuanzisha vita 3 ya dunia, uko tayari?

Ka Zelensky kanapewa confidance na Wazungu wa Magharibi, Putin ana support ya Kiduku na XI Jinping
Yes ila sana sana kutoka Kwa China , Lakin kaka Mkubwa alimuita china na India kwamba mki msaidia tutawashughulikia,

Britanicca
 
Joe Biden, jana amelipua visima na maghala ya mafuta huko Urusi karibu kabisa na Moscow, alafu akamwambia Zelesky atangaze kwamba kafunya yeye...😂
Na Putin alivyo jeuri, akaitangazia dunia kwamba hiyo ni ajali ya kawaida kama ajali zingine...😀
Kiduku amemwambia Putin akimruhusu anarusha ma scud mawili moja New York na lingine London.
 
Mwaka 1939 Adolf Hitler aliivamia Poland, pale Uingereza kulikuwa na Waziri Mkuu anaitwa Neville Chamberlain alikuwa mpole mpole ana kitu inaitwa "Appeasement Policy". Chamberlain alishindwa kuchukua hatua dhidi ya Hitler tangu mwanzo kabisa dalili zikionekana, Hitler akajua Ulaya ni wazembe hamna kitu watamfanya alipomalizana na Poland akavamia France na baadae USSR.

Chamberlain aligundua alikosea sera ila alikuwa ashachelewa akajiuzuru akaja one of the best PM in British history naye ni Winston Churchill. Huyu hakuwa na kubembelezana ni kupigana, dawa ya jeuri ni kuwa jeuri zaidi yake mapema ukimuacha aote meno anakusumbua zaidi baadae.

Unachotaka kufanyike ni sawa na kilichofanywa na Sir Chamberlain. Ni sawa na kinachofanywa na Olaf Scholz. Ili WW3 isiwepo Putin anatakiwa apigwe hapo hapo Ukraine ajue kabisa yeye hana uwezo wa kusumbua dunia. Wakimuacha atavimba kichwa kama Hitler, ataona wamemuogopa kwahiyo akivamia kwingine watamuogopa vilevile ndio maana haishiwi kutest makombora, last time Marekani imetest ballistic missile ni zamani. Putin akiachwa amalizane na Ukraine atafuata Finland, Sweden na Poland na ndio itakuwa real WW3.

Kwenye Gulf war Saddam Hussein aliivamia Kuwait akaipiga kizembe. Akajipanga kuivamia Saudi Arabia na haikuwa na jeshi kubwa that time, Ufalme unaomba msaada kwa Marekani. Coalition forces wakapigana na Iraq ikaondoa majeshi Kuwait na kuacha mashambulizi kwa Saudi. Angeachwa angechukua hizo claims zake na kusumbua zaidi.

Italian PM ashasema kujadiliana na Putin ni kazi bure. Washafanya kina Naftali wa Israel, Erdogan pale Turkey na timu yake washajaribu, China ishapendekeza mgogoro uishe lakini wapi. Mtu anakuja na panga wewe unaleta mazungumzo
 
Kama ungekuwa na busara ungewaita Rais Putin na Zelensky meza moja kujadiliana namna ya kumaliza vita hii lakini umeamua kuwa upande wa Ukraine. Huu ni ujinga mkubwa sana, unachochea uanzishwaji wa vita vya tatu ya dunia. Uko tayari?

Acha kiburi Marekani, ndiyo maana afande sele alikuambia ule ndiyo ukweli. Watu wanaokufa kule Ukraine unaweza kusema kuwa ni Putin anasababisha lakini ni wewe Marekani. Kama usingemsupoti zelensky vita hii ingekuwa imeisha. Ulitakiwa kupima madhara makubwa ambayo yatajitokeza kwa kuisupoti Ukraine.

Ndugu wakigombana unakaa katikati na siyo kuegemea upande mmoja, ukishindwa vita hii dunia itakudharau sana. Ukianzisha vita ya tatu ya dunia, utachekwa sana.
Safari hii ni zamu yake kupigwa nyumbani kwake USA . Auwae kwa upanga naye hufa kwa upanga.
 
Yes ila sana sana kutoka Kwa China , Lakin kaka Mkubwa alimuita china na India kwamba mki msaidia tutawashughulikia,

Britanicca
We jamaa bhana eti kaka mkubwa sijui tutawashughulikia blah blah blah .....unashughulikiaje taifa linalojitengenezea silaha lenyewe halinunui kwa mtu ...na kwenye uchumi liko vizuri .....haya mambo ya kutishiana hapa duniani ilikuwa miaka ya 90 now now kila moja ana mapembe mzee na kuyakata inabidi huyo unaemwita kaka mkubwa ajipange kweli kweli ......
 
afadhali sijui lihitler lingefanikiwa kuifanya ujerumani kuwa super power
 
Acha vichekesho we dada/mama.
Hao jamaa zenu ni vichaa ila huwa akili wanazo linapokuja suala la Marekani na Uingereza.
The same kama vile marekani na allies wake walizoea kupiga vijinchi vidogo vidogo .......iraq wakasingizia silaha za maangamizi ....ila linapokuja swala la URUSI OR CHINA hao vichaa marekani na wenzie akili zina wakaa sawa ....na URUSI hiyo hapo ina silaha za maangamizi ....ila hutawaona wakisogea na ukraine na ni wazungu wenzao inabondwa kwanin wasiingilie kati .....kama wanavifanya nchi zingine ....
 
Kama ungekuwa na busara ungewaita Rais Putin na Zelensky meza moja kujadiliana namna ya kumaliza vita hii lakini umeamua kuwa upande wa Ukraine. Huu ni ujinga mkubwa sana, unachochea uanzishwaji wa vita vya tatu ya dunia. Uko tayari?

Acha kiburi Marekani, ndiyo maana afande sele alikuambia ule ndiyo ukweli. Watu wanaokufa kule Ukraine unaweza kusema kuwa ni Putin anasababisha lakini ni wewe Marekani. Kama usingemsupoti zelensky vita hii ingekuwa imeisha. Ulitakiwa kupima madhara makubwa ambayo yatajitokeza kwa kuisupoti Ukraine.

Ndugu wakigombana unakaa katikati na siyo kuegemea upande mmoja, ukishindwa vita hii dunia itakudharau sana. Ukianzisha vita ya tatu ya dunia, utachekwa sana.
Kupitia vita hii marekani anapima uwezo WA Russia kwenye medani za vita.mpaka sasa ameshajua Russia ni dhaifu Sana kuliko ilivyotegemewa,mpaka sasa Russia hakuna eneo la kimkakati aliloteka anarusha makombora hovyo.analenga mpaka watoto WA chekechea.mara ya kwanza vifaru vyake vilitapaka Ukraine vikapogwa hovyo.
 
Kama vita ya dunia, marekani alikuwa anaombea vita iendelee ili azidi kusupply silaha, unadhani hii operation ndo atatamani iishe angali ana supply silaha kwa Ukraine.

Kosa kubwa dunia ililolifanya ni kuruhusu marekani iwe sehemu yake ya dunia.
 
Kama ungekuwa na busara ungewaita Rais Putin na Zelensky meza moja kujadiliana namna ya kumaliza vita hii lakini umeamua kuwa upande wa Ukraine. Huu ni ujinga mkubwa sana, unachochea uanzishwaji wa vita vya tatu ya dunia. Uko tayari?

Acha kiburi Marekani, ndiyo maana afande sele alikuambia ule ndiyo ukweli. Watu wanaokufa kule Ukraine unaweza kusema kuwa ni Putin anasababisha lakini ni wewe Marekani. Kama usingemsupoti zelensky vita hii ingekuwa imeisha. Ulitakiwa kupima madhara makubwa ambayo yatajitokeza kwa kuisupoti Ukraine.

Ndugu wakigombana unakaa katikati na siyo kuegemea upande mmoja, ukishindwa vita hii dunia itakudharau sana. Ukianzisha vita ya tatu ya dunia, utachekwa sana.
Vianze tuu,mimi nitachagua upande wa Beberu
 
Back
Top Bottom