Marekani yaacha kuiendekeza Israel. Yapeleka azimio UN kutaka vita vya Gaza visitishwe bila masharti yoyote

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Mfadhili mkubwa wa Israel,Marekani baada ya kuona madhara kwa pande zote ya vita vya Gaza,ghafla imebadili mwelekeo na kupeleka azimio baraza la usalama la Umoja wa mataifa linalotaka vita hivyo visitishwe haraka.
Katika azimio lililopelekwa baraza hilo mwezi Februari kikwazo ilikuwa ni Marekani tu iliyopiga kura ya veto kupinga azimio hilo.

Kipengele kilichosimamiwa na Marekani wakati huo kwa kufuata misimamo ya Israel ilikuw ni kuunganishwa na kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas na kwamba muda haukuwa muwafaka kwa kuitaka Israel kusitisha vita kwani kungewapa ushindi Hamas.

Katika siku za karibuni misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu imemuudhi sana raisi Biden wa Marekani .Ikiunganishwa na ukatili wa kuzuia chakula na kuua ovyo kunakofanywa na Israel huenda ni miongoni mwa sababu zilizopelekea nchi hiyo kubadilisha nia yake.

US pushes UN resolution calling for 'immediate and sustained cease-fire': Live updates

Na hawatasikiliza chochote!

Kinachofanyika hapo Gaza, Ni Mungu tu ajuaye!

Wengenewe jitahidini sana kumrudia Mungu na ama muendelee kuziba masikio na kupuuza haya
 
Huyo Mungu ndiye tunayemtegemea na ndiye atakayebadili kila kitu kuwa ushindi kwa anayedhulumiwa.
 
Mungu huwa hawezi kuingilia kati kwa waliomwacha na kutokuwa na habari naye, matokeo yake huwaacha waangamie kwa ujinga wao
 
Ushindi utaenda Kwa Israel, taifa lake takativu na watu wake. Nani aliwatuma Hamas wateke watu?
 
Mungu huwa hawezi kuingilia kati kwa waliomwacha na kutokuwa na habari naye, matokeo yake huwaacha waangamie kwa ujinga wao
Watu wa Gaza kila siku ndiye wanayemlilia.
Sisi wengine ndio huwa tunalaumu Saudia na vibaraka wengine lakini kwa hakika wengi wa wapalestina wanaohojiwa huwa wanataja walivyoumia au njaa ilivyowafanya na halafu wanamtaja Mungu.Si rahisi kusikia wakilaumu watu wa nje wala Hamas na mwisho huwa wanamtaja Allah kuwa ndiye wa kuwaokoa.
Majibu ndio sasa yanakuja kwa faida yao.
 
Basi waendelee kupiga tu mpaka Hamas washike adabu. Muhimu kulinda uhai'' wa raia ila Hamas wapigwe sana.
Mpaka sasa watu wa Gaza wote ni Hamas.Watafanya kufru kubwa kwenye kuua na hawatawamaliza
 
Mfadhili mkubwa wa Israel,Marekani baada ya kuona madhara kwa pande zote ya vita vya Gaza,ghafla imebadili mwelekeo na kupeleka azimio baraza la usalama la Umoja wa mataifa linalotaka vita hivyo visitishwe haraka.
Katika azimio lililopelekwa baraza hilo mwezi Februari kikwazo ilikuwa ni Marekani tu iliyopiga kura ya veto kupinga azimio hilo.

Kipengele kilichosimamiwa na Marekani wakati huo kwa kufuata misimamo ya Israel ilikuw ni kuunganishwa na kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas na kwamba muda haukuwa muwafaka kwa kuitaka Israel kusitisha vita kwani kungewapa ushindi Hamas.

Katika siku za karibuni misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu imemuudhi sana raisi Biden wa Marekani .Ikiunganishwa na ukatili wa kuzuia chakula na kuua ovyo kunakofanywa na Israel huenda ni miongoni mwa sababu zilizopelekea nchi hiyo kubadilisha nia yake.

US pushes UN resolution calling for 'immediate and sustained cease-fire': Live updates

Israel ilishasema kuwa kama wanataka vita isimame kabisa walete mateka, na hata wakileta mateka Hama's haitarusiwa tena ku rule gaza sasa kwakuwa mateka hawarejeshwi Acha azima yao ya ku dismantle Hama's itimie wake mfumo wao wanaotaka
 
Misimamo hiyo ya Israel ni ya zamani.Walisema watapiga Ramadhani ikianza kama hawajapewa mateka wao,
Hamas hawakutoa hata mmoja.
 
Mimi nashauri Hamas waendelee kupigwa, hakuna namna tutaacha vita hii. Kazi iendelee.
 
Spain,Ireland,Canada,Wamarekani na nchi nyingi wanaona bora liundwe taifa la Palestina ili papatikane suluhisho la kweli.
Hiyo kupiga haikuanza leo na kuna viongozi wengi wa wapalestina wameshauliwa huko nyuma na haikuwa lolote.
 
Mimi binafsi siamini kama Kuna mateka wa Israel wanashikiliwa na Hamasi

Na pia siamini kama lile shambulizi lilikuwa la Hamasi kweli

Ni vita iliyoanzishwa Kwa mchongo kati ya Israel na Marekani Kwa malengo wanayoyajua wao
 
Misimamo hiyo ya Israel ni ya zamani.Walisema watapiga Ramadhani ikianza kama hawajapewa mateka wao,
Hamas hawakutoa hata mmoja.
Uongoz wa Israel ulishaidhinisha mashambulizi uko rafah, sema wanachofanya ni operation na siyo uvamizi kamili kutokana na wingi wa watu kwenye neo ilo
 
Back
Top Bottom