Marekani yaikamata ndege ya Rais Maduro wa Venezuela

Dunia lazima iwe na Kiranja Mkuu; Marekeni ndo Kiranja wa Dunia,Ulaya was ni viranja wadogo wadogo.
 

HUELEWI KIINGEREZA. LEO KAMA KAWAIDA UMEKURUPUKA NA HII ID YAKO KAMA UNAVYOKURUPUKA NA ILE ID YAKO NYINGINE. JIPIGE PIGE KIFUA SEMA "MIMI NI KILAZA PRO"

BADO HUJASEMA DOGO. IDs ZAKO ZOTE ZINAKWAMA.
 
Shida waiba kura na washinda maporini wakati wa uchaguzi lazima wamtetee Mwizi mwenzao.

Wamarekani wakamate na mali za majizi na wateka watu walioko TZ.

Mashujaa wenu ni akina Putin ambao wanaona madaraka yao ni ya maisha.
 
Nipo zangu Kyela, ninachojua kuhusu USA ni kile ninachoona kwenye TV.

Sina cha u pro wowote. Mtu kaanzisha uzi na kunukuu source ya habari ila alichoandika na kilicho kwenye source ni vitu 2 tofauti. Kwahiyo kurekebisha ndio kumenifanya pro USA?
Ugonile
 


Marekani imekamata ndege ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ikidai ilinunuliwa kinyume cha sheria kwa kiasi cha $13m (£9.8m) na kutoroshwa nje ya nchi.

Kulingana na wizara ya sheria ya Marekani, ndege hiyo aina ya Falcon 900EX ilikamatwa katika Jamhuri ya Dominika na kuhamishiwa jimbo la Florida nchini Marekani.

Haijulikani ni jinsi gani na lini ndege hiyo iliishia katika Jamhuri ya Dominika. Data ya ufuatiliaji ilionesha ikiondoka kwenye uwanja wa ndege wa La Isabela karibu na mji mkuu Santo Domingo siku ya Jumatatu, na kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale huko Florida baadaye.

Venezuela imeshutumu unyakuzi huo, ikisema kuwa ni sawa na kitendo cha "uharamia".
Katika taarifa, serikali ya Venezuela ilisema "inahifadhi haki ya kuchukua hatua zozote za kisheria kurekebisha uharibifu huu kwa taifa".

Maafisa wa Marekani walisema ndege hiyo ilikamatwa kwa tuhuma za ukiukaji wa udhibiti wa mauzo ya nje na sheria za vikwazo vya Marekani.

Waliongeza kuwa uchunguzi uligundua kuwa watu wanaohusishwa na Bw Maduro walidaiwa kutumia kampuni ya shell ya Caribbean kuficha kuhusika kwao katika ununuzi haramu wa ndege hiyo kutoka kwa kampuni iliyoko Florida mwishoni mwa 2022 na mapema 2023.

Ndege hiyo kisha ilisafirishwa kinyume cha sheria kutoka Marekani hadi Venezuela kupitia Karibiani mwezi Aprili 2023.

Hoja ya maafisa wa Marekani kwamba mauzo ya ndege hiyo ni kinyume na vikwazo vya Marekani haiwezi kuwa na uzito mkubwa kwa Rais Maduro, ambaye mara kwa mara amekuwa akiishutumu Marekani kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

BBC Swahili
 
Kama ni ndoto ya kila mtu kuishi huko ww mbona hujaenda kuishi huko badala yake upo huku unapingwa vumbi?
Yaani unachukua matamanio yako unawahusisha na watu wengine?
Acha uongo wewe, kwa hiyo wewe ndio unajifanya kupenda vumbi.
 
Marekani inaingilia sana mambo ya ndani ya Venezuela kwa tamaa ya mali.Akina Maduro wako kila nchi inayoitwa ya kidemokrasia.
Nchi ya kidemokrasia tena iwe na akina Maduro kivipi..😛😛😛
 
This is blatant theft on the part of the US government,there is no other way to describe it.But the US government is used to this sort of behaviour.It is stealing Syrian oil and Iraq oil right now as we speak,confiscated more than US $300 million of Russia assets and funds and more.By the way this is not the first time the US is stealing a Venezuelan plane,it also stole a Boeing 747-300M cargo plane in 2022.
 
Unavijua visiwa vinavyoitwa Marshall Islands??
USA na EU wamekuwa wakifanya test za nuke weapons na biological weapons kwa watu wa hivyo visiwa.
Yani watu wa Marshall islands wamegeuzwa kuwa lab rats hadi sasa.
USA and Westerners are the MOST DANGEROUS HUMANS TO BE FEARED.
Mkuu huna unalojua hujui mambo mengi kubali uelimishwe.
Unamjua Julian Assange!?
Alitoa documentary za uvamizi wa kimakosa wa USA nchini Iraq na mauaji ya makusudi ya jeshi la USA kwa raia na waandishi wa habari Iraq.
It means Iraq was falsely accused and invaded.
MKuu tulia uelimishwe.
 
Huyo jamaa akili yake ni stagnant.
Hakuna kitu mtaongea mtaelewana achana naye.
 
Kuna ujinga kwa baadhi ya members humu kufikiri kuwa marekani anajali kuhusu sijui demokrasia na human rights na takataka zake kwa mataifa mengine wanakosea sana.

Marekani huyu anaye ilalamikia China na kuiwekea vikwazo sababu ni nini ? Anasema China inatesa na kuua waislam wa Uyghurs.

Lakini ndio marekani huyu huyu ambaye anazidi kushusha mizigo kwa mizigo ya makombora kwa Israel kuua wapalestina ambao majority ni Muslim kama angekuwa anajali sijui hiyo demokrasia Israel isingeendelea kufanya kile afanyacho miaka na miaka, asingekuwa rafiki wa Saudia, Rwanda............

Marekani anacho tazama siku zote ni maslahi yake sio kingine.

Iraq ana silaha za maangamizi tukamvamia haya Urusi, China, North Korea, Iran wanazo na wanazifanyia mazoezi vile watakavyo waende sasa wakamvamie mmoja wao
 
Hata Marekani sio nchi ya kidemokirasia na ndio maana Trump alilalamika kuibiwa kura.
Au anajifanya hajaliona lile tukio la kufanyika vurugu ofisi za the capitol!?
 
Huwa wanavamiwa wanyonge tu.
Hao uliowataja kuwavamia uagane na nyonga.
 
Akikujibu n tag mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…