Marekani yaikamata ndege ya Rais Maduro wa Venezuela

Marekani yaikamata ndege ya Rais Maduro wa Venezuela

Unafahamu vizuri Kiingereza? Mbona hujaeleza kwa nini USA imechukua uamuzi huo?

Utawala wa kidikteta wa Maduro umewafanya wananchi zaidi ya milioni moja kuwa wakimbizi. Kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na Serikali ya Maduro, USA iliamua kuiwekea vikwazo Venezuela. Lakini zikafanyika njama za kukwepa vikwazo, na kampuni moja ya US ikaamua kufanya biashara na Venezuela. Hivyo ilichofanya USA ni sahihi kabisa kwani ni sehemu ya kuhakikisha maamuzi ya kuiwekea vikwazo vya biashara Venezuela yanaheshimiwa.

Katika uhalisia, pamoja na mapungufu ya hapa na pale, USA na nchi za Ulaya Magharibi, ndiyo mataifa pekee yanayotegemewa kuwa walinzi wa wananchi wote wanaoonewa na kudhulumiwa na tawala dhalimu Duniani. Ndiyo maana wakimbizi wenye uwezo, wanaokimbia tawala dhalimu, kuanzia mataifa ya Kiarabu, Afrika, Asia na Ulaya Mashariki, wanakimbilia kwenye mataifa hayo. Waarabu wanaoonewa na waarabu wenzao huwezi kusikia wanakimbilia kwa waarabu wenzao, wote wanakimbilia Ulaya, labda wakose uwezo wa kufika huko.
Udikteta wa baadhi ya viongozi husababishwa na marekani wenyewe. Marekani wakiona kiongozi wa nchi unaegemea upande ambao wao hawautaki wanafanya njama ya kukuangusha kwa kupandikiza viongozi wa upinzani juu yako. Wakishindwa kukuangusha wanaanza kukutuhumu hufuati demokrasia na kukufitinisha na wananchi wako kwa kukuwekea vikwazo vya kuumiza wananchi wako.
Mwisho wa picha kiongozi anaamua kuhakikisha anasambaratisha watu wote wanaotishia uongozi wake kuondoa ushawishi wa marekani na hapo udikteta ndiyo hutokea. Marekani wenyewe wanataka either ufuate sera na matakwa yao au wakuwekee vikwazo na uonekane dikteta
 
Back
Top Bottom