Unafahamu vizuri Kiingereza? Mbona hujaeleza kwa nini USA imechukua uamuzi huo?
Utawala wa kidikteta wa Maduro umewafanya wananchi zaidi ya milioni moja kuwa wakimbizi. Kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na Serikali ya Maduro, USA iliamua kuiwekea vikwazo Venezuela. Lakini zikafanyika njama za kukwepa vikwazo, na kampuni moja ya US ikaamua kufanya biashara na Venezuela. Hivyo ilichofanya USA ni sahihi kabisa kwani ni sehemu ya kuhakikisha maamuzi ya kuiwekea vikwazo vya biashara Venezuela yanaheshimiwa.
Katika uhalisia, pamoja na mapungufu ya hapa na pale, USA na nchi za Ulaya Magharibi, ndiyo mataifa pekee yanayotegemewa kuwa walinzi wa wananchi wote wanaoonewa na kudhulumiwa na tawala dhalimu Duniani. Ndiyo maana wakimbizi wenye uwezo, wanaokimbia tawala dhalimu, kuanzia mataifa ya Kiarabu, Afrika, Asia na Ulaya Mashariki, wanakimbilia kwenye mataifa hayo. Waarabu wanaoonewa na waarabu wenzao huwezi kusikia wanakimbilia kwa waarabu wenzao, wote wanakimbilia Ulaya, labda wakose uwezo wa kufika huko.