Marekani yaipatia Tanzania billioni 12 kukabiliana na Corona

Marekani yaipatia Tanzania billioni 12 kukabiliana na Corona

Hao ni wadau wa maendeleo na sio mabeberu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
hawa Mabeberu watuache, wana nini na sisi - tumewaomba hiyo doo kwani? watu wengine bana.
 
walete waletu tu tununue sukari hata ikiuzwa elf 10 tutanunua tuuu
 
Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza USD 2.4 M (Tsh. Bil. 5.6) ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara, jitihada za utoaji taarifa na miradi mingine mbalimbali. #MillardAyoUPDATES
•
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani leo imesema fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa USD milioni moja unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya kirusi corona uliotolewa hivi karibuni hivyo kufanya kiasi kipya cha pesa zilizotolewa kwa Tanzania kukabiliana na corona kufikia USD milioni 3.4.
•
Taarifa hiyo imesema kiasi kingine cha dola za kimarekani milioni 1.9 zilibadilishwa matumizi na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya corona na kufanya jumla ya pesa zilizotolewa na Marekani katika kukabiliana na corona Tanzania hadi sasa kufikia jumla ya USD milioni 5.3 (Bilioni 12 Tsh. )
Wanajikomba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zito anajua hili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
(NJE YA MAADA) .Mkuu chama kinamfia mbowe huko,nimeangalia video sasa hivi kuna wabunge wakike wawili wamekihama CHADEMA kisa unyanyasaji wa kingono unaofanywa na DJ Mbowe

Nasikia anatembeza miti kama hana akili timamu kwa wabunge wanawake

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ana miti mingapi?
Wacheni uzushi usiokuwa na macho wala miguu.
Mukiambiwa muthibitishe hoja hizi munaweza?
Natamani nchi hii ingelikuwa inaruhusu Badhi ya Sheria za Kiislamu ya kumsingizia mtu Uzinzi apigwe bakora 80 bila huruma.
Hoja Hii nitaipeleka Bungeni Mwakani ili ipate baraka za watanzania.
Sheria Ikipita Tutawatafuta ili mupate haki yenu stahiki.
Shenzi TaYp.
 
Haya majirani sasa hamuna sababu zingine za kukwama, amsheni madubwasha ya kupima na kutoa taarifa, acheni kuchoka kisa umaskini, mabeberu wamewawezesha....

===================
Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 2.4 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5.6), ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya nchini Tanzania ambapo msaada huu unalenga kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara, kusaidia jitihada za utoaji taarifa, miradi ya maji na usafi wa mazingira, kuzuia na kudhibiti maambukizi, kutoa elimu ya afya kwa umma na miradi mingine.

Fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 1 unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya janga la COVID-19 uliotolewa hivi karibuni na kufanya kiasi kipya cha fedha zilizotolewa kwa Tanzania ili kukabiliana na janga hili kufikia Dola za Kimarekani milioni 3.4. Isitoshe, kiasi kingine cha Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimebadilishwa matumizi na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya janga hili. Hii inafanya jumla ya fedha zote zilizotolewa na Marekani katika kukabiliana na COVID-19 nchini Tanzania hadi hivi sasa kufikia Dola za Kimarekani milioni 5.3 (Sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 12.2).

Taarifa hiyo imeongea kuwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita Marekani imewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 7.5 kwa maendeleo ya Tanzania huku karibu Dola za Kimarekani bilioni 4.9 zikielekezwa kwenye sekta ya afya pekee ambapo toka mwaka 2009 Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 100 kusaidia miradi ya afya na takriban Dola za Kimarekani bilioni 70 kama msaada wa kibinadamu duniani kote.

dar-millardayo.jpg

Imeeleza pia kuwa, Serikali ya Marekani inaendelea kuwa mfadhili mkubwa zaidi duniani wa miradi ya afya na shughuli za kibinadamu zinazolenga maendeleo ya muda mrefu na jitihada za washirika wake kujijengea uwezo na kuchukua hatua za dharura wakati wa majanga. Aidha tunaongoza duniani katika utoaji wa misaada ya kibinadamu na kiafya katika kukabiliana na janga la COVID-19.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Marekani inaendelea kuonyesha uongozi katika jitihada za kimataifa za kukabiliana na janga la COVID-19, Watu wa Marekani wametoa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 10 zitakazosaidia jitihada za kimataifa za kukabiliana na COVID-19 >>> “tutaendelea kuhakikisha kuwa mchango mkubwa wa kifedha na wa kisayansi wa Marekani katika mapambano haya unabaki kuwa kitovu na sehemu ya jitihada za pamoja na zilizoratibiwa vyema za jumuiya ya kimataifa dhidi ya COVID-19”

“Ikiwa ni miezi kadhaa sasa tukipambana na janga hili nchini kwetu na nje ya nchi yetu, Marekani inaendelea kuongoza jitihada za kimataifa dhidi ya mlipuko huu, ikijenga katika uzoefu wa miongo kadhaa ya uongozi katika utoaji misaada ya kiafya inayookoa maisha na misaada ya kibinadamu”

Marekani kuipa Tanzania Bilioni 5.6 za ziada kusaidia kupambana na corona – Millardayo.com
 
Nilijua tu lazima utakuja uzi kama huu
 
Sio kigezo cha kutoa taarifa ya kitu cha kawaida kwetu labda tuwape takwimu za malaria ila corona tutapambana nayo kimya kimya sio lazima tuwape taarifa ya visa, wanataka vya nn kwanza kwani ni ufahari kuwa na visa vingi?
 
Kwani ana miti mingapi?
Wacheni uzushi usiokuwa na macho wala miguu.
Mukiambiwa muthibitishe hoja hizi munaweza?
Natamani nchi hii ingelikuwa inaruhusu Badhi ya Sheria za Kiislamu ya kumsingizia mtu Uzinzi apigwe bakora 80 bila huruma.
Hoja Hii nitaipeleka Bungeni Mwakani ili ipate baraka za watanzania.
Sheria Ikipita Tutawatafuta ili mupate haki yenu stahiki.
Shenzi TaYp.
Ngoja nkuletee video mkuu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walete wasilewe.
Mwendo ni ule ule wa kutotangaza tu.

Masharti ya misaada lazima ifuatwe, ukiwa maskini huna usemi wowote, unapokenua meno ukipokea msaada wao, ujue siku wakikuhitaji lazima uwe tayari kuachia kila kitu hadi wenyewe wachoke.
Waulize machangu inavyokuaga wakati wamelipwa kutoa huduma.
 
TZ sio Kenya wewe narudia tena kukumbusha.

hatukutoa data ili tupewe mikopo,hatutatoa data sababu tumepewa msaada wala mkopo[emoji23][emoji23][emoji23].

unaweza ukaona kwanini tuna kiburi,yaani ukiwa unajiamini bana raha sana.
 
Back
Top Bottom