Marekani yamkamata alievujisha taarifa za siri za kijasusi

Marekani yamkamata alievujisha taarifa za siri za kijasusi

Na nyinyi mna amini maigizo haya ya vyombo vya usalama vya Merikani - hakuna cha uvujaji wa siri zo zozote hizo ni mbinu za kutafuta sababu za kusitisha msaada wa vita kwa Zelensky wamekwisha ona jeshi la Ukraine likisaidiwa na vikozi kutoka Merikani na Uingereza hawawezi kushinda vita hii ndio maana wakabuni mbinu za kutokea kwa kuwasingizia vijana wadogo wanao cheza games za computer - vijana hao wana uwezo gani wa kun hack top Govt military secretes - how?
Umeona mbali sana na kama vile kumaliza corona duniani vikaanza vita vya Russia na Ukraine, na Sasa wamepata sababu ya nitokee au tukio lingine litakalopewa airtime ya kutosha na vita kuisha
 
Afungwe maisha huyo...

Naipenda U.S.A sababu sisi weusi walau tunathaminiwa tunapozamia huko hadi ajira tunapa....haya wahuni wa upande mwingine ruksa kutoa povu [emoji1783][emoji1783]
Afungwr Maisha USA inatubeba sana weusi tukienda kuhemia huko
 
Wapiga Ramli chonganishi washakuja sasa
Intel iko juu ya uwezo wako kufikiri bro.
Ndio maana wanaitwa Intelligence wanao operate kati giza, Secret Service.
Soma habari zote katika media zote, usipoweza kudadavua utatoka patupu everytime.
 
Jack Tixeira (21) mfanyakazi wa Jeshi la Anga la Marekani chini ya kitengo maalumu cha ulinzi wa taifa, ameshtakiwa rasmi katika Mahakama huko Boston kwa kuvujisha nyaraka za siri.

Tixeira ameshtakiwa kwa makosa ya usambazaji wa taarifa za ulinzi pamoja na uhamishaji na uhifadhi wa nyaraka za siri kinyume na sheria. Nyaraka hizo ni mali ya idara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon).

Kuvuja kwa nyaraka hizi kumeifedhehesha Marekani na kumeibua maswali mapya juu ya Usalama wa taarifa za siri.

Kwa ombi la waendesha mashtaka, Tixeira amerudishwa rumande hadi kesi yake itakaposikilizwa Aprili 19. Ikiwa atakutwa na hatia anaweza akahukumiwa kifungo cha takribani miaka 15.

Rais Joe Biden amezishukuru Mamlaka za usalama kwa kuchukua hatua za haraka kuchunguza chanzo cha kuvuja kwa nyaraka hizo.

Vilevile, Biden amelielekeza Jeshi la Marekani na intelijensia kuhifadhi kwa umakini na kupunguza usambazaji wa taarifa zozote za siri.View attachment 2588100
Kawezaje kufika kweny Anga Za kijasusi kijana mdogo
 
Back
Top Bottom