Marekani yamkamata alievujisha taarifa za siri za kijasusi

Marekani yamkamata alievujisha taarifa za siri za kijasusi

Dogo kaleta "damage" kubwa sana kwa Marekani.

Hii ni "big scandal" na yaipita ile ya Edward Snowden.
Ya Snowden na yenyewe ilikuwa kubwa. Zote na Snowden zinalingana
 
Ya Snowden na yenyewe ilikuwa kubwa. Zote na Snowden zinalingana
Snowden akikomba docs kwa kutumia hifadhi ya usb ndogo.

Huyu Jack amepiga picha (still pictures) za docs. Ila bado kuna uwezekano ana docs zaidi alinywila ndani ya mifumo.
 
Nimetoka kumsoma dogo, kazi aliyokuwa anafanya kwenye base ni pamoja na kupitia classified docs na lengo lake halikuwa kuvujisha alikuwa tu anajimwambafy kwenye group ambalo yeye alikuwa admin na baada ya docs kusambaa aliogopa sana na kaanza zipost toka mwaka jana ila zilikuwa hazijasambaa hadi mwaka huu.
Huku tayari kuna watu walikuwa washaivisha Urusi na Chini joho la kudukua hizi taarifa.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kijana Jack Teixeira ambae jana alhamisi alikamatwa kwa makosa ya kuvujisha siri za ujasusi wa Marekani kuhusu vita ya Ukraine, amefunguliwa mashtaka ya ujasusi au espionage.

Mashitaka hayo ni pamoja na kuchukua taarifa hizo za siri, kuzihodhi na kisha kuzisambaza kwenye mtandao wa internet.

Wakitetea mashtaka hayo na kuyaweka mahakamani idara ya ujasusi wa ndani FBI imesema ilianza uchunguzi wake wiki ilopita kwa kumhoji mmoja wa washiriki wa mtandao wa Discord ambae amewaambia kuwa Jack alianza kampeni ya kuweka vyaraka hizo mtandaoni tangia mwezi December mwaka 2022.

FBI wameweka mahakamani vifungu vya mashataka vipatavyo 21 na kueleza kwamba Jack alikuwa cleared yaani kufanyiwa "vetting" mwaka 2021 na hivyo kuaminika kuwa na access ya siri nzito za serikali.

Jack pia alikuwa amepewa uwezo wa kuona siri zaidi za kijasusi za serikali kupitia ruhusa maalum iitwayo SCI au "sensitive compartmented access" ambayo yakuruhusu kuingia kwemnye programs zingine za siri kubwa.

Lakini kwa kuwa Jack amesaini mkataba na serikali uitwao Non -Disclosure Agreement ambao wakutaka uijulishe serikali kwamba umepata nyaraka fulani fulani na unazihodhi na akashindwa kufanya hivyo ni wazi kuwa ametenda kosa la jinai.

Endapo atapatikana na hatia Jack Teixeira anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela.
 
Jack Tixeira (21) mfanyakazi wa Jeshi la Anga la Marekani chini ya kitengo maalumu cha ulinzi wa taifa, ameshtakiwa rasmi katika Mahakama huko Boston kwa kuvujisha nyaraka za siri.

Tixeira ameshtakiwa kwa makosa ya usambazaji wa taarifa za ulinzi pamoja na uhamishaji na uhifadhi wa nyaraka za siri kinyume na sheria. Nyaraka hizo ni mali ya idara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon).

Kuvuja kwa nyaraka hizi kumeifedhehesha Marekani na kumeibua maswali mapya juu ya Usalama wa taarifa za siri.

Kwa ombi la waendesha mashtaka, Tixeira amerudishwa rumande hadi kesi yake itakaposikilizwa Aprili 19. Ikiwa atakutwa na hatia anaweza akahukumiwa kifungo cha takribani miaka 15.

Rais Joe Biden amezishukuru Mamlaka za usalama kwa kuchukua hatua za haraka kuchunguza chanzo cha kuvuja kwa nyaraka hizo.

Vilevile, Biden amelielekeza Jeshi la Marekani na intelijensia kuhifadhi kwa umakini na kupunguza usambazaji wa taarifa zozote za siri.
IMG_20230415_002656.jpg
 
Hakuna mbabe Dunia hii, kila mmoja anajaribu kuishi tu apate msosi na siku ziende

Dogo kawavuruga so called wababe wa Dunia
Kazi kwao sasa maana wasije wakasema mchina nae ana mkono
Hawashindwi kujitetea
 
Halafu huyo dogo eti kaajiriwa 2019,awe ana access na Classified docs kirahisi hivyo bado napata maswali
Itakuwa kweli,maana kama wangetaka kuuza story vizuri zaidi,wangemchukua candidate ambaye ataaminika Kwa audience kirahisi!
 
Huyo dogo rasmi kaisha anza kazi ya "ujasusi" after vetting yake 2021...
Wataalamu wanakuambia ni miongoni mwa talent kubwa sana kwenye ujasusi wa dunia ya sasa kuwahi kutokea..

Idara nzima imempitisha na kuwa na access ya sensitive information akiwa na umri mdogo sana kuwahi kutokea.
 
Nimetoka kumsoma dogo, kazi aliyokuwa anafanya kwenye base ni pamoja na kupitia classified docs na lengo lake halikuwa kuvujisha alikuwa tu anajimwambafy kwenye group ambalo yeye alikuwa admin na baada ya docs kusambaa aliogopa sana na kaanza zipost toka mwaka jana ila zilikuwa hazijasambaa hadi mwaka huu.
Ngumu kumesa bro.
Nyaraka za siri huwa ziko very well protected.
Sasa hiyo release ya documents ni very well planned ili ionyeshe hali halisi ilivyo mbovu Ukraine.
 
TAHADHARI.

si rahisi taarifa kuvuja kiasia hiki

HUU NI MPANGO WA MAREKANI NIMEMSIKIA MCHAMBUZI WA MASWALA YA KIDIPLOMASIA WA KUTOKA UINGEREZA AKISEMA MAREKANI ANAJARIBU KULISHA TAARIFA ZA UONGO KWA DUNIA

KUNA MPANGO WANAUPANGA NA TUTAKUJA KUONA MATOKEO BAADA YA MUDA

-ALISEMA KUWA MAREKANI ANAJARIBU KUTULISHA FALSE INFO


IT WAS ALL PLANNED
Lengo nini?

Wa afrika tunaamini wamarekani kama malaika awakosei au si rahisi kuhujumiwa.
 
""Kumatwa kwa Jack kwafuatia taarifa alozotoa kijana mwingine ambae walikuwa wakicheza pamoja mchezo wa computer na kuona Jack akisambaza taarifa hizo""

Marafiki sio.

Always SNITCHING.

#YNWA
hata mimi ningemripoti huyo Jack hajitambui ndo shida wa watoto wadogo kuwa na access na mambo nyeti ya nchi
 
Mind you, the leak is not that simple.
Marekani kuna upinzani mkubwa dhidi ya vita ya Ukraine.
Marekan ni nchi huru unakosoa na huafanywi lolote labda uguse maisha binafs ya kiongoz, sio China na Urusi unauawa mchana kweupen, Jehanam kule
 
Huo ni ukweli ambao hawataki kuusema wazi.
Marekan watu wapo huru sio Putin alisweka watu elf 3 ili kuendeleza vita Ukraine ila USA iliona raia wameandamana walitoa jeshi lao Vietnam , na serikal inabid iwe hv
 
TAHADHARI.

si rahisi taarifa kuvuja kiasia hiki

HUU NI MPANGO WA MAREKANI NIMEMSIKIA MCHAMBUZI WA MASWALA YA KIDIPLOMASIA WA KUTOKA UINGEREZA AKISEMA MAREKANI ANAJARIBU KULISHA TAARIFA ZA UONGO KWA DUNIA

KUNA MPANGO WANAUPANGA NA TUTAKUJA KUONA MATOKEO BAADA YA MUDA

-ALISEMA KUWA MAREKANI ANAJARIBU KUTULISHA FALSE INFO


IT WAS ALL PLANNED
Nakubaliana na hilo 100%.
Marekani wanatafuta Exit Strategy huko Ukraine
 
Back
Top Bottom