Marekani yamkamata alievujisha taarifa za siri za kijasusi

Nimetoka kumsoma dogo, kazi aliyokuwa anafanya kwenye base ni pamoja na kupitia classified docs na lengo lake halikuwa kuvujisha alikuwa tu anajimwambafy kwenye group ambalo yeye alikuwa admin na baada ya docs kusambaa aliogopa sana na kaanza zipost toka mwaka jana ila zilikuwa hazijasambaa hadi mwaka huu.
Ni kweli alizitoa pale (kwenye group).

Tatizo lipo masuala haya yakiwafikia mazee kama wa GRU wale wa mitandaoni.

Ndo maana zilisambazwa kwa kasi kwa miezi miwili na hakuna jasusi yoyote mahiri wa Marekani alegundua hilo hadi juzi.
 
Kavujisha docs 300 ila assange alivujisha 700000
Assange alikuwa aliuziwa au kupewa na alieiba hizo nyaraka na si kwamba ni yeye alikuwa akidukua mitambo na kuingia front.

Huyu dogo ni kama Snowden kwamba wana access na Documents na wameamua kuchukua kiasi na haijulikani ni kiasi gani cha docs anazo.

Hiyo ya 300 unosema ni ndogo sana zipo taarifa zaidi ambazo zingine hazijawekwa hadharani.
 
Jack Teixeira kijana mwenye umri wa miaka 21 ambae ni mwanajeshi katika jeshi la anga la Air National Guad ambalo lipo katika mji wa Masachusetts.

Kijana huyo tayari yupo mikononi mwa FBI na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya Espionage.

Jack amekamatwa mchana huu nyumbani kwake kwenye kitongoji cha Swansea ambapo ameonakana akiwa amefungwa pingu.

Kukamatwa kwa Jack kwafuatia taarifa alozotoa kijana mwingine ambae walikuwa wakicheza pamoja mchezo wa computer na kuona Jack akisambaza taarifa hizo.

Hadi sasa imefahamika kuwa taaarifa hizo zilitokea katika mchezo wa computer yaani "online game" na zilikuwa katika vipande vipande yaani "slides", zikielezea mipango yote ya majeshi ya Ukraine dhidi ya Russia kuanzia mwishoni mwa mwezi March mwaka huu.

Lakini uthibitisho kuwa taarifa hizo ni za kweli bado haujawa wazi ingawa zaonesha udhaifu mkubwa wa majeshi ya Ukraine na matumizi ya hovyo ya silaha jambo linopelekea kumaliza akiba ya silaha walokuwa wakipewa na nchi za NATO.

Pia taarifa hizo zaonyesha idadi kubwa ya majeshi maalum yaani "special forces" kutoka nchi za NATO vikiwemo vikosi vya UK ambao Russia yawachukulia kuwa ndo wachagizaji wakuu wa vita hiyo.

Uvujaji wa taarifa hizo umewastua maofisa wengi wa serikali ya Marekani akiwemo mkuu wa Pentagona ambae nae amesema hafahamu imekuwaje na kudai kuwa taarifa hizo zilikuwa mahala fulani mtandaoni na "hata hata yule aliekuwa amezipata kwa wakati huo hajulikani", amedai waziri wa Ulinzi Llyod Austin.

Shirika la habari la AP lilidai kuwa taarifa hizo za siri huenda zilianikwa katika ukumbi wa mazungumzo au "Chart Room" utumiwao na wachezaji michezo ya computer ujulikano kama Discord na haijulikani idadi halisi ya taarifa hizo na yasadikiwa kuwa ni mamia kwa mamia.

Jack na wenzie wapatao 20 waliunda kikundi chao hichi cha kucheza game online wakati wa Pandemic na wakawa wameshibana.
Wanatuchora tu hao,i don't trust them
 
Nyaraka muhimu zilikuwa mikononi mwa kijana mdogo kabisa......zaidi ya uzembe huo.
 
Huku kuvuja inaweza ikawa mbambamba tu.
Yaweza kuwa vyovyote vile lakini lazima iwe established dogo amewezaje kupata hizi documents.

Kumbuka katumia muda kupiga picha za docs na si kwamba amechukua docs halisi.

Sasa ni mara ngapi alikuwa afanya hivyo na nani alikuwa nae na mambo mengine.
 
Nyaraka muhimu zilikuwa mikononi mwa kijana mdogo kabisa......zaidi ya uzembe huo.
Kuna kitendawili hapo.

Kwa ninavyofahamu zipo levels za access kwenye sensitive areas khasa hiyo kazi yake ambayo yaonyesha alikuwa akifanya "reconnaissance missions" au alikuwa akiziweka sawa docs kutoka huko.

Hivyo lazima supervisor au top bos alie kwenye zamu awe makini na nani na level ipi ya access mtu fulani aruhusiwa.
 
Back
Top Bottom