Marekani yamuua Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Iran katika shambulio la roketi la uwanja wa ndege wa Baghdad

Mimi nachojua waarabu walipigwa....kuhusu walipigwaje hayo jua wewe..
Kwani intellijensia sio uimara wa kijeshi??
Unaweza toa sababu kwanini Israel walishinda mpaka kesho kutwa lakini hata kama wangekuwa wanapigania uhai wao kama uwezo (inteligency,military,tactics) wasingekuwa navyo hata kama morali ya kupigania existence ingekuwa kubwa kiasi gani WASINGESHINDA...
Lakini ukweli ni kuwa saivi Israel kawapiga gep wengi Kwenye technology ya kivita saiv...so the next Israeli war will be total obliteration of enemies
Kasome six days war, usiwe unasikia story kwenye vijiwe mkuu, soma kwa nini Israel ni undefeated till now dhidi ya
waarabu, usikae ukisema tu wapo mbali kwenye nguvu za kijeshi wakati wanapambania existence yao juu ya waarabu hapo
middle east, hata wanamgambo Libya walimmaliza Muammar kwa aid toka western. So usije ona Israel anapigania mipaka
yake uka dhani ataweza kuja simama na Nations kama China,India,Turkey,Russia,South Korea au Iran ukadhani itakuwa kama hio ya 1967 six days war, bro haitakuwa kama unavyoongea kishabiki.

Iran vita ya 1980 ilipambana na Iraq wakati huo Saddam anatisha ikiwa supported na mataifa ya kiarabu zaidi ya 8 ikiwemo Saudia na Kuwait pia walipewa msaada wa kijeshi na USA pamoja na Soviet Union, waliokuwa wakimsaidia allies wa Iran ilikuwa ni Syria na Libya tu, lakini ilipigwa vita 1980 mpaka 88 na UN kuingilia kati hakuna aliyetoka mshindi zaidi ya Iraq kuzidiwa.

Israel haiwezi kuikabili Iran, Israel haina technology Iran hawana, Israel iache ipambanie existence yake, ukitaka iingie kwenye vita na taifa kama Iran ndio mwisho wa existence yao middle East, Iran ina vikundi vingi middle East, tupo hapa.
 
Wewe kweli akili zako mchichapori..
Sababu ya kupigana haikufanyi ushinde vita ila uwezo wa kupigana ndo unakufanya ushinde..
Unaponiambia israel alishinda kwasababu anapigania existence unaongea pumba
Israel alipigana nao waarabu directly yaani Egypt ,jordan,Syria lakini kwa Iran na Iraq...iran hakupigana directly na wasaidizi wa Iran
Kwanza sadam alikuwa punga unaweza ukapewa silaha ukashindwa kuzitumia
Halafu kuhusu military technology Israel is by far the best as of now.. Hata hayo mabeutiful equipments ambayo bwana trump anajisifia kuspend 2tril dollars over. .mengi yametengenezwa na kampuni za Israel..hizo new drones za mmarekani zimetengenezwa israel hata zile drones ambazo Iran alitumia kumpiga Iraq alipewa na muisrael(yes Iran alisaidiwa na Israel) sasa hawa jamaa usiwachukulie simpo na sio kila technologia waliyo nayo wameiuza ...siku kikinuka ndo utashangaa mtume na maria Iran hionekani Kwenye ramani
 
Israel haiwezi kuikabili Iran, Israel haina technology Iran hawana
Ndugu, una ushahidi wa hiki ulichokiandika?

Based on facts, taifa lenye nuclear triad linaweza kushindwa kukabiliana na taifa ambalo ni non-nuclear? Hicho ni kigezo kimoja tu.

Unadhani hayo mataifa kama China, Uturuki, India, SK, Iran n.k. yataweza kustahimili vita na Israel endapo nukes zikitumika?
 
Kumbe bado hatujaelewana ninachomaanisha ni kwamba siku ukisikia Israel imepigwa haki ya mungu ndio mwisho wao hapo middle East, ndio maana huwezi sikia imeshindwa, siku ikishindwa Israel haipo, vita ya Israel na waarabu sio ya kwawaida au vinginevyo ni waarabu hawawataki Israel pale. Kwa hio Israel akidundwa anatoka pale, sio ile vita ya USA kwenda kuiba mafuta middle East au Tanzania na Uganda, nasema hivo kwa sababu watu wanasema Israel kila vita inashinda, ndio acha ishinde, ikishindwa tunazungumza mengine tena.
Existence yake middle east ndio ushindi wake hicho ndicho namaanisha, kama una mawazo finyu huwezi elewa kwa sababu usifikiri Israel hawapati hasara kwenye hizo vita za kila siku.

Vita ya Israel ya six days war ni kama bondia kupiga punching bag, mkuu nimesema soma hio vita uelewe, Israel ili strike kabla ya, nadhani umenipata.

Huna uthibitisho hizo silaha za USA imetengeneza kampuni ya Israel, hebu sema hata moja mkuu usiongee hadithi za vijiweni, toa evidence, usiwe una kariri tu na kusikia Israel anatengeneza silaha US bila ya kufuatilia.

Nakwambiaje iache Israel iendelee kupambana na Hamas na Hezbollah vita ya Iran usitarajie.
 
Ndugu, una ushahidi wa hiki ulichokiandika?

Based on facts, taifa lenye nuclear triad linaweza kushindwa kukabiliana na taifa ambalo ni non-nuclear? Hicho ni kigezo kimoja tu.

Unadhani hayo mataifa kama China, Uturuki, India, SK, Iran n.k. yataweza kustahimili vita na Israel endapo nukes zikitumika?
Asante sana, Israel kuwa na nukes doesnt mean atashinda, Iran kuna wakati ilisema Israel ikishambulia itaokota vipande vya Tel-Aviv, Sasa tujiulize Iran ina jiamini kiasi gani wakati ipo wazi Israel ina nukes?

Ukiachilia mbali nukes Israel inazidiwa askari, pia population x10.

Iran ina allies wengi katika eneo hilo Syria,Iraq,Qatar, Kusini mwa Yemen,Palestine na Turkey hao wote ni allies wake hapo ina maana Iran inaeza fanya shambulizi la hatari kupitia Hezbollah, Syria au Iraq.
Hezbollah ina zaidi ya kombora 100,000 zote zimeipoint Israel, unaweza soma 2006 war Hezbollah alichomfanya Israel hapo hujachanganya na kombora toka Iran pia.

Tukiachilia mbali hao allies wakubwa pia kuna vikundi vya kishia katika eneo vinavyomuunga mkono Iran kama The Badr Brigade ,The Imam Mahdi Army , The Fatimeyoun Militia na The Popular Mobilization kama hilo kundi la the Popular Mobilization wana askari zaidi ya 150,000, Najua Israel ina askari wana range kwenye 170K mpaka 180k active kwenye service.

Ranks za global fire power Index Israel inazidiwa na Iran 13 kwa 17.

Haya tuje sasa kwenye nukes unazosema, mkuu vita itakapoanza Iran itarudi haraka sana kutengeneza silaha za nuclear na jamaa hawana wasi wapo tayari.
Iran inaweza enrich uranium ndani ya siku 5 tu kufikia kiwango cha kutengeneza bomb la nuclear, enrichment inadaiwa ni kwa 20% kiasi ambacho kitatosha kabisa kutumia kuunda silaha ya nuclear, so usifikiri Iran haijui nini cha kufanya kama Israel ana nuclear na wataingia vitani, utashangaa kuna kombora za nukes za hatari na dunia itashangaa.
Iran: Five days needed to ramp up uranium enrichment

Kwa hio Iran ina uwezo kabisa wa kuitandika Israel tukiacha ushabiki.
 
Sawa! Ila maelezo yako bado kwa kiasi kikubwa hayajakidhi haja ya maswali haya mawili;

1. Taifa lenye nuclear triad linaweza kushindwa kukabiliana na taifa ambalo ni non-nuclear?

2. Unadhani hayo mataifa kama China, Uturuki, India, SK, Iran n.k. yataweza kustahimili vita na Israel endapo nukes zikitumika?

Israeli inakadiriwa kuwa na silaha takribani 100 za kinyuklia na zenye uwezo wa kuwa launched kupitia platforms tofauti tofauti. Silaha zao tayari zipo katika deployment na utayari wa kufanya mashambulizi muda wowote tofauti na hicho unachokisema kuhusu Iran.

Kwa namna yeyote itakapo tokea vita (Conventional Warfare) yenye adhari za kutishia uwepo wa taifa hilo unafikiri watashindwa kuzitumia nukes zao kuimaliza vita?

Iran hata kama itakuwa ikipigana indirect kwa kutumia vikundi vya wapiganaji, unadhani hawa Israel pamoja na vitengo vyake vya Kijeshi na Kiintelijensia vitakapoona kuna tishio kubwa katika mustakabali wa taifa lao pale Mashariki ya Kati, unadhani watashindwa kufyatua makombora kuelekea mainland Iran ili kulinusuru taifa lao?

Na Israel itakapofanya hivyo, unadhani mustakabali wa taifa la Iran utakuwaje?
 
  • Thanks
Reactions: PNC

Inategemea ni taifa gani vs taifa gani, ndio maana nimekueleza vizuri tu, swali lako na nimetolea maelezo, Tanzania ikiwa na nuclear itapigwa vizuri tu na Egypt na nuclear yao, kumbuka tunazungumzia Iran Vs Israel.

Nachosema ni kwamba vita ikianza usifikiri nuclear ndio itamaliza vita, nuclear yaweza kuwa intercepted vile vile, Nuclear ni silaha ya mass destruction, na unapozungumzia mass destruction kuna chemical weapons ambazo ni far more dangerous sana kuliko nuclear amini nachosema, kibaya zaidi biological weapon hata kwenye maabara ya kawaida inaweza tengenezwa, sasa Israel irushe nuclear, means no way out, hio inakuwa ni vita ya kufa na kupona, tazama eneo la Israel na Iran, Tazama population halafu ujiulize mwenyewe nani ataumia zaidi wakianza vita ya mass destruction plus Iran itaweza kutengeneza nuclear bomb in no time.
Nuclear ikipigwa inaweza leta athari up to 20km in radius, and nuclear usisahau can be intercepted too.

Israel haiwezi jipima ubavu na hayo mataifa amini nachosema, China ana mass destruction weapons zikiwemo nuclear na chemical weapons, kibaya zaidi china na India wana hydrogen bomb, hydrogen bomb ni bomb baya kabisa hata nuclear haifuati, nuclear haifuati hata robo kwa hydrogen bomb, zile bomb zilizopigwa Nagasaki na Hiroshima yalikuwa na uwezo wa 15kilotons na 20 kilotons lile la pili, but hydrogen bomb USA walilojaribu 1952 lilikuwa na 10000 kilotons, sasa umeelewa Israel itakuwaje ikishushiwa hydrogen bomb moja tu, in any means Israel haiwezi simama hata na India.
 
Shukrani kwa maelezo yako ila bado yanaongeza maswali mengi kuliko majibu.

Tanzania haina mpango wa nuclear triad na wala haimiliki silaha za nyuklia achilia mbali nishati yake, hivyo mfano wako huo ni irrelevant.

Jaribu kujikita kwenye facts zilizopo na si mifano isiyo na uhalisia wa kile tunachokijadili hapa.

Swali bado linabaki pale pale: Taifa lenye nuclear triad linaweza kushindwa kukabiliana na taifa ambalo ni non-nuclear?

Tambua kwamba Nuclear Triad ni mfumo wa nyuklia uliojengwa mahsusi kwa ajili ya ulinzi katika nyanja zote za kiulinzi na huwezi kuujenga kikamilifu mfumo huu na ukashindwa kuutumia. Israel imekuwa ikijishughulisha na hili tangu miaka ya sitini (1960s).

Ukizungumzia chemical weapons huwezi kuacha kuitaja Israel sababu wamekuwa wakizifanyia kazi tangu miaka ya themanini (1980s), na si jambo geni kwao, they have the capabilities both offensive and defensive.

Kumbuka kwamba mwanzoni nilitumia kigezo kimoja tu cha silaha za nyuklia na kama ukiongeza na kigezo hicho cha chemical weapons, you do the math.

Umesema kuwa Israel haiwezi kujipima ubavu na China, India n.k. Unadhani ni kwanini Israel imeunda makombora ya masafa marefu (ICBM) yenye kupiga shabaha za mbali za hadi kilometa 10,000 achilia mbali maadui zake wakuu wapo karibu naye?
 
Nashukuru sana nadhani tutaelewana mkuu.
Tanzania haina mpango wa nuclear triad na wala haimiliki silaha za nyuklia achilia mbali nishati yake, hivyo mfano wako huo ni irrelevant.

Jaribu kujikita kwenye facts zilizopo na si mifano isiyo na uhalisia wa kile tunachokijadili hapa.
Nilimaanisha inategemea na taifa gani vs taifa gani kwa mambo mengi, usiseme tu nuclear kuna facts nyingi lazima ziwe considered ili kujua, na hizi facts haziepukiki ndio maana nimetoa mfano kama huo. tuachane na hili.

Swali bado linabaki pale pale: Taifa lenye nuclear triad linaweza kushindwa kukabiliana na taifa ambalo ni non-nuclear?
Labda nikujibu hivi, tunatoa uhalisia sasa, japo umepinga mfano wangu, vita ya Taifa moja lenye nuclear vs non-nuclear hapo inajulikana atapigwa asiye na nuclear, lakini in real battle tena hasa hii vita ya Israel vs Iran, Israel haitoanza kwa kupiga nuclear, vita ikitangwazwa ndio utajua Iran nuclear imetolea wapi, na pia nimesema toka mwanzo kama ni vita ya nuclear hio ni mass destruction, kwa hio mkuu tarajia kuona mambo mapya kabisa na nuclear inanunuliwa mkuu, kama Israel ilivokuwa ikinunua uranium toka France in 1960s.

Niruke kwenye swali lingine huko nimeelezea kabisa mpaka facts za chemical weapons, area, population vita matter, huelewi nini mkuu?

Umesema kuwa Israel haiwezi kujipima ubavu na China, India n.k. Unadhani ni kwanini Israel imeunda makombora ya masafa marefu (ICBM) yenye kupiga shabaha za mbali za hadi kilometa 10,000 achilia mbali maadui zake wakuu wapo karibu naye?
Israel imetengeneza hizo kombora kujihami tu lakini sio kwamba itashinda ikiingia vitani na India au China kisa ina 10000km range misiles.

Naomba tumalize kama ifuatavyo mfano, China ikiingia vitani na Israel kwa vita ya nuclear na isiyo ya nuclear Israel itapigwa kwa facts zifuatazo.

1-China ina war heads kama 250 kama wanalingana na Israel japo wataalamu wanasema China ina 1700 warheads.

2-Kombora wanalojivunia Israel ni Jericho 3 ambapo hata kwenye kumi bora ya makombora ya masafa halipo, Jericho 3 inaweza fika hadi 10000km ila kwa kupunguzwa uzito fulani(iwe chini ya payload yake ya kawaida ambapo ni 1000kg), lakini range yake kabisa ni kati ya 4500 mpaka 6500 ikiwa na payload ya 1000kg, kwa hio Jericho 3 Beijing haifiki mkuu.

Jericho 3 payload yake ni 1000 to 1300 kg wakati DF ya china ina payload ya 2500kg

Jericho 3 imefeli mara 3 nje ya 9 wakati wana launch, sasa tazama mwenyewe in case of war what could happen, China ina kombora za masafa ambapo zipo kwenye list ya kombora zenye long range labda nikupe list.

R-36M (SS-18 Satan), Russia – 16,000km

Dongfeng-41 (DF-41, CSS-X-10), China – Between 12,000km and 15,000km

DongFeng 5A (DF-5A), China – 13,000km

Hwasong-15, North Korea – 13,000km

R-29RMU Sineva (RSM-54), Russia – 11,547km

UGM-133 Trident II (Trident D5), US – 11,300km

DongFeng 31 A (DF-31A), China – 11,200km

RT-2UTTKh Topol-M, Russia – 11,000km

Minuteman-III (LGM-30G), US – 10,000km

M51 ICBM, France – 10,000km

China ana hizo missile zake za series ya DF na JL ambapo zina range kubwa zaidi kuliko hio jericho 3 Israel inayojivuna.

3-Israel inaingia mara 2 kwa Beijing tu peke ake kwa vita ya nuclear tuseme kila mmoja apige bomu la nuclear lenye radius ya 10km radius damage, Israel itapigwa bomu 80 tu inaishilia yote, China ni kubwa mara 450 ya Israel sasa piga hesabu mwenyewe uone Israel itakua na hali gani.

4-facts ya watu ndio kabisa niache kabisa unajua mwenyewe India na China zinafuatana kwa population.

Hitimisho kwa vyovyote vile Israel haiwezi mkuu, haiwezi kabisa amini nachosema, tunaiona bingwa tokana na kukabiliana na wanyonge.
 
Kwa mara nyingine tena nikushukuru kwa maelezo yako hayo ndugu na pia kwa mara nyingine tena bado kuna 'Ukakasi' katika baadhi ya hoja zako.

Nitauelezea vyema 'Ukakasi' huo:

Niliuliza hapo awali kabisa kuwa;

Taifa lenye nuclear triad linaweza kushindwa kukabiliana na taifa ambalo ni non-nuclear?

Kwa sasa umelijibu swali hili kama ifuatavyo hapo chini;
vita ya Taifa moja lenye nuclear vs non-nuclear hapo inajulikana atapigwa asiye na nuclear

Kwa jibu hilo ndugu, kwa kiasi fulani tumepaweka sawa pale mwanzoni kabisa nilipouliza hilo swali lenye wino mzito katika post #664.

Nilielezea katika bandiko langu lililopita angalau kidogo kuhusiana na mfumo wa Nuclear Triad. Maelezo ya kirefu zaidi nakumbuka nilishawahi kuyatoa humu humu jukwaani miaka ya nyuma.

Kwa taifa lililojizatiti kwa kufanya research & developments za kutosha kwa miaka zaidi ya 50 katika masuala haya ni factor kubwa sana ya uimara wake katika masuala ya kivita.
***

Twende sasa moja kwa moja katika 'Ukakasi':

real battle tena hasa hii vita ya Israel vs Iran, Israel haitoanza kwa kupiga nuclear
"Real Battle" ni battle ya namna gani?

Nina-assume kuwa unamaanisha vita ya ana kwa ana kati ya mataifa hayo mawili. Yaani 'Direct Military Confrontation'.

Nilishazungumzia kuhusu hili hapo awali na niligusia vita ya silaha za kawaida kabla ya kuhusisha silaha za nyuklia na nilihoji kama ifuatavyo:
Kwa namna yeyote itakapo tokea vita (Conventional Warfare) yenye adhari za kutishia uwepo wa taifa hilo unafikiri watashindwa kuzitumia nukes zao kuimaliza vita?

Iran hata kama itakuwa ikipigana indirect kwa kutumia vikundi vya wapiganaji, unadhani hawa Israel pamoja na vitengo vyake vya Kijeshi na Kiintelijensia vitakapoona kuna tishio kubwa katika mustakabali wa taifa lao pale Mashariki ya Kati, unadhani watashindwa kufyatua makombora kuelekea mainland Iran ili kulinusuru taifa lao?

Katika masuala ya kivita ya kinyuklia (Nuclear Warfare), kila nchi yenye kumiliki silaha za nyuklia ina sera ama policies ilizojiwekea kuhusiana na matumizi ya silaha hizo. Hizi ni facts zilizopo!

Kuna mataifa ambayo yana policies zinazoainisha matumizi ya silaha za nyuklia dhidi ya mataifa yenye silaha hizo za nyuklia pekee. Yaani nchi husika itatekeleza shambulizi la kinyuklia endapo itakuwa imeshambuliwa na taifa jingine kwa silaha hizo za nyuklia na wala haitazitumia dhidi ya taifa lisilo na silaha hizo.

Lakini, Je unazifahamu vizuri policies za kinyuklia katika mataifa mbalimbali hususani Israel?

Kuna kitu kinaitwa Samson Option ambacho kimejaribu kuainisha kuhusu matumizi ya silaha za nyuklia za Israel na wakati ambapo matumizi yake yatakuwa ni ya lazima dhidi ya nchi adui. Kipo kitabu chenye maelezo juu ya hiki ninachokisema; The Samson Option cha mwaka 1991.

Jambo jingine, unaposema kuwa;
vita ikitangwazwa ndio utajua Iran nuclear imetolea wapi

Kwamba vita ikitangazwa ndiyo nitajua Iran nuclear imetolea wapi? hiyo moja kwa moja ni kauli isiyokuwa supported na facts bali ni kama kauli ya kubashiri jambo (Guessing). Kwanini nisubiri vita itangazwe? Ni nini basi maana ya mjadala? Kwanini tusijikite katika taarifa na tafiti zenye kuakisi wakati uliopo ili kujengea hoja?

Unaweza kuwa na hoja nzuri lakini katika njia ya uwasilishaji wako ukaifanya ile hoja kwa namna moja ama nyingine kupoteza 'mashiko'.

Israel imetengeneza hizo kombora kujihami tu
Ni kweli kabisa na ninakubaliana na wewe kuwa, makombora hayo ni kwaajili ya kujihami.

IN FACT kila nchi yenye makombora ya nyuklia duniani ni kwaajili hiyo hiyo ya kujihami. Marekani, Urusi, China, Uingereza, Ufaransa n.k. wote hao makombora yao ni kwaajili ya kujihami yaani 'Deterrence'.

sio kwamba itashinda ikiingia vitani na India au China kisa ina 10000km range misiles.
Kabla ya kwenda moja kwa moja katika 'Ushindi' wa vita, kuna suala la makabiliano au mapambano katika vita husika baina ya pande mbili hizo.

Katika vita ya kinyuklia, Ili kuweza "kukabiliana" na mashambulizi ya kinyuklia dhidi ya taifa jingine ni lazima taifa husika liwe na uwezo wa kujibu shambulizi/mashambulizi na hapo ndipo ule mfumo wa Nuclear Triad unapofanya majukumu yake.

Kitendo cha nchi kuweza kuyajibu mashambulizi ya kinyuklia kwa silaha hizo hizo za nyuklia ndiyo njia moja wapo ya "kukabiliana" na mashambulizi ya nyuklia kwa maana ya kuweza kupeleka adhari kwa adui aliyekushambulia na kuleta adhari upande wako. Kwahiyo suala si kushinda, bado suala ni "Kukabiliana" kwanza.

Kombora wanalojivunia Israel ni Jericho 3 ambapo hata kwenye kumi bora ya makombora ya masafa halipo, Jericho 3 inaweza fika hadi 10000km ila kwa kupunguzwa uzito fulani(iwe chini ya payload yake ya kawaida ambapo ni 1000kg), lakini range yake kabisa ni kati ya 4500 mpaka 6500 ikiwa na payload ya 1000kg, kwa hio Jericho 3 Beijing haifiki mkuu.
Umetaja Jericho III.

Makombora ya Balistiki uhusisha factors nyingi wakati wa kufanyiwa deployment na kisha kusafirishwa kuelekea katika shabaha iliyokusudiwa. Moja ya factors hizo ni 'payload delivery'.

Uzito wa payload ni kitu kinachoathiri mwendo wa makombora haya ya Balistiki na ndiyo maana kimahesabu suala hilo huzingatiwa ili kupata kipimo sahihi cha uwezo wa kombora husika kusafiri na kufanikiwa kuumaliza mwendo wake (Range).

Kwahiyo kutokana na vyanzo mbalimbali kumekuwa na utofauti wa vipimo kulingana na hizo factors mbalimbali. Kuhusu Jericho III na kwa kuzingatia hicho nilichokisema vipo vyanzo vinavyoweka kiwango chake cha juu zaidi cha mwisho wa masafa kuwa ni kilometa 11,500 na vipo vyanzo ambavyo vimeweka chini ya hapo.

Kwahiyo kwa kuzingatia factors hizo, mass of payload, technologies kama warhead miniaturization, pamoja na modifications mbalimbali za hata pia makombora mengineyo kama Jericho II, Beijing is within range. Pia bila kusahau miji mingine mashuhuri kama Shanghai, Shenzhen, Guangzhou n.k. yaweza kuwa targeted.

Jericho 3 imefeli mara 3 nje ya 9 wakati wana launch
Sikatai kuhusu majaribio ya silaha kupata hitilafu ama ajali za hapa na pale kutokea katika sites za majaribio ya silaha maana matatizo haya huzikumba nchi zote zenye nguvu kijeshi katika nyakati tofauti tofauti.

ILA, hoja yako hii ina 'hang'. Kwamba Jericho 3 imefeli mara 3 nje ya 9? Lini? Kwa sababu zipi? Na ni kipi chanzo cha taarifa hiyo?

kila mmoja apige bomu la nuclear lenye radius ya 10km radius damage, Israel itapigwa bomu 80 tu inaishilia yote
Sawa! Lakini hapa umezungumza kiwepesi sana.

China ni kubwa sana kijiografia ukilinganisha na Israel lakini hilo halimaanishi kuwa Israel haiwezi kukabiliana na mashambulizi kutoka China. Silaha za nyuklia na facilities zake haziwekwi maeneo ya wazi kama uonavyo supermarkets, matawi ya benki n.k. Nuclear facilities pamoja na mifumo mingineyo inayoiwakilisha Nuclear Triad kwa ujumla wake ni highly classified na yenye miundombinu imara sana ya kuilinda dhidi ya mashambulizi ya kinyuklia.

Hivyo basi, bado kunaiwezesha nchi husika kufanya 'second strike' yaani kujibu mashambulizi hata kama asilimia kubwa ya taifa hilo litakuwa limeadhiriwa na mashambulizi ya adui.

Nimalizie kwa kusema kuwa; udogo ama ukubwa wa nchi kijiografia si kigezo cha msingi cha kuweza kukitumia kama advantage ya kuhimili mashambulizi ya kinyuklia, bali ni uwezo wa nchi husika wa kuweza kujibu mashambulizi endapo itakaposhambuliwa isitoshe main purpose ya silaha za nyuklia ni kupiga shabaha 'strategic' zitakazoleta adhari kubwa zaidi kwa mustakabali wa nchi lengwa.

Ahsante!
 
Asante sana, Israel kuwa na nukes doesnt mean atashinda, Iran kuna wakati ilisema Israel ikishambulia itaokota vipande vya Tel-Aviv, Sasa tujiulize Iran ina jiamini kiasi gani wakati ipo wazi Israel ina nukes?

Ukiachilia mbali nukes Israel inazidiwa askari, pia population x10.

Iran ina allies wengi katika eneo hilo Syria,Iraq,Qatar, Kusini mwa Yemen,Palestine na Turkey hao wote ni allies wake hapo ina maana Iran inaeza fanya shambulizi la hatari kupitia Hezbollah, Syria au Iraq.
Hezbollah ina zaidi ya kombora 100,000 zote zimeipoint Israel, unaweza soma 2006 war Hezbollah alichomfanya Israel hapo hujachanganya na kombora toka Iran pia.

Tukiachilia mbali hao allies wakubwa pia kuna vikundi vya kishia katika eneo vinavyomuunga mkono Iran kama The Badr Brigade ,The Imam Mahdi Army , The Fatimeyoun Militia na The Popular Mobilization kama hilo kundi la the Popular Mobilization wana askari zaidi ya 150,000, Najua Israel ina askari wana range kwenye 170K mpaka 180k active kwenye service.

Ranks za global fire power Index Israel inazidiwa na Iran 13 kwa 17.

Haya tuje sasa kwenye nukes unazosema, mkuu vita itakapoanza Iran itarudi haraka sana kutengeneza silaha za nuclear na jamaa hawana wasi wapo tayari.
Iran inaweza enrich uranium ndani ya siku 5 tu kufikia kiwango cha kutengeneza bomb la nuclear, enrichment inadaiwa ni kwa 20% kiasi ambacho kitatosha kabisa kutumia kuunda silaha ya nuclear, so usifikiri Iran haijui nini cha kufanya kama Israel ana nuclear na wataingia vitani, utashangaa kuna kombora za nukes za hatari na dunia itashangaa.
Iran: Five days needed to ramp up uranium enrichment

Kwa hio Iran ina uwezo kabisa wa kuitandika Israel tukiacha ushabiki.
Sasa inasubiria nini kuifuta kwenye ramani ya dunia. Israel inajilinda aingie basi mle aifute aone moto wake maamaee. Siyo mchezo pale kumbuka yakobo baba wa Israel alipigana na malaika wa Mungu sasa waje hawa Shia
 
Iran hana uwezo wa kwenda kwenye open war na USA, labda ajifiche kwenye proxy zake afanye mashambulizi ya kujificha gizani. Tofauti na hapo Iran itakuwa Libya ya pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Atajifiicha vipi wakati marekani anadai wale militias wa Iraq ni wanapokea amri toka iran?,kwa hiyo hata hao walishambulia marekani anatakiwa ashambulie iran
 
Back
Top Bottom