Kwa mara nyingine tena nikushukuru kwa maelezo yako hayo ndugu na pia kwa mara nyingine tena bado kuna 'Ukakasi' katika baadhi ya hoja zako.
Nitauelezea vyema 'Ukakasi' huo:
Niliuliza hapo awali kabisa kuwa;
Taifa lenye nuclear triad linaweza kushindwa kukabiliana na taifa ambalo ni non-nuclear?
Kwa sasa umelijibu swali hili kama ifuatavyo hapo chini;
vita ya Taifa moja lenye nuclear vs non-nuclear hapo inajulikana atapigwa asiye na nuclear
Kwa jibu hilo ndugu, kwa kiasi fulani tumepaweka sawa pale mwanzoni kabisa nilipouliza hilo swali lenye wino mzito katika post #664.
Nilielezea katika bandiko langu lililopita angalau kidogo kuhusiana na mfumo wa Nuclear Triad. Maelezo ya kirefu zaidi nakumbuka nilishawahi kuyatoa humu humu jukwaani miaka ya nyuma.
Kwa taifa lililojizatiti kwa kufanya research & developments za kutosha kwa miaka zaidi ya 50 katika masuala haya ni factor kubwa sana ya uimara wake katika masuala ya kivita.
***
Twende sasa moja kwa moja katika 'Ukakasi':
real battle tena hasa hii vita ya Israel vs Iran, Israel haitoanza kwa kupiga nuclear
"Real Battle" ni battle ya namna gani?
Nina-assume kuwa unamaanisha vita ya ana kwa ana kati ya mataifa hayo mawili. Yaani 'Direct Military Confrontation'.
Nilishazungumzia kuhusu hili hapo awali na niligusia vita ya silaha za kawaida kabla ya kuhusisha silaha za nyuklia na nilihoji kama ifuatavyo:
Kwa namna yeyote itakapo tokea vita (Conventional Warfare) yenye adhari za kutishia uwepo wa taifa hilo unafikiri watashindwa kuzitumia nukes zao kuimaliza vita?
Iran hata kama itakuwa ikipigana indirect kwa kutumia vikundi vya wapiganaji, unadhani hawa Israel pamoja na vitengo vyake vya Kijeshi na Kiintelijensia vitakapoona kuna tishio kubwa katika mustakabali wa taifa lao pale Mashariki ya Kati, unadhani watashindwa kufyatua makombora kuelekea mainland Iran ili kulinusuru taifa lao?
Katika masuala ya kivita ya kinyuklia (Nuclear Warfare), kila nchi yenye kumiliki silaha za nyuklia ina sera ama policies ilizojiwekea kuhusiana na matumizi ya silaha hizo. Hizi ni facts zilizopo!
Kuna mataifa ambayo yana policies zinazoainisha matumizi ya silaha za nyuklia dhidi ya mataifa yenye silaha hizo za nyuklia pekee. Yaani nchi husika itatekeleza shambulizi la kinyuklia endapo itakuwa imeshambuliwa na taifa jingine kwa silaha hizo za nyuklia na wala haitazitumia dhidi ya taifa lisilo na silaha hizo.
Lakini, Je unazifahamu vizuri policies za kinyuklia katika mataifa mbalimbali hususani Israel?
Kuna kitu kinaitwa Samson Option ambacho kimejaribu kuainisha kuhusu matumizi ya silaha za nyuklia za Israel na wakati ambapo matumizi yake yatakuwa ni ya lazima dhidi ya nchi adui. Kipo kitabu chenye maelezo juu ya hiki ninachokisema; The Samson Option cha mwaka 1991.
Jambo jingine, unaposema kuwa;
vita ikitangwazwa ndio utajua Iran nuclear imetolea wapi
Kwamba vita ikitangazwa ndiyo nitajua Iran nuclear imetolea wapi? hiyo moja kwa moja ni kauli isiyokuwa supported na facts bali ni kama kauli ya kubashiri jambo (Guessing). Kwanini nisubiri vita itangazwe? Ni nini basi maana ya mjadala? Kwanini tusijikite katika taarifa na tafiti zenye kuakisi wakati uliopo ili kujengea hoja?
Unaweza kuwa na hoja nzuri lakini katika njia ya uwasilishaji wako ukaifanya ile hoja kwa namna moja ama nyingine kupoteza 'mashiko'.
Israel imetengeneza hizo kombora kujihami tu
Ni kweli kabisa na ninakubaliana na wewe kuwa, makombora hayo ni kwaajili ya kujihami.
IN FACT kila nchi yenye makombora ya nyuklia duniani ni kwaajili hiyo hiyo ya kujihami. Marekani, Urusi, China, Uingereza, Ufaransa n.k. wote hao makombora yao ni kwaajili ya kujihami yaani 'Deterrence'.
sio kwamba itashinda ikiingia vitani na India au China kisa ina 10000km range misiles.
Kabla ya kwenda moja kwa moja katika 'Ushindi' wa vita, kuna suala la makabiliano au mapambano katika vita husika baina ya pande mbili hizo.
Katika vita ya kinyuklia, Ili kuweza "kukabiliana" na mashambulizi ya kinyuklia dhidi ya taifa jingine ni lazima taifa husika liwe na uwezo wa kujibu shambulizi/mashambulizi na hapo ndipo ule mfumo wa Nuclear Triad unapofanya majukumu yake.
Kitendo cha nchi kuweza kuyajibu mashambulizi ya kinyuklia kwa silaha hizo hizo za nyuklia ndiyo njia moja wapo ya "kukabiliana" na mashambulizi ya nyuklia kwa maana ya kuweza kupeleka adhari kwa adui aliyekushambulia na kuleta adhari upande wako. Kwahiyo suala si kushinda, bado suala ni "Kukabiliana" kwanza.
Kombora wanalojivunia Israel ni Jericho 3 ambapo hata kwenye kumi bora ya makombora ya masafa halipo, Jericho 3 inaweza fika hadi 10000km ila kwa kupunguzwa uzito fulani(iwe chini ya payload yake ya kawaida ambapo ni 1000kg), lakini range yake kabisa ni kati ya 4500 mpaka 6500 ikiwa na payload ya 1000kg, kwa hio Jericho 3 Beijing haifiki mkuu.
Umetaja Jericho III.
Makombora ya Balistiki uhusisha factors nyingi wakati wa kufanyiwa deployment na kisha kusafirishwa kuelekea katika shabaha iliyokusudiwa. Moja ya factors hizo ni 'payload delivery'.
Uzito wa payload ni kitu kinachoathiri mwendo wa makombora haya ya Balistiki na ndiyo maana kimahesabu suala hilo huzingatiwa ili kupata kipimo sahihi cha uwezo wa kombora husika kusafiri na kufanikiwa kuumaliza mwendo wake (Range).
Kwahiyo kutokana na vyanzo mbalimbali kumekuwa na utofauti wa vipimo kulingana na hizo factors mbalimbali. Kuhusu Jericho III na kwa kuzingatia hicho nilichokisema vipo vyanzo vinavyoweka kiwango chake cha juu zaidi cha mwisho wa masafa kuwa ni kilometa 11,500 na vipo vyanzo ambavyo vimeweka chini ya hapo.
Kwahiyo kwa kuzingatia factors hizo, mass of payload, technologies kama warhead miniaturization, pamoja na modifications mbalimbali za hata pia makombora mengineyo kama Jericho II, Beijing is within range. Pia bila kusahau miji mingine mashuhuri kama Shanghai, Shenzhen, Guangzhou n.k. yaweza kuwa targeted.
Jericho 3 imefeli mara 3 nje ya 9 wakati wana launch
Sikatai kuhusu majaribio ya silaha kupata hitilafu ama ajali za hapa na pale kutokea katika sites za majaribio ya silaha maana matatizo haya huzikumba nchi zote zenye nguvu kijeshi katika nyakati tofauti tofauti.
ILA, hoja yako hii ina 'hang'. Kwamba Jericho 3 imefeli mara 3 nje ya 9? Lini? Kwa sababu zipi? Na ni kipi chanzo cha taarifa hiyo?
kila mmoja apige bomu la nuclear lenye radius ya 10km radius damage, Israel itapigwa bomu 80 tu inaishilia yote
Sawa! Lakini hapa umezungumza kiwepesi sana.
China ni kubwa sana kijiografia ukilinganisha na Israel lakini hilo halimaanishi kuwa Israel haiwezi kukabiliana na mashambulizi kutoka China. Silaha za nyuklia na facilities zake haziwekwi maeneo ya wazi kama uonavyo supermarkets, matawi ya benki n.k. Nuclear facilities pamoja na mifumo mingineyo inayoiwakilisha Nuclear Triad kwa ujumla wake ni highly classified na yenye miundombinu imara sana ya kuilinda dhidi ya mashambulizi ya kinyuklia.
Hivyo basi, bado kunaiwezesha nchi husika kufanya 'second strike' yaani kujibu mashambulizi hata kama asilimia kubwa ya taifa hilo litakuwa limeadhiriwa na mashambulizi ya adui.
Nimalizie kwa kusema kuwa; udogo ama ukubwa wa nchi kijiografia si kigezo cha msingi cha kuweza kukitumia kama advantage ya kuhimili mashambulizi ya kinyuklia, bali ni uwezo wa nchi husika wa kuweza kujibu mashambulizi endapo itakaposhambuliwa isitoshe main purpose ya silaha za nyuklia ni kupiga shabaha 'strategic' zitakazoleta adhari kubwa zaidi kwa mustakabali wa nchi lengwa.
Ahsante!