Marekani yaondoa baadhi ya masharti makali kwa Tanzania

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
My Take
Beberu ameufyata vibaraka watakuwa na Hali gani?

Beberu USA amelegeza Masharti kwenye mswaada wake wa kutathmini mahusiano yake na Tanzania Kwa sababu walizowahi zitaja.

Hii inakuja siku chache baada ya Rais Samia kufanya ziara Nchini Urusi iliyotikisa Duniani.

Ieleweke kwamba Tanzania ni Nchi ya Kimkakati wataruka na kukanyagana ila lazima waje.

Haya ndio matokeo ya Kishindo Cha Ziara ya Rais Samia Nchini Russia kilivyotokisa Kuta za Mabeberu Hadi wamelegea.
==============
Bunge la Marekani, limeondoa baadhi ya vipengele vilivyotoa masharti makali kuhusu uhusiano wa Taifa hilo na Tanzania, huku moja ya mabadiliko makubwa ikiwa ni kufutwa kwa pendekezo la kusitisha ushirikiano wa usalama na kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

Hatua hiyo imebainika katika marekebisho ya Muswada wa S.4577 unaohusu kutathmini upya uhusiano wa Marekani na Tanzania, unaotarajiwa kujadiliwa na Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti ya Marekani Juni 17, 2026.

Mabadiliko makubwa zaidi ni kuondolewa kwa pendekezo la kusitisha ushirikiano wa usalama na kijeshi kati ya Marekani na Tanzania. Rasimu ya kwanza ilitaka msaada wa kiusalama pamoja na fedha za maendeleo vizuiwe, lakini sasa kipengele hicho kimefutwa.

Mbali na kuondoa kipengele cha msaada wa kiusalama, toleo jipya la muswada huo, limeongeza mamlaka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, kuruhusu baadhi ya misaada au uwekezaji wa Marekani kuendelea Tanzania, iwapo hatua hiyo itaonekana kuwa na maslahi kwa taifa hilo.

Muswada huo pia umeongeza mamlaka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuruhusu baadhi ya misaada au uwekezaji kuendelea ikiwa itahitajika kwa maslahi ya taifa la Marekani.

Soma Pia: Rais Samia kufanya ziara nchini Urusi kuanzia Juni 3 hadi Juni 5, 2026

Iwapo utapitishwa na kamati, muswada huo bado utahitaji kupitishwa na Seneti nzima, Baraza la Wawakilishi na hatimaye kutiwa saini na Rais wa Marekani kabla ya kuwa sheria.

Source ITV
===

Mabadiliko yaliyofanyika ni kwenye kipengele cha 7 cha muswada huo ambapo awali ilipendekezwa kuweka zuio la misaada ya kijeshi kwa Tanzania
1781282598388.png

Ambapo kwenye maboresho ya muswada kipengele hicho kimeondolewa huku sehemu nyingine nyingi zikisalia kama ilivyokuwa awali
1781282690820.png
 
My Take
Mods (AI Mods)sibadilishe heading Ili wale vibaraka waisome namba.

Beberu USA amelegeza Masharti kwenye mswaada wake wa kutathmini mahusiano yake na Tanzania Kwa sababu walizowahi zitaja.

Hii inakuja siku chache baada ya Rais Samia kufanya ziara Nchini Urusi iliyotikisa Duniani.

Ieleweke kwamba Tanzania ni Nchi ya Kimkakati wataruka na kukanyagana ila lazima waje.

Haya ndio matokeo ya Kishindo Cha Ziara ya Rais Samia Nchini Russia kilivyotokisa Kuta za Mabeberu Hadi wamelegea.

View: https://www.instagram.com/p/DZcmzLhssbw/?igsh=c3dlN2kzbHZuMXVj

Kama ungekuwa unasoma na kuelewa ungegundua kwamba Marekani haina tatizo na Tanzania bali ina tatizo na mazafakas wa Serikali ya CCM, ambao (kama unavyoona) dawa yao inaendelea kuchemka jikoni.
 
Uwe na tatizo na Viongozi binafsi harafu useme unatathmini uhusiano mzima wa Nchi na Nchi kisa stori za upande mmja.
 
kuna vitu baadhi ya watu wanashindwa kuvielewa na kutofautisha, navyo ni regime ya tanzagiza vs nchi na wananchi, hivyo ni vitu viwili tofauti, USA hana tatizo na sisi au nchi yetu bali ana shida na regime ya tanzagiza, i.e regime inapita na itapita soon lkn nchi na wananchi wanabakia, kesho atakuja raisi mwingine na mambo yatarudia kama kawaida.

hiyo tofauti ni muhimu kuielewa kwenye haya mambo ...
 
My Take
Mods (AI Mods)sibadilishe heading Ili wale vibaraka waisome namba.

Beberu USA amelegeza Masharti kwenye mswaada wake wa kutathmini mahusiano yake na Tanzania Kwa sababu walizowahi zitaja.

Hii inakuja siku chache baada ya Rais Samia kufanya ziara Nchini Urusi iliyotikisa Duniani.

Ieleweke kwamba Tanzania ni Nchi ya Kimkakati wataruka na kukanyagana ila lazima waje.

Haya ndio matokeo ya Kishindo Cha Ziara ya Rais Samia Nchini Russia kilivyotokisa Kuta za Mabeberu Hadi wamelegea.

View: https://www.instagram.com/p/DZcmzLhssbw/?igsh=c3dlN2kzbHZuMXVj

Hey you, Shut up you!
 
Huna hoja unaitikia vichocheo vya mihemko
kwa akina siye,, "Mihemuko" belongs to our past, when we did not know the scriptures or the patterns that govern our lives.

The stage is yours..... keep on entertaining the gullible and feed them these delusions....
 
My Take
Mods (AI Mods) msibadilishe heading Ili wale vibaraka waisome namba.

Beberu USA amelegeza Masharti kwenye mswaada wake wa kutathmini mahusiano yake na Tanzania Kwa sababu walizowahi zitaja.

Hii inakuja siku chache baada ya Rais Samia kufanya ziara Nchini Urusi iliyotikisa Duniani.

Ieleweke kwamba Tanzania ni Nchi ya Kimkakati wataruka na kukanyagana ila lazima waje.

Haya ndio matokeo ya Kishindo Cha Ziara ya Rais Samia Nchini Russia kilivyotokisa Kuta za Mabeberu Hadi wamelegea.

View: https://www.instagram.com/p/DZcmzLhssbw/?igsh=c3dlN2kzbHZuMXVj

Tupe link tujionee wenyewe sio kutuletea link ya ITV.

Kwahiyo issue ya kujitegemea imekufa tena tuendelee kushirikiana na mabeberu.
 
Back
Top Bottom