My Take
Beberu ameufyata vibaraka watakuwa na Hali gani?
Beberu USA amelegeza Masharti kwenye mswaada wake wa kutathmini mahusiano yake na Tanzania Kwa sababu walizowahi zitaja.
Hii inakuja siku chache baada ya Rais Samia kufanya ziara Nchini Urusi iliyotikisa Duniani.
Ieleweke kwamba Tanzania ni Nchi ya Kimkakati wataruka na kukanyagana ila lazima waje.
Haya ndio matokeo ya Kishindo Cha Ziara ya Rais Samia Nchini Russia kilivyotokisa Kuta za Mabeberu Hadi wamelegea.
==============
Bunge la Marekani, limeondoa baadhi ya vipengele vilivyotoa masharti makali kuhusu uhusiano wa Taifa hilo na Tanzania, huku moja ya mabadiliko makubwa ikiwa ni kufutwa kwa pendekezo la kusitisha ushirikiano wa usalama na kijeshi kati ya nchi hizo mbili.
Hatua hiyo imebainika katika marekebisho ya Muswada wa S.4577 unaohusu kutathmini upya uhusiano wa Marekani na Tanzania, unaotarajiwa kujadiliwa na Kamati ya Mahusiano ya Nje ya Seneti ya Marekani Juni 17, 2026.
Mabadiliko makubwa zaidi ni kuondolewa kwa pendekezo la kusitisha ushirikiano wa usalama na kijeshi kati ya Marekani na Tanzania. Rasimu ya kwanza ilitaka msaada wa kiusalama pamoja na fedha za maendeleo vizuiwe, lakini sasa kipengele hicho kimefutwa.
Mbali na kuondoa kipengele cha msaada wa kiusalama, toleo jipya la muswada huo, limeongeza mamlaka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, kuruhusu baadhi ya misaada au uwekezaji wa Marekani kuendelea Tanzania, iwapo hatua hiyo itaonekana kuwa na maslahi kwa taifa hilo.
Muswada huo pia umeongeza mamlaka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuruhusu baadhi ya misaada au uwekezaji kuendelea ikiwa itahitajika kwa maslahi ya taifa la Marekani.
Soma Pia: Rais Samia kufanya ziara nchini Urusi kuanzia Juni 3 hadi Juni 5, 2026
Iwapo utapitishwa na kamati, muswada huo bado utahitaji kupitishwa na Seneti nzima, Baraza la Wawakilishi na hatimaye kutiwa saini na Rais wa Marekani kabla ya kuwa sheria.
Source ITV
===
Mabadiliko yaliyofanyika ni kwenye kipengele cha 7 cha muswada huo ambapo awali ilipendekezwa kuweka zuio la misaada ya kijeshi kwa Tanzania
Ambapo kwenye maboresho ya muswada kipengele hicho kimeondolewa huku sehemu nyingine nyingi zikisalia kama ilivyokuwa awali