Marekani yaondoa baadhi ya masharti makali kwa Tanzania

TATEPA
 
Moderators Active , Paw , Maxence Melo mbona hii habari haipo kwenye tovuti za Senate wala Congress wala DoS!!??
 
Haya matangopori ndo mnamlisha Bi Msumi anawalipa?
 
Chawa jinga hili yaani taarifa ya , senate source yake iwe ni ITV?

Nenda upitie vyanzo rasmi vya senate uone kama kuna kilichobadilika.

Buku 7 hazitowahi kusafisha damu za October 29.
 

..haina shida.

..jambo la msingi wanaohusika na ukandamizaji, na mauaji, na wasiotaka kuwajibika, wabanwe na mswaada huo.
 
Mods Kwa nini mumebadili heading?
 
Mliuwa watu ndugu,.jamaa na marafi zetu Kisha mka kama kwamba hawakuwa watz mara walihongwa. Mara tume na ujinga mwingine
Mlijua dunia itakuwa kimya
Kumbe,Kuna tume ya uchunguzi inaendelea
 
Uongouongo hausaidii kuondoa dhiki na dhihaka kwa nchi.Be sensible and grow up,chap!
 
Kumbe hukuelewa hata lengo la huo mswada!! Marekani haina tatizo na nchi ya Tanzania wala wananchi wake. Huo mswada lengo lake siyo kuiadhibu Tanzania au wananchi wa Tanzania. Mswada lengo lake ni kuwasaidia wananchi wa Tanzania wanaogandamizwa na kuonewa na watawala ili wapate haki zao.
Mswada huo wote lengo lake kuu ni kuwaadhibu watawala katili, siyo wananchi. Watawala gandamizi wakiondoka, au wakiachia madaraka, wakaja wanaowapaenda wananchi na kuwatendea haki, huo mswada wote unafutika, na ushirikiano na Marekani na Ulaya Magharibi utaongezeka. Mswada una lengo la kuwasaidia watanzania waheshimike na kuwa na haki ya maumuzi kwenye nchi yao.
 
Amelegea,wapi nimesema aufyate? Siko kwenye payroll yeyote Wala sipambani Kwa lolote badala yake napenda kuona Nchi hii haiingiliwi Wala kupangiwa na hao bwana zenu.
Mwananchi pekee mwenye uzalendo wa kweli kwa nchi hii, mwenye akili timamu, ni yule pekee ambaye anapenda nchi yetu iwe ni nchi yenye watawala wanaowaheshimu
wananchi, wanaoheshimu haki, uhuru na demokrasia., siyo watawala wanaoweka mifumo ya kuteka na kuua watu au kupora uchaguzi. Utakuwa ni mtu mwendawazimu kupindukia kama watu wanauawa, wanatekwa na kuporwa haki zao za kidemokrasia, likitokea taifa lolote likakemea vitendo hivyo viovu, halafu mtu anainuka na kusema kuwa mataifa hayo yanaingilia uhuru wa nchi. Yeyote mwenye akili timamu na anayejua sheria za kimataifa, anajua kuwa hakuna uhuru wa watawala kuua wananchi wao. Ulimwengu, kwa sheria za kimaitafa, una wajibu wa kuchukua hatua dhidi ya mtawala yeyote anayeteka au kuua wananchi. Hakuna uhuru wa kuteka na kuwaua wananchi.
Marekani, pamoja na madhaifu yake ya hapa na pale, lakini ni taifa mkombozi Duniani kwa wananchi wanaoonewa.
 
Kuwepo kwenye anga la watu hao ni hatari. Ni vyema wamarekani watusahau kwani kwa historia nchi yetu haichezi michezo ya kua kibaraka wao. Ukweli kama nchi nyingi tunaiogopa nchi hiyo yenye hila mbaya nyingi. Sisi tunataka kuheshimiwa uhuru wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…