Marekani yapaswa kujirekebisha kwanza katika suala la haki za binadamu

Marekani yapaswa kujirekebisha kwanza katika suala la haki za binadamu

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111390337181.jpg
Hivi karibuni Marekani ilitoa “Ripoti ya Haki za Kibinadamu katika Nchi mbalimbali Duniani”, na kulaani baadhi ya nchi kwa kutofanya vizuri katika kulinda haki za binadamu. Marekani hutoa ripoti kama hiyo kila mwaka. Lakini ukweli ni kwamba, utekelezaji wa haki za binadamu katika nchi moja unafahamika na wananchi wao wenyewe, na pia, Marekani ina haki gani kutoa matamshi kuhusu hali hiyo? Maana nchi hiyo yenyewe imefanya vibaya sana katika kulinda haki za binadamu.

Marekani inajidai kuwa ni “mwalimu wa haki za binadamu duniani”, lakini changamoto zake za ndani za haki za binadamu ni kubwa zaidi kuliko nchi nyingine duniani. Matatizo makubwa ya haki za binadamu yakiwemo ubaguzi wa rangi, mashambulizi ya bunduki, mshahara tofauti kati ya wanaume na wanawake, ajira haramu ya watoto na biashara haramu ya binadamu, yanazidi kuwa mbaya mwaka baada ya mwaka nchini Marekani, lakini serikali ya nchi hiyo haiyatilii maanani, bila kuchukua hatua yenye madhubuti kuyatatulia. Ikiwa nchi tajiri na yenye nguvu zaidi duniani, Marekani imekataa kujiunga na makubaliano sita kati ya makubaliano tisa muhimu zaidi ya kimataifa ya haki za biandamu. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, Marekani inakabiliwa na changamoto kubwa ya haki za binadamu. Kwa mfano, zaidi ya watu milioni 30 nchini Marekani hawana bima yoyote ya matibabu.

Unafiki wa Marekani katika suala la haki za binadamu unadhihirika zaidi katika nchi za nje. Marekani ndiyo nchi iliyoanzisha vita zaidi duniani. Kuanzia mwaka 1789 hadi 2022, Marekani ilianzisha mashambulizi 469 ya kijeshi nje ya nchi, na kuleta maafa makubwa ya kibinadamu duniani. Kwa mfano vita ya Afghanistan iliyoanzishwa na Marekani ilidumu kwa miaka 20, na kusababisha vifo vya zaidi ya raia 200,000, na zaidi ya watu milioni 10 kuwa wakimbizi.

Marekani pia ni nchi iliyoanzisha zaidi vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi nyingine duniani. Vikwazo hivyo pia vinaleta maafa ya kibinadamu mara kwa mara. Mwezi Februari mwaka huu, tetemeko kubwa la ardhi lilitokea nchini Syria, na kusababisha vifo na majeruhi ya watu wengi. Hata hivyo, Marekani ilikataa kuondoa vikwazo dhidi ya nchi hiyo, na kuzuia misaada ya dharura kupelekwa nchini humo. Afrika pia ni eneo lililoathirika sana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani.

Nchini Zimbabwe vikwazo vya Marekani vimeendelea kwa zaidi ya miaka 20, na kusababisha hasara ya moja kwa moja ya dola bilioni 40 za kimarekani. Vikwazo hivyo vimesababisha maisha magumu kwa Wazimbabwe. Hivi karibuni, Marekani pia ilikataa wito wa jumuiya ya kimataifa wa kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan na Sudan Kusini, bila kujali kwamba watu wa nchi hizo mbili wanakabiliwa na maafa yaliyosababishwa na migogoro pamoja na mabadiliko ya taibanchi.

Kama msemo unavyosema: “Unaponyooshea kidole chako watu wengine, vidole vingine vinne vinakuelekea wewe mwenyewe.” Kabla ya kukosoa nchi nyingine kuhusu suala la haki za binadamu, Marekani inapaswa kusahihisha kwanza makosa yake yenyewe katika suala hilo.
 
Waislamu waliwekwa Kwenye concentration camps Uyghur mnawatesa, kuwabaka na wengine mnawaua, mmeenda kuivuruga Tibet mmeua asili yao kwa kuwalazimisha waiabudu CCP na XI, vurugu Hong Kong na sasa mnataka kuivamia Taiwan.

Mnachunguza watu na kuchukua data za watu bila ridhaa zao kwa kutumia teknologjia mfano mlipandikiza vingamuzi jengo zima la African Union AU Mnatumia tiktok kuharibu vijana na jamii za nchi nyingine.

Wachina hamna uhuru wa kujieleza, na Kamwe haitakaa itokee utawala wa kikomunisti ukawa super power.
 
Maelezo Yako yanakusadifu kabisa...pole Kwa kuoshwa akili na west.ndo nachoweza kukwambia...una mengi ya kujifunza na kusimama Kwa kutumia ufahamu wako.
 
Maelezo Yako yanakusadifu kabisa...pole Kwa kuoshwa akili na west.ndo nachoweza kukwambia...una mengi ya kujifunza na kusimama Kwa kutumia ufahamu wako.
Usiniattack mimi toa point zitakazoweza kunipinga
 
Maelezo Yako yanakusadifu kabisa...pole Kwa kuoshwa akili na west.ndo nachoweza kukwambia...una mengi ya kujifunza na kusimama Kwa kutumia ufahamu wako.
Kuna msuguano kwenye south China sea, sasahivi mna migogoro na majirani zenu Philippines, Vietnam, Burnham, Malaysia n.k China inawafukuza watu kwenye maeneo yao yaani sovereignty area. Mna tamaa sana mnapora kila kitu.

Mmezivamia nchi za Africa hamjali kuhusu Mazingira mnafanya uharibifu mkubwa sana wa kimazingira

Na project yenu ya Road and Belt Initiative hamjali kuhusu next generation mnakata miti hovyo, mpango wenu wa Dept trap diplomacy umeziingiza nchi nyingi sana kwenye madeni na mnapora Mali za nchi hizo mfano srilanka na Djibouti pia Uganda na sasa mna mpango huo Kenya. Mnadhalilisha waAfrica huko Malawi na Zambia mnazivamia nchi mnaziharibu na ku establish utawala wenu. Wa west walikuwa hawaendi kwa style zenu nyinyi Africa na waafrica walisha wakataa na swala la muda tu. Angalia mfano MAANDAMANO huko Kenya na south Africa ya kuwakataa.

There is no way ukomunisti utaweza kutawala Dunia. Dunia inatakiwa iwe mahali pa Usawa uwazi na upendo na kushirikiana sio uwanja wa vita. Democracy is the best option njia ya AMANI duniani
 
Maelezo Yako yanakusadifu kabisa...pole Kwa kuoshwa akili na west.ndo nachoweza kukwambia...una mengi ya kujifunza na kusimama Kwa kutumia ufahamu wako.
Hakuna nilichokaririshwa ukweli upo wazi, Uyghur kwenye jimbo la Xinjiang ni swala lililowazi Waislamu Dunia nzima wanawaangalia tu. Soon mtaamza kufukuzwa Kwenye nchi za kiislam, wachina waliowekeza Afghanistan wameshaanza kufukuzwa kwasababu hiyo ya kuwatesa wailsamu wenzao.

Mnauda dini za watu, asili za watu mnanyima uhuru mfano wananchi wa Tibet

Sasaivi mmewekewa vikwazo vya kiuchumi. Jana tu C.E.O wa tiktok iliwekwa kikao kwenye baraza la Congress la USA Alibanwa kwa tuhuma za chama cha CCP kuiba taarifa za watu kupitia tiktok
CCP ilibadilisha katiba na kuzitaka kampuni kushirikiana kutoa intelligence information kwa SERIKALI na ccp. Wachina Hamfai hamtufai na hamuifai kuitawala Dunia
 
Pole
 
Back
Top Bottom