Marekani yashambuliwa na Jeshi la Wanamaji la Iran ambalo inadaiwa liliangamizwa


 
Watu wanapigania uchumi wao sisi tunapigania dini zao. Aliyetuloga alikufa mdomo wazi
Yeyote anayeingiza huu mgogoro kwenye masuala ya udini , ujue uwezo wake wa kuchakata mambo, kutathmini na kutafakari upo chini.

Huu mgogoro una athari kwa dunia yote ndio maana watu wanafuatilia, mtu ukishaisifu Iran unaonekana wewe ni muislamu, anakuja wa dini nyingine na kuchukua mjadala kuupeleka kidini. Wakati hii vita haihusiani na dini.

Kwa akili za kawaida tu US na Israel wanachofanya si sawa, na ili uelewe si sawa lazima kwanza uwe na sifa tajwa hapo kinyume na hao wanaoingiza hili suala kidini, kwanza uwe na uwezo mkubwa kuchakata mambo, kutahmini mambo kwa undani na uwezo mkubwa wa kujitafakari.

Ndio maana watu wanao iponda US ukiwafuatilia ni watu waliofuatilia vitu, wanajua mambo mengi na historia , wana facts.

Ukishakuwa na hizo sifa hutoona tena haya ni masuala ya kidini, lakini kama hizo sifa hazipo ndipo unakuwa wale wale wa 'Israel ni taifa teule' , 'Iran ni magaidi' , 'Hezbollah ni kikundi cha kigaidi' , 'Iran ipigwe ichakae' ukifuatilia wengi wanaotoa hizo kauli utakuta wana sifa zinafanana ama tabia (Collective Behavior) ama fikra kundi(groupthink).

kwanza hawajui mengi kuhusu historia, uwezo mdogo wa kiakili na kuchanganua mambo kwa kifupi hawajielewi, hata uchambuzi wao utagundua hawajui wanacho kizungumza. Haijalishi umri, umri , jinsia , muonekano ama cheo.

Ni kama lile toto la Museveni nadhani mkuu wa majeshi, jamaa ni lipumbavu hadi aibu. Nawasikitikia wana Uganda.
 
Kwa muktadha huo huo uliodadavua kuna wengine wana support Iran kwa sababu ni dola ya kiislamu...

Watu wanaochambua hii vita kwa sababu ya uislamu au ukristo au uyahudi ni makanjanja wa mwendo wa SGR....

Hii vita ni uchumi na control ya midle east inapiganiwa. Kuna wanaotamani iendelee ili wapate faida zaidi na kuna wanaotamani iishe ili maisha yapate haueni.

Marekani anapigania pertodollar yake Iran anapigania uhuru wake....

Kanjanja anapigania uislam au ukristo wake.
 
To understand this, you first need to have an open mind...

Lazima uwe na fikra huru, na akili yako uiweke huru.

Maana wengi wanaamini West na US ndiko kuna teknolojia pekee za hali ya juu.
 
Nakubaliana na wewe, huu mgogoro kuuweka kidini katika pande zote, huyo mtu achunguzwe akili yake.
 
Iran ina jam GPS hapo na nilisoma, kuna baadhi ya meli captain wanaona wapo nchi kavu, huku meli nyingine zikionekana zipo airport.

HawaIran kwa kweli hii tabia ya kuipeleka vessel airport haikubaliki.

Lakini inasaidia kujilinda dhidi ya drones na missiles ambazo ni gps guided, na pia ku confuse military vessels na meli zingine za mizigo.

Kwa chinese na beidou yao inasemekana military grade beidou ni ngumu sana kuifanyia jamming, japo sio kwamba itashindikana kabisa kuwa jammed. Hivyo Iran inatumia GLONASS na BeiDou.
 
MADUNYA nazani ni wingi wa "DUNYA" lakini MABAZAZI ni wingi wa "BAZAZI" kama Niko sawa, swali:, je DUNYA na BAZAZI ni mtu wa aina gani mkuu?, mana tusije tukamuita Dunya au Bazazi mubashara tukala mkong'oto uku mtaani.
 
Upo sahiii kwa %100 tukikumbuka kile kisa cha ile Vessel yenye askari w Marekani walikiri kupoteza mawasiliano kabisa walipoingia tu maji ya Iranian
Ikabidi wa surrender Wote.

Kuachiwa kwao ikawabidi Waziri wao !!
mambo ya nje afike mwenyewe Iranian kuchutamaa wkt wa Obama!!!!!!
 

Attachments

  • 4cbtb4c4260e742omgh_440C247.jpg
    28.8 KB · Views: 19
  • download-1.jpeg
    8.3 KB · Views: 16
Sasa wewe ndio unafanya nini, una copy ujinga unakuja ku paste huku, yaani wewe vyanzo vyako ndio vya kweli, algorithm siku zote inakuletea kile unataka kukisikia hata kama cha uongo.
 
Marekani ikazishambulia boats za Iran, 3 zilizamishwa moja kwa moja, baadhi ya askari wa Iran ndani ya boats hizo walikufa, Iran imethibitisha.
Huu uongo mkubwa.
Iran imekanusha boats zake 6 kuzamishwa.
Marekani imekanusha manowari zake kushambuliwa.
Aljazeera, RT na vyombo vingine vya habari vikubwa vimetoa taarifa hizo za kukanusha toka pande zote mbili.
 
Umemaliza Kila kitu hapa
Mi kinachoniumiza ni kuona mkristo tena msomi,eti kwa kua tu muislam mbumbumbu anaitetea Iran,basi yeye anaitetea Israel, na U.S πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜,Ili tu aonekane mshindi,.......wakati huo huo anawaponda wakoloni na wazungu kwa kuwatawala waafrika huku akishangilia Iran kutaka kutawaliwaπŸ˜…πŸ€£πŸ€£
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…