Marekani yasikitishwa na Zelensky kukataa Dili la madini kuijenga upya UKRAINE

Acha uwongo,ndovu kiasi gani wanaweza fidia gharama za reli ya tazara?
 
Sharti zito mno. Waru wapewe hati miliki ya madini halafu wewe wakujengee nyumba...!!! Ni bora zele atafute wachimba madini kisha fedha zitumike kujenga hizo nyumba na ukraine mpya
Haaaaa...huku kwetu wanachukua bila kutujengea chochote.
 
Angekuwa mtu fulani angesha saini huo mkataba mapema asubuhi😃
 
Ulidhani silaha nzitonzito alizokua akipeleka Joe Biden nilikua ni nini kama sio mahari?
Kabisa mkuu,hawa jamaa hawatoi kitu bure,,halafu viongozi wetu sijui kwanini huwa wanadanganya ati msaada!!!,,nakumbuka hata issue ya chanjo ya korona,haikuwa bure kama tulivokuwa tukiambiwa,,tena nchi zetu zilikuwa zinalazimishwa.
 
Ipo wazi... Ona sasa wakubwa wamekaa mezani huku Ukraine ikiwa ndio kifungua kinywa
EU sio Afrika elewa hilo , EU wanajua kumruhusu Putin aiteke Ukraine kesho itamfanya atamani kusogea ndan zaid ya Ulaya , EU haitakubali kbs
 
Huyu zele aungane na urusi aachane na NATO uswahili ni mwingi huko
 
Mwisho wa siku watakubali Tu.... Ukraine hawana tena uwezo wa kukataa masharti ya USA, tusubiri muda utakuja kuongea
 
Trump bwana, angesema tu hataki kuwasaidia hao Ukraine,sasa ndio sharti gani hilo amewapa!
Alijua watagoma tu ili baadae asilaumiwe.
Nionavyo mimi Ukoloni unarudi kwa mlango wa nyuma, na hasa kwa kutumia misaada. Unapewa misaada ya bure kabisa , hulipii chochote lakini unapewa masharti ambayo ukiyafuata, utahatarisha Uhuru wako. Fikiria unajengewa majumba na miundombinu yote iliyoharibiwa kwa sharti la kuachia madini yako yote kwa huyo anayekupa Msaada! Aliyasema Mwalimu, kutegemea mikopo na misaada hatima yake tutaupoteza Uhuru wetu.
 
Ni sawa na mimi nikuambie, nitakujengea nyumba, kusomesha watoto wako, kwa sharti la kunipa mkeo niishi naye; je ungeweza?

Vinginevyo, wakubaliane iwe ndani ya miaka isiyozidi 5 katika umiliki.​
Hiyo offer bado unakuwa ni Hobson's choice! Ukimwachia umiliki kwa miaka mitano, uwe na hakika utaishia kubaki na mashimo matupu! Atahakikisha anayachimba 24/7, hakuna kulala. Kwa teknolojia aliyonayo mwisho wa miaka mitano huna kitu.
 
Wamarekani hawashindwi hili
Hiyo offer bado unakuwa ni Hobson's choice! Ukimwachia umiliki kwa miaka mitano, uwe na hakika utaishia kubaki na mashimo matupu! Atahakikisha anayachimba 24/7, hakuna kulala. Kwa teknolojia aliyonayo mwisho wa miaka mitano huna kitu.
 
Hilo dili angepewa cheshekedi wa congo,

Ajengewe apartments kwenye misitu yote.

Awe anapewa na ruzuku kila mwaka.

Us aweke na military base kabisa pale kivu.

Hili dili hachomoi kwa hali ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…