#COVID19 Marekani yatoa msaada wa dozi Milioni 1 za Chanjo ya Coronavirus

#COVID19 Marekani yatoa msaada wa dozi Milioni 1 za Chanjo ya Coronavirus

Mkuu umegonga nondo za kutosha.
Cicero alisema - "The wise are instructed by reason ,average minds by experience, the stupid by neccesity and the brute by instinct"

Sijui tutakuwa wapi katika Hayo makundi manne
 
Taarifa kama hizi ndo zinavunja moyo na ushabiki kwa viongozi wetu. Tumeona Chanjo imeshuka kwa maringo, wapokeaji wakivalia barakoa. NImeoneshwa kwamba tumeletewa Johnson & Johnson. Ndo nini sasa?

Hii ni chanjo iliyotiliwa mashaka siku nyingi na nchi nyingi kwa tatizo la damu kuganda. Yaani sisi ndo tumeletewa hivo! Tuleteeni aina zote ili sisi tuchague kitanzi. Wanaotuletea, kwao wanachagua iweje sisi?
 
Uwezo wetu ni kupima mapapai,tutaweza kujua hiyo chanjo kama feki au si feki
 
Wahenga walisema, "Mambo ya kusikisikia, mbweha akapata mimba ya watoto mapacha".
Taarifa kama hizi ndo zinavunja moyo na ushabiki kwa viongozi wetu. Tumeona Chanjo imeshuka kwa maringo, wapokeaji wakivalia barakoa. NImeoneshwa kwamba tumeletewa Johnson & Johnson. Ndo nini sasa?

Hii ni chanjo iliyotuliwa mashaka siku nyingi na nchi nyingi kwa tatizo la damu kuganda. Yaani sisi ndo tumelewa hivo! Tuleteeni ain zote ili sisi tuchague kitanzi. Wanaotuletea, kwao wanachagua iweje sisi?
 
Lakini chanjo si ni hiari? Asiyetaka kuchanjwa na asichanjwe tu.
Kinachofanyika ni sawa na mtu mwenye allergy ya karanga halafu unaletewa chakula pekee chenye karanga wakati una njaa na kuambiwa unaweza kula kama unataka au usile!

Ndicho ambacho serikali inafanya kwa sasa!
 
Huyo mtu hana uwezo wa kutafuta chakula kingine?
 
Marekani imeipatia Serikali ya #Tanzania zaidi ya dozi milioni 1 za chanjo dhidi ya COVID-19, ukiwa ni msaada kupitia mpango wa usambazaji chanjo wa #COVAX kwa uratibu wa Umoja wa Afrika

Upokeaji wa Chanjo hizo umefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ukiongozwa na Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima.

Chanjo ya Johnson and Johnson iliyopingwa Marekani na Ulaya kwa damu kuganda tumeletewa Tanzania. Tuchomwe tu maana damu zetu sisi weusi haina mfumo wa kuganda. Hata tukifa poa tu kwani nini
 
Huyo mtu hana uwezo wa kutafuta chakula kingine?
Unampikia mwanao chakula hicho halafu unamwambia kama hataki atafute chakula kingine wakati hana uwezo wa kutafuta chakula kingine!

Kwa nini usipike vyakula mbali mbali halafu umwambie achague anachopenda!

Nchi ambazo hiyo chanjo inatoka wananchi wake wamepikiwa vyakula mbali mbali(chanjo) na kuambiwa wachague wanachokipenda!
 
Unalinganisha vitu ambavyo havilinganishiki!

Kwanza, chanjo si chakula. Chakula ni kitu essential kwa uhai.

Hivyo, chanjo ya Corona si essential kwa uhai. Unaweza usichanjwe na usife.

Huwezi kuishi bila chakula!

Linganisha vinavyolinganishika.
 
Habari za jioni wakuu,
Serikali leo imepokea awamu ya kwanza ya chanjo ya kupambana na ugonjwa wa corona iliyowasili leo mchana.
Chanjo hiyo imewasili na kupokelewa na Waziri wa afya ndugu,Dkt Dorothy Gwajima.
Chanjo hiyo imewasili na ndege ya shirika la ndege la Emirates na kupokelewa mchana huu.
Jikinge, wakinge na wengine .
Corona inazuilika.View attachment 1866489View attachment 1866490
View attachment 1866495
Chanjo zilizokosa wateja huko mbele ndio zinaletwa huku..
Gwajima aendeleze libeneke. Wachanjane wao kwa wao sie hatutaki...
 
Marekani imeipatia Serikali ya #Tanzania zaidi ya dozi milioni 1 za chanjo dhidi ya COVID-19, ukiwa ni msaada kupitia mpango wa usambazaji chanjo wa #COVAX kwa uratibu wa Umoja wa Afrika

Upokeaji wa Chanjo hizo umefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ukiongozwa na Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima.

Kuna yeyote yule anaejua ni aina gani (type) ya chanjo ambayo Tanzania wamekubali kuipokoea kutoka US of A?
 
Unalinganisha vitu ambavyo havilinganishiki!

Kwanza, chanjo si chakula. Chakula ni kitu essential kwa uhai.

Hivyo, chanjo ya Corona si essential kwa uhai. Unaweza usichanjwe na usife.

Huwezi kuishi bila chakula!

Linganisha vinavyolinganishika.
Ninalinganisha kama chakula kwa sababu kuna mataifa yanasema kama hujachanjwa huwezi kuingia katika nchi zao.

Kuna watu wanachanjwa sio kwa sababu ya kuogopa ugonjwa bali kwa sababu ya kutimiza masharti fulani ambayo yanawataka kwa lazima.

Kuna watu wanatakiwa kwenye kuhiji na wasipochanjwa hawawezi kuruhusiwa kwenda kuhiji. Hawa kuna baadhi sio kwamba wanachanjwa ili kujihami na korona bali kwa sababu ya kutimiza sharti.

Chanjo inayopatikana nchini ni moja tu na wakiikataa hawawezi kwenda kuhiji.

Kwa mantiki hii ndio maana hoja ya chakula nimeweka kama mfano muhimu.
 
Back
Top Bottom