Serikali ya Marekani kupitia Taasisi ya Centre for Desease Control ama CDC imetoa onyo kwa raia wa Marekani kuchukua tahadhari ya kutembelea Tanzania kwani kuna uwezekano mkubwa wa kuambukizwa corona.
CDC imesisitiza kua watu waepuke kwa gharama zozote kutembelea Tanzania na kama ikitokea ulazima basi wasiache kufuata masharti yote ya kupambana na corona yaliyowekwa na CDC.
Nota Bene.
TusiTusisahau kua Marekani inaongoza kwa kuleta watalii nchini ikifuatiwa na Uingereza na nchi nyingine za Ulaya. Kwa Afrika Kenya ndio inaongoza kuleta watalii Tanzania.
Hii ina madhara makubwa kwa uchumi wetu.