Marekani yawaonya raia wake kutembelea Tanzania kuepuka kuambukizwa COVID-19

We una corona au hauna? Na je upo karantini au haupo? Unavaa barakoa au huvai? Unatumia Sanitizer au hutumii? Maeneo unayotembelea yana msongamano au hayana? Hebu tupe majibu ya haya maswali kwanza
 
Dawa tunayo kitambo sana, US msiogope
Your browser is not able to display this video.
 
Kuna hospital kama Hindumandal wako careless sana. Wahudumu na Drs hawavai Barakoa hata wagonjwa ni free movement tu.
 
Nchi tumeikabidhi kwa washamba, kila kitu kinajibiwa kwa majibu mepesi, imekuwa kama Tanzania inajitosheleza haiitaji uhusiano na nchi nyingine
 
Tukikaza tusife kwa korona tutakufa njaa!!! Kuchagua ni kupanga
 
Hivi ni vita vya kiuchumi je tufukuze mabeberu/
Corona ipo Duniani kote Ndege zinakuja wageni wanakuja kinachowafanya Serikali kuongopa kuhimiza unawaji mikono kupaka vitakasa mikono ni nni? au Serikali inataka watu wafe kwa wingi ili wapate pesa za misaada kuzuia corona?
Covid 19 IPO anaebisha nitamtumia dozi ninayo itumia saizi afu nimejitenga Niko lodge yapata wiki sasa kuepusha mambukizi ktk familia
Corona ipo ingawa hofu ya kusema imetawala ndiyo maana Serikali wanaona wamese haipo
 
Inchi tumeikabizi kwa washamba, kila kitu kinajibiwa kwa majibu mepesi, imekuwa kama Tanzania inajitosheleza haiitaji uhusiano na inchi nyingine
Tatizo la Serikali hii ni kujaa washauri wa hovyo hata vya tahadhari hawataki, hebu fikiria kila siku kuna Ndege toka mataifa mbalimbali lakini Serikali hawataki kuhimiza hata kunawa mikono tu unategemea nini hapo? Siku Serikali wasikie corona ipo CHADEMA au ipo ACT utawasikia waanza kampeni ya kunawa mikono kupata vitakasa mikono na kuvaa barakoa
 
Hapa Nina Mary a toka juzi. Wiki iliyopita nilipata tendinitis nikipiga kwa salt gagling unaondoka. Sasa Mafua yanachuruzika vibaya sana. Sikohoi. Ila napiga mchemsho wa mchaichai, tangawizi, jani ombo la kichaga, kitunguu swaumu na ndimu. Nakunywa ya moto. Mazoezi ya mapafu kuvuta pumzi. Ninaamini siyo Corona Ile anything to do with Mafua a n.k sifanyi ajizi.
 
Yaani hapo Marekani washafeli...
Naipenda nchi yangu Tanzania.
Kuipenda Nchi ni kujikinga kunawa mikono kujipaka vitakasa mikono ikibidi vaa barakoa siyo kupiga chafya kwenda chooni bila kunawa mikono kisha unawaambukiza watu UTI mafua na magonjwa mengine, hakuna Nchi inapendwa kwa kuambukizana magonjwa kizembe zembe
 
Propaganda! Adui muombee njaa.
Corona mbona hatuijui Tanzania
 
Ndiyo, ila kwangu cha muhimu kwanza ni kuiombea nchi yangu Tanzania.
 
Waache kuhangaika dawa ya kutibu huu ugonjwa haijapatikana ko kila taifa linapambana na ugonjwa huu kwa njia linazozijua na sisi hatuziamini njia wanazozitumia kupambana na corona wa tz wawe na tahadhhari waendapo huko
 
Hata sitaki kuamini wale wanaofurahia hili tangazo! Kweli ndio hawa hawa wanatumia barabara, umeme, huduma za afya, maji, ndege, miundombinu na huduma zote chini ya JPM???!!!
 
Wasi wasi wangu ni kwamba hawa jamaa wanaweza wakatuletea virus hata kwenye bidhaa mbali mbali ili kutukomoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…