Uchaguzi 2020 Marekani yawasihi NEC na Magufuli kujali misingi ya demokrasia kwenye Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Marekani yawasihi NEC na Magufuli kujali misingi ya demokrasia kwenye Uchaguzi Mkuu 2020

Kamati ya bunge la Marekani la seneti ya mambo ya nje imeisihi tume ya uchaguzi Tanzania kujirekebisha, kuondoa makosa yaliyofanyika ndani ya miaka 5 iliyopita, kuacha kumshitaki Lissu kwa hoja ya kijinga.

Kamati hiyo inamtuhumu Magufuli kuminya Demokrasia, utawala bora, uhuru wa kujieleza toka ameingia madarakani miaka 5 iliyopita, wamemsihi kuwa sasa ni wakati wa kurekebisha makosa aliyoyafanya kwa miaka 5 iliyopita.

======

OCTOBER 05, 2020

CHAIRMAN RISCH: TANZANIA OFFICIALS MUST CORRECT PAST ERRORS AND HOLD CREDIBLE VOTE

BOISE, Idaho – U.S. Senator Jim Risch, chairman of the Senate Foreign Relations Committee, today issued the following statement regarding the recent suspension of the leading Tanzanian opposition candidate's campaign by electoral officials:

“Suspending the leading opposition candidate's presidential campaign on bogus charges raises serious questions about the independence of Tanzania's electoral commission. The political violence and repression of opposition candidates, restrictions on independent media, lack of autonomy and transparency by electoral officials, and government authorities' interference reflect Tanzania's history of flawed elections and the country's democratic erosion over the past five years.

“Despite profoundly troubling developments throughout the electoral campaigns, Tanzania's October 28 general elections provide an opportunity for President Magufuli and electoral officials to correct past errors and return Tanzania to a positive democratic trajectory by holding free, fair, and credible elections. Otherwise, Tanzania's continued democratic decline stands to undermine its future and will negatively influence democratic progress in the rest of the region.”

Background: On Friday, Tanzania's National Electoral Commission (NEC) suspended leading opposition presidential candidate Tundu Lissu from campaigning for seven days for violating the electoral code of ethics. The NEC accused Mr. Lissu of making seditious comments during one of his rallies in complaints filed by two political parties, including the ruling Chama Cha Mapinduzi party. NEC membership is selected solely by the president of Tanzania.

Chanzo:Chairman Risch: Tanzania Officials Must Correct Past Errors and Hold Credible Vote | United States Senate Committee on Foreign Relations
Mungu wabariki Wazungu
 
Hivi wale wamarekani weusi wanavyouawanl na mapolisi wao kwa ubaguzi huwa wanatoa matamko gani?
Wasijifanye wanajua demokrasia wakati kwao kuna madudu hawayasemi.

1. Watu waliandamana bila kuzuiwa

2. Vyombo vya habari vililaani bila kufungiwa

3. Baadhi ya wakuu wa polisi walijiuzulu

4. Wahusika walifunguliwa mashitaka
 
1. Watu waliandamana bila kuzuiwa

2. Vyombo vya habari vililaani bila kufungiwa

3. Baadhi ya wakuu wa polisi walijiuzulu

4. Wahusika walifunguliwa mashitaka
Hayo mauaji yalikoma, mbona yaliendelea au hufatilii vizuri mambo ya nje ya nchi.
 
Hakika hii mishale inayopigwa kila upande toka pande mbalimbali za dunia, zikituonya nchi hii tuendeshe uchaguzi ulio huru na wa haki, ni message tosha kwa watawala kuwa wasitende kama walivyozoea, ni lazima watambue kuwa dunia nzima inauangalia kwa makini sana, uchaguzi huu

Iwapo Rais wetu na NEC yake watajifanya wana kiburi na kutotaka kusikiliza hizo kelele za dunia nzima, basi watakapoburuzwa kwenye mahakama ya kimataifa The Hague, wasije wakalaumu mtu!

Hakika uchaguzi wa mwaka huu ni wa historia, kama ambavyo amekuwa akisikika akisema Tundu Lissu.
Niliota leo nikaona nyambizi tatu ufukweni bara hindi. Zikiwa na ndege za kijeshi. Ndoto zangu huwaga kweli lakini
 
Hakika hii mishale inayopigwa kila upande toka pande mbalimbali za dunia, zikituonya nchi hii tuendeshe uchaguzi ulio huru na wa haki, ni message tosha kwa watawala kuwa wasitende kama walivyozoea, ni lazima watambue kuwa dunia nzima inauangalia kwa makini sana, uchaguzi huu

Iwapo Rais wetu na NEC yake watajifanya wana kiburi na kutotaka kusikiliza hizo kelele za dunia nzima, basi watakapoburuzwa kwenye mahakama ya kimataifa The Hague, wasije wakalaumu mtu!

Hakika uchaguzi wa mwaka huu ni wa historia, kama ambavyo amekuwa akisikika akisema Tundu Lissu.
Marekani yenyewe uchaguzi hovyo na unalalamikiwa na Rais wao ajabu sana
 
Hayo mauaji yalikoma, mbona yaliendelea au hufatilii vizuri mambo ya nje ya nchi.

Uhalifu upo kila kona ya dunia lakini cha msingi ni kuwa na vyombo vya kuwashughulikia wahalifu, uhuru wa watu kuelezea hisia zao n.k. na vitu hivyo wao wanavyo. Hivi uchunguzi wa yule mwanasiasa aliyepigwa risasi 16 umeishia wapi?
 
Kwanza, kuhusu ulalamikaji wa Donald Trump kuhusu upigaji wa kura kwa njia ya posta ni maoni yake binafsi. Inawezekana anatafuta kisingizio kwani kwenye polls yuko nyuma zaidi ya points 10. Utaratibu huo umekuwepo kwa miaka mingi bila ya kulalamikiwa.

Pili, kuhusu Trump kwamba anaweza kukataa kuachia ofisi ni jambo la kupuuza. Ki historia jambo hilo halijawahi kutokea kwenye taifa hilo. Halafu hata ikitokea kwamba atakataa kuachia ofisi bado taifa hilo lina vyombo huru vya kumshughulikia mgombea huyo.

Napenda kumalizia kwa kusema kwamba hata kama kukitokea kasoro za hapa na pale kwenye uchaguzi wa Marekani lakini bado wataweza kuzitatua kwasababu wana vyombo madhubuti na huru. Vyombo madhubuti na huru vya kutatua mambo yao ndio tofauti kubwa kati yao na nchi isiyo ya kidemokrasia.
Ni maoni yake kama ilivyo maoni binafsi ya mgombea wa Chadema anayedhani kuna mpango wa kumuibia kura kura
 
Njia pekee ni kifo cha jiwe ndio tutapona kama taifa!!watu wa system mko wapi?PIGA SHOTI PACEMAKER JIWE LIPASUKE!AMANI IRUDI TUTEUE MWINGINE WA KUTUVUSHA!!
 
Ni maoni yake kama ilivyo maoni binafsi ya mgombea wa Chadema anayedhani kuna mpango wa kumuibia kura kura

Tofauti ni kwamba kule Marekani utaratibu wao ni wakuaminika kwa miaka mingi na wa hapa hauaminiki. Kwahiyo huwezi kumlaumu Lissu akiwa na mashaka. Msimamizi anachaguliwa na rais na rais amesema hawezi kumlipa mtu na kumpa gari kisha akamtangaza mpinzani.
 
Utaratibu wa Marekani bi wa kuaminika na nani?

Uchaguzi wa 2016 Marekani unalalamikiwa kuingiliwa na serikali ya Urusi.
Watanzania wana imani na tume yao ya uchaguzi NEC.
 
Kunakaribia kukucha.

Jiwe katuharibia sana hii nchi, Tatizo watanzania wengi si waelewa.

Hii ni Dalili kuwa utawala wa Jiwe unapingwa kila kona Watanzania wengi hatumpendi Magufuli, Wazungu hawampendi Magufuli, watetezi wa haki za binadamu hawampendi Magufuli, mashirika ya umoja wa mataifa na msaada hayampendi Magufuli.

Kwaheli Magufuli, kwaheri CCM, kwaheri ukoloni, Kwaheri umasikini.
Sijui sisi watanzania tulikua wapi kudai tume HURU ya Uchaguzi , majirani zetu Kenya wanashangaa, mgombea ndiye anayeteua wajumbe, wakurugenzi na makamishna wa tume kweli tutegemee mkurugenzi atamwangusha aliyempa ugali?? Tuamke tuamke
 
Utaratibu wa Marekani bi wa kuaminika na nani?

Uchaguzi wa 2016 Marekani unalalamikiwa kuingiliwa na serikali ya Urusi.
Watanzania wana imani na tume yao ya uchaguzi NEC.

"...kuingiliwa na serikali ya Urusi" bado haimaanishi kwamba haukuwa huru. Hata hapa Tanzania Warusi wanaweza kuingia kwenye kompyuta za CCM na NEC bila sisi kujua.
 
Uchaguzi wa Marekani unaotarajiwa kufanyika November mwaka huu umeingia kasoro nyingi kiasi kwamba Rais Trump amekataa kutoa ahadi ya kukubali matokeo yatakayotangazwa na tume.

Trump amesema kuwa utaratibu wa kupiga kura umepangwa kwa mtindo unaolenga kukandamiza wapiga kura wanaomuunga mkono.

Vilevile kumekuwa na hours kuwa matokeo ya uchaguzi huo yatachelewa kutolewa kwa sababu uhesabuji kura katika baadhi ya majimbo utaendelea kwa siku 4 baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa.
MAREKANI, kuna tume huru mpaka zaidi ya uhuru,Rais wa nchi haigusi wala serikari haiwezi kuingilia tume,ndio maana hata yeye unamuona analalamika huenda wamedhibiti magumashi yake ya uchaguzi uliopita.
 
Nilisha sema sitakuwa pamoja, eti tukomae /tuwe wazalendo tukitekeleza vikwazo kwa uchu wa madaraka, hapa tu naishi kama nipo kwenye vikwazo, halafu eti viongezeke sababu siasa!
 
Wanamuomba JPM atakaporudi tena madarakani arekebishe.
Wanatakiwa wajue ya kwamba baada ya uchaguzi ni marufuku siasa mpaka uchaguzi ujao.
Spana,, spana tu mpaka mwisho.
 
Ninyi CCM hamna ubavu wa kuwabishia hao Marekani kwa watakayoyasema............

Kwani misaada yao mnaendelea kupokea kwa wingi hao mnaowaita mabeberu
Usisahau pia Wao wanafaidika na mengi kutoka kwetu! Usipende kujizarau sana,hata Tajiri kuna kitu huwa anataka kutoka kwa masikini, ndiyo maana anamzuga na vizawadi vidogovidogo anavyoviita Msaada!!
 
Back
Top Bottom