Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

America watu wanauwawa kuliko nchi yoyote east Africa halafu leo wanaleta kidomodomo.
Naona Tanzania,Kenya na Uganda zimewekwa level moja,halafu eti Rwanda hakuna hatari yoyote.
Mwenye akili ataona shida ilipo.
 
Hawa Jamaa wananusa Mbali, wameisha nusa Mbali! Ngoja tuendelee Kusubiria!

Jamaa anawatahadhalisha raia wake lakini cha ajabu sie tunaanza kulaani badala ya kuwa makini na onyo hilo na kulifanyia kazi?, hivi mtu akisema nyumbani kwenu kumeingia mdudu basi ni kweli anakuwa hakupendi? endapo hapo baadae tendo ovu likatendeka nani alaumiwe?
 
Unasema kweli kabisa. Hawa jamaa ndio waliomtengeneza Osama, ndio walioanzisha kundi la ISLAMIC STATES. Inabidi kila mwananchi awe mlinzi wa nchi hii kwani vita vya kiuchumi vina namna yake ya kupigana. Na hii ni vita rahisi kama tutashikamana kama taifa. Wanaotumiwa tutawasubiria 2020.

Mshikane na mnaowapiga risasi na kuwabambikia kesi? Najua gaidi habagui mtu lakini jiwe ndie amewapa sababu na njia ya kuingilia. Unadhani kijana aliekosa masomo au mahali pa kulala kwa kuwa nyumba yao ilivunjwa bila fidia na/au wazazi wake kudhulumiwa haki zao bila fidia atakuwa na uchungu gani?
 
Sijui chanzo cha hii taarifa(validity yake) though jambo hili linaleta ukakasi kwenye intelligence yetu. Kama jambo hili ni kweli basi kuna haja ya kuhoji efficiency ya idara yetu ya usalama wa Taifa kama organ iliyopewa jukumu la kutulinda kwa kubaini viashiria vyote vya uvunjifu wa amani.
Mungu atuepushe kama hii taarifa ni ya kweli


Hapana kwa hili hawawezi mkuu subiri kuwe na mikutano ya kisiasa ndio utaijua hiyo idara
 
Back
Top Bottom