Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

Wanajidanganya wenyewe uzuri wa Tanzania tunaongea tu sana lakini mambo ya kushika mitutu na mabomu hayo tunawachia Congo na Burundi
 
America watu wanauwawa kuliko nchi yoyote east Africa halafu leo wanaleta kidomodomo.
Naona Tanzania,Kenya na Uganda zimewekwa level moja,halafu eti Rwanda hakuna hatari yoyote.
Mwenye akili ataona shida ilipo.
Ivi tukio Kama lakutekwa MO lile sio ugaid,, AU matukio ya watu kutekwa ovyo,, Kuna mambo mengine tunayachukulia easy ila yanaharibu image ya taifa letu lenye sifa nzuri tangu zamani,,
Mimi nilitegemea Yule Dereva aliekuwa anajinasibu kuwa yeye ndio alikodiwa na waliomteka MO,,
YULE Dereva ilitakiwa atolewe kafara apigwe ht risasi za kichwa maana ameshirikiana na watenda uhalifu.... Lakini mpk Leo yupo huru anakula magimbi
 
Mnaangaika na taarifa zilizotoka pale kwenye jumba ambalo liko ufipa kwa mabeberu, hivi lile jumba haipo kwenye Road reserves kweli
 
Wanajidanganya wenyewe uzuri wa Tanzania tunaongea tu sana lakini mambo ya kushika mitutu na mabomu hayo tunawachia Congo na Burundi
Mkuu hawa waseng.... kwa kuwatumia wake zao wanaweza kuwaleta wale wakujitoa muhanga wakasababisha machafuko. Muhimu ni kuwaondoa kabisa nchini.
 
The warning statement says US citizens should be cautious against violent crime, such as assault, sexual assault, express kidnapping, mugging, and carjacking, is common.

Express kidnapping tena?
 
Maana yake ni kwamba hata raia wa tanzania pia chukueni tahadhari. Tumekwisha!!
 
ningekuwa bashite now ningesha achia cheo

ushoga hatuutaki kweli lkn kwann bashite alopoke vile?

nimeamini jamaa anaupeo finyu wa kufikilia yaani alishindwa ata na watoto wa form four wanajua kabisa wazungu wanamuwinda jiwe

muheshimiwa raisi nitadili na hao wanaopinga kwenye mitandao

haya maendeleo ni miaka mitatu tu je akiongoza miaka 30

kama mtu ni mfupi tusiseme

all in all bashite cheo kimekushinda UWEZO
 
US warns on Tanzania travel due to ' crime and terror '

Rais Magufuli, Waziri Mahiga na Mkuu wa Mkoa Makonda ' mfupa ' wenu huu tafadhali. Tunahitaji kusikia maoni yenu kwani Mmarekani huwa hakosei na akikosea basi jua kuna ukweli wa 99.9% kama siyo ile 100% kabisa.

Kumekucha!

Nawasilisha.

Source: The EastAfrican Online.
 
Hivi kuna ugaidi gani hapa Tz? Na raia wapi wa nje wamekuwa wakifanyiwa vitendo kinyume na inavyotakiwa? Us bhana. Ukute jata Ttump hafajamu kama state department wanaongea upuuzi.
 
Kikubwa ni kuufunga ubalozi wa marekani tanzania. Hakuna njia nyingine.nimeona hata watu wakijinasibu kuwa 2019 hawatajali police 🚔 wala mtu awae yote. Sasa tuwe makini na marekani. Inawezekana ime imesha watuma hao wanaotaka kutumia ubabe bila kuogopa police. Tanzania 🇹🇿 niyetu. Wapo watu wanajinasibu kuwa hawaogopi kupigwa risasi. Tuanze kuwakamata hao na kuwahoji na kuwazibiti
 
USA mitandao ya magaidi mingi wanaifahamu, magaidi wengi wanawafahamu, na mawasiliano yao mengi wanayanasa.

Na hata ndani ya magaidi mara nyingi huwa kunakuwa na CIA.
 
USA mitandao ya magaidi mingi wanaifahamu, magaidi wengi wanawafahamu, na mawasiliano yao mengi wanayanasa.

Na hata ndani ya magaidi mara nyingi huwa kunakuwa na CIA.

Kwahiyo kwa lugha iliyo nyepesi na nyoofu kabisa hapa unataka kusema au kufunguka nini labda?
 
Tahadhari tayari imeshatolewa, ni jukumu la vyombo vyetu vibovu vya usalama navyo kuchukua hatua mahususi kujipanga, maana huwa vinajifanyaga viko usingizini tena fofofo wakati magaidi wako busy kutushambulia.
Vibovu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…