Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

MAMBO MENGINE YANAHITAJI HEKIMA, KUJIFANYA MBABE HALAFU BADO UNATEMBEZA BAKULI KWA HUYO HUYO UNAYEMTUKANA KUNA GHARAMA YAKE. KINA KIGWANGALA WANATUKANA OVYO KWA SABABU HAWANA EXPOSURE...ANGEJUA WENZETU MNAYOYAANDIKA YANA IMPACT KUBWA NA WANAWEZA WASIJE KABISA...UNAWATUKANA HALAFU UNATAKA WAJE WATUMIE FEDHA ZAO KWAKO.....THUBUTU, UTALII UNAWEZA UKAANGUKA HADI JIWE ASHANGAE, HATA HAO MILLIONI MOJA MSIWAPATE.
We Subiri tu..
 
Kama wewe ni mfatiliaji wa harakati nyingi za kivita na choko choko za marekani utaelewa hiyo tarifa bila kujali validity of the source.

Kwani mkuu nchii hii tuna usalama wa taifa au wa ccm??
Hilo ni kosa kutumia taaluma yako kisiasa. Kuna haja hao TISS kupitia upya viapo vyao na lengo na makusudio ya kuanzishwa kwake hiyo taasisi. Wajifunze kwa wenzao CIA
 
Unasema kweli kabisa. Hawa jamaa ndio waliomtengeneza Osama, ndio walioanzisha kundi la ISLAMIC STATES. Inabidi kila mwananchi awe mlinzi wa nchi hii kwani vita vya kiuchumi vina namna yake ya kupigana. Na hii ni vita rahisi kama tutashikamana kama taifa. Wanaotumiwa tutawasubiria 2020.
We kanyama wewe! Wakati mwingine muwe mnatumia akili za kawaida tu, kwa mgawanyiko na mparaganyiko huu wa kitaifa,unadhani kwa Maneno kama haya mepesi utawashawishi walioudhiwa na utawala huu kuwa pamoja na kupigana na adui!!! Ivi watu wengine ninyi mnatumia nini kufikiri!? Wazungu hujipenyeza palipo na mparaganyiko na kufanya ya kwako. Ninyi mnawaza kuwa wanataka raslimali zenu,lakini pia mkumbuke wanazalisha siraha,na soko lao ni mahali watu wanapogombana,na wakati mwingine huwagombanisha ili wapate soko la SIRAHA zao. Sasa kwa Tanzania mmewarahisishia, chokochoko mmeianzisha mwenyewe,mmefitiniana,mmeudhiana mpaka mmegawanyika. Kazi hiyo mmeifanya mwenyewe kwa uroho wa madaraka,kwa kutaka wengine wawe matumwa ndani ya nchi yao na mengi wawe mabwana wa kutumikiwa na kutetemekewa. Sasa mmarekani anakuja na kuunda makundi ili mmalizane kwakuwa tayari mmemtengenezea njia rahisi. Kuna wakati Mungu hutuma watu bila wenyewe kujijua kama wametumwa na Mungu kufikisha ujumbe, NAAM,Mimi naamini Mungu alituma watu ktk nchi hii kupiga kelele juu ya jinsi utawala unavyoliparaganyisha Taifa,wamepiga kelele weeeee! Kama vile Yohana mbatizaji ktk nyika zile za uyahudi, hawakusikilizwa walilipwa malipo wasiyo stahili kama alivyolipwa Yohana mbatizaji kwa kukatwa kichwa kwakuwa alimwambia mfalme kuwa si halali kwake kuwa na mke wa nduguye. Sasa ooooooh tushikamane, na nani!? Nilitia comment kwenye Uzi mmoja humu kuwa, ukiwa wewe ni mbabe na unaonea Jirani zako kwa kuwapiga, kupora haki zao,kuwafanya walale mapema kwa kukuogopa. Hao hawatatamani kuendelea kuishi,watakitamani kifo kiwaondolee mateso. Akitokea mbabe kuliko wewe kutaka kuangamiza Mtaa mzima,Jirani zako watafurahi sana kwakuwa wanajua na wewe utakufa pamoja nao. Samson alipomkosea Mungu,wafilisti walimtoboa macho. Alipomlilia Mungu alimsamehe. Wafilisti wampeleka kwenye sherehe yao acheze mziki wamdhihaki. Samson aliziegemea Nguzo za jengo,akamwomba Mungu amlipie kisasi na afe na wafilisti wale. HAKUKIJUTIA KIFO,ALIKIFURAHIA KWAKUWA ALIJUA ATAEPUKANA NA MATESO,PIA ADUI YAKE NAE ATAKUFA. Hamjachelewa KANYAMA. Kwashujaa huenda kilio,kwa mwoga huenda kicheko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Idara yetu ya Usalama wa Taifa ingekuwa Vizuri kuna mambo yasingweza kutokea au kama yalivyotokea nafikiri tungekuwa tumeishapata ufumbuzi na Hatua kali kuchukuliwa kwa wahusika
1. EPA
2. RICHMOND
3. KAGODA
4. MEREMETA
5. ESCROW
6. Kutekwa watu, kuuawa, kupotea na wengine kupigwa risasi hovyo.
**Pia tukumbuke tunaambiwa huku mitaani kuwa kuna baadhi ya viongozi wanalindwa na walinzi kutoka nje ya nchi nafikiri pia hili ni kielelezo kuwa kuna udhaifu fulani katika Idara hii.
Uko sahihi kiongozi, TISS ni jicho la Nchi katika kubaini viashiria vyote vya uvunjifu wa amani pamoja na kubaini na kuzuia ufisadi, mdololo wa uchumi. Kifupi ni organ muhimu kwa maendeleo ya nchi yeyote. Huku kwetu wanajisahau
 
Pamoja na hila za whites particularly Americans , bado tunatakiwa tukubari kwamba 'they are ahead us for many steps if we really dare to give the very truth to what they have speculated as to our national security (terrorism etc)'.

Vyombo yetu vya ulinzi na usalama kwa sehemu kubwa 'are good in fighting after harm but the US may smell the signs of terror and protect them'. Bado nashawishika kusema kwamba lisemwalo na US lipo kama halipo laja.


Mungu Ibariki Tanzania kama nchi na wananchi wake wanyonge, 'this prayer excludes the stronger parties (ones)'.

Sent using Jamii Forums mobile app

Usisahau American's wapo vizuri sana kuunda propaganda's na wakatumia international media zao kuuaminisha ulimwengu... ugaidi upi unaouona wewe hapa? Ushawahi sikia kwenye mkusanyiko wowote wa watu hapa Tz bomu zimelipuliwa au shootings zimefanyika na kuua halaiki ya watu hapana...

Americans have enemies everywhere...


Cc: mahondaw
 
Wakwende zao pumbav kabisa....kwani wao nani???....nchi inajiimarisha kiuchumi wanaanza visa...wanataka kila siku tuwapigie magoti tuwaombe misaade watupangie namna ya kuishi..... ie ushoga
 
Serikali ya Marekani imewaonya raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania kuwa makini na matukio ya Ugaidi , uvunjifu wa haki za binadamu na uhalifu ndani ya Tanzania.

Katika taarifa yao wamedai kuwa kuna makundi ya kigaidi ndani ya nchi ambayo huenda yanajipanga kufanya mashambulizi ndani ya nchi.

Pia taarifa hio inadai kuwa ndai ya nchi wanaohisiwa kuwa wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja hukamatwa na huenda wakalazimishwa kupimwa njia ya haja kubwa kwa nguvu na mamlaka husika.

Pia wamedai kuwa polisi ndani ya nchi hawana uwezo na miundombinu ya kupambana na uhalifu kwa hiyo wananchi wao wawe makini.

Katika suala la ugaidi wamedai kuwa mashambulizi huenda yakalenga vituo vya polisi, balozi za nchi mbali mbali, misikiti na maeneo mengine ambayo watu wa Magharibi(wazungu) wanakuwepo.
=========


Exercise increased caution in Tanzania due to crime, terrorism, and targeting of LGBTI persons.

Violent crime, such as assault, sexual assault, express kidnapping, mugging, and carjacking, is common. Local police may lack the resources to respond effectively to serious crime.

Terrorist groups continue plotting possible attacks in Tanzania. Terrorists may attack with little or no warning, targeting embassies, police stations, mosques, and other places frequented by Westerners.

Members of the LGBTI community have been arrested, targeted, harassed, and/or charged with unrelated offenses. Individuals detained under suspicion of same-sex sexual conduct could be subject to forced anal examinations.

Read the Safety and Security section on the country information page.

If you decide to travel to Tanzania:
  • Always carry a copy of your U.S. passport and visa and keep original documents in a secure location.
  • Be aware of your surroundings.
  • Do not leave your food or drink unattended.
  • Stay alert in all locations, especially those frequented by Westerners.
  • Avoid public displays of affection particularly between same-sex couples.
  • Enroll in the Smart Traveler Enrollment Program (STEP) to receive Alerts and make it easier to locate you in an emergency.
Follow the Department of State and the US Embassy in Tanzania on Facebook and Twitter Review the Crime and Safety Report for Tanzania.

U.S. citizens who travel abroad should always have a contingency plan for emergency situations. Review the Traveler’s Checklist.

Souce: Tanzania Travel Advisory

Ni uandishi wa kitoto...tahadhari imetolewa kwa nchi kadhaa lakini andiko hili kwa Kiswahili limeilenga Tanzania tu...
 
Wakwende zao pumbav kabisa....kwani wao nani???....nchi inajiimarisha kiuchumi wanaanza visa...wanataka kila siku tuwapigie magoti tuwaombe misaade watupangie namna ya kuishi..... ie ushoga
Nchi gani inajiimarisha kiuchumi?
 
Sijui chanzo cha hii taarifa(validity yake) though jambo hili linaleta ukakasi kwenye intelligence yetu. Kama jambo hili ni kweli basi kuna haja ya kuhoji efficiency ya idara yetu ya usalama wa Taifa kama organ iliyopewa jukumu la kutulinda kwa kubaini viashiria vyote vya uvunjifu wa amani.
Mungu atuepushe kama hii taarifa ni ya kweli
Hizi habari wanapewa na wapinzani ili wapate kiki ya kwenda Ikulu! Yaani bila bumumunya maneno ni machadema hayo kuchongea nchi kwa mabepari utadhani ni mama yao!
Watu wa kuhoji siyo vyombo vya usalama bali wapinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ndivyo basi wanakuwa wanakiuka kiapo chao kwa kuendekeza mambo ya vyama badala ya taaluma. Vyama vipo vitapita (refer TANU+ASP=CCM) lakini Tanzania itabaki milele. Nakumbuka hata lile tukio la kigaidi la kulipuliwa kwa balozi za Marekani za Dsm na Nairobi intelligensia yetu haikuweza kunotice mpaka maafa yakatokea. So muhimu TISS ikarudi kwenye misingi na dhima ya kuanzishwa kwake na kuachana na kutumika kwa faida za wanasiasa.


Ni ngumu sana kwa huu utawala wa JIWE yeye anawaza kujilinda mwenyewe tuu... ila ngoja lisemalo lipo
 
Ila mda mwingine ni sawa tu maana haki tena haipo ...ukoloni waTz wenzetu umetamalaki sana,polisi ana mamlaka kamili ya kuamua nani awe hai Leo na nani afe ..R.I.p Akwilini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii sijui ni kweli au ndiyo yale mambo ya propaganda "eti kuna tukio la kigaidi linakuja na magaidi wanajiandaa kushambulia wakati wowote"!!! Hivyo imewaonya raia wake kuwa makini wanapokuja Tanzania!!
Terrorist groups continue plotting possible attacks in Tanzania. Terrorists may attack with little or no warning, targeting embassies, police stations, mosques, and other places frequented by Westerners.
If you decide to travel to Tanzania:
  • Always carry a copy of your U.S. passport and visa and keep original documents in a secure location.
  • Be aware of your surroundings.
  • Do not leave your food or drink unattended.
  • Stay alert in all locations, especially those frequented by Westerners.
  • Avoid public displays of affection particularly between same-sex couples.
  • Enroll in the Smart Traveler Enrollment Program (STEP) to receive Alerts and make it easier to locate you in an emergency.
  • Follow the Department of State and the US Embassy in Tanzania on Facebook and Twitter
  • Review the Crime and Safety Report for Tanzania.
  • U.S. citizens who travel abroad should always have a contingency plan for emergency situations. Review the Traveler’s Checklist.
Duh!! Hapo kwenye "Food or drink"!!!
Source: Travel.State.Gov > International Travel > Country Information > Tanzania International Travel Information
 
Back
Top Bottom