Marekani yawawekea vikwazo waendesha mashitaka (ICC)

Marekani yawawekea vikwazo waendesha mashitaka (ICC)

Mocumentary

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
806
Reaction score
2,049
Marekani imewawekea vikwazo waendesha mashitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku kadhaa baada ya mahakama hiyo kuidhinisha uchunguzi kuhusu tuhuma za uhalifu wa kivita unaodaiwa kutekelezwa na Marekani nchini Afghanistan.
IMG_20200903_113744.jpg
IMG_20200903_113746.jpg
IMG_20200903_113748.jpg


WALE MASHABIKI WA USA NA WASHIRIKA WAKE, NA KUAMINI KUWA JAMAA WAPO SAHIHI KWA KILA KITU KUNA, JAMBO KUBWA SANA LA KUJIFUNZA HAPA
 
Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya mwendesha mashitaka mkuu wa ICC
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alitangaza jana kuwa Marekani imeweka vikwazo dhidi ya mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda kwasababu ya ofisi yake kuendelea na uchunguzi wa watu wa Marekani.

Pompeo alisema aliyeongezwa pia katika orodha ya vikwazo ni Phakiso Mochochoko mkuu wa idara ya sheria ya ICC, anayehusika na ushirikiano na hisani, kwa kutoa msaada kwa Bensouda za taarifa mbali mbali. Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani ameiita mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita, ambayo Marekani haihusiki nayo, kuwa ni taasisi iliyovurugika na yenye ufisadi wa hali ya juu

Mwezi Juni , rais wa Marekani Donald Trump alitoa amri ya rais inayoweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya maafisa wa ICC wanaohusika katika uchunguzi wa vikosi vya jeshi la Marekani kwa uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.
 
Hao ndio watetezi wa haki za binadamu duniani ambao ni marufuku kabisa kuguswa na chombo chochote siku zote hao wanatakiwa waachwe tu wafanye chochote hata Kama ma Askari wao wanabaka ma binti za watu huko wanakolinda amani lakini ni marufuku kabisa kuchunguzwa.
 
Trump anatuonyeha rangi halisi ya Marekani.
Wahenga na msemo wao wa kunya anye kuku akinya bata kaharisha waliona mbali sana.
 
Maafisa wa ICC itakuwa walishajipanga walikuwa wanajua kabisa kwamba wakianza huu mchakato lazima watakutana na haya toka USA ila kwa kuwa wameamua kuipigania haki wala hawajaonyesha kuogopa na kusita sita dhidi ya maamuzi yao ...kwa kweli wanastahiki pongezi kubwa mno
 
Kwa sasa Hivi ni dhahili kwamba Taifa Hilo sio Taifa linalotetea haki, Bali ni Taifa linatetea udhalimu na unyonyaji

Kitendo cha kuchunguzwa watu wake ni lini limekuwa ni kosa la jinai
 
Back
Top Bottom