Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2022 yatagusa maeneo haya

Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2022 yatagusa maeneo haya

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Muswada huu unapendekeza kufanya mrekebisho katika Sheria tano ambazo ni Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura ya 147, Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, Sura ya 220 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura ya 148.

Muswada huu umegawanyika katika Sehemu Kuu Sita. Sehemu ya Kwanza inahusu masharti ya utangulizi ambayo yanajumuisha jina la Muswada na namna ambavyo Sheria mbalimbali zinapendekezwa kurekebishwa katika Sehemu husika.

Sehemu ya Pili ya Muswada inapendekeza kurekebisha Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura ya 147, ambapo kifungu cha 128 kinapendekezwa kurekebishwa ili kumuwezesha Waziri kusamehe ushuru kwenye bidhaa zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi ya uwekezaji mahiri na mahiri maalumu itakayoidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji.

Marekebisho yanayopendekezwa yanalenga kuwianisha masharti ya Sheria hii na masharti ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania ili kuboresha utekelezaji wa vivutio vitakavyotolewa kwa wawekezaji. Aidha, Jedwali la Nne linapendekezwa kurekebishwa kwa kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye mvinyo unaotokana na zao la zabibu unaoingizwa nchini. Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kuhakikisha upatikanaji wa soko la zabibu zinazolimwa nchini.

Sehemu ya Tatu ya Muswada inapendekeza kurekebisha Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332, ambapo kifungu cha 10 kinarekebishwa ili kujumuisha uwekezaji mahiri ulioidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji katika wigo wa maeneo ambayo Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha anaweza kutoa msamaha wa kodi ya mapato. Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kuwianisha masharti ya Sheria hii na masharti ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania ili kuboresha utekelezaji wa vivutio vitakavyotolewa kwa wawekezaji.

Sehemu ya Nne ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Madini, Sura ya 123. Kifungu cha 87(1) kinarekebishwa ili kubainisha kiwango cha mrabaha kwa malighafi za mbolea zinazochimbwa hapa nchini. Kwa mujibu wa marekebisho yanayopendekezwa, kiwango cha mrabaha kinapunguzwa kutoka asilimia 3 hadi asilimia 1. Lengo la marekebisho haya ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa ndani wa bidhaa za mbolea.


Sehemu ya Tano ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, Sura ya 220. Kifungu cha 8 kinarekebishwa ili kumpa Waziri mamlaka ya kusamehe ushuru wa mafuta kwa miradi ya uwekezaji mahiri na mahiri maalumu itakayoidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji. Marekebisho yanayopendekezwa yanalenga kuwianisha masharti ya Sheria hii na masharti ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania ili kuboresha utekelezaji wa vivutio vitakavyotolewa kwa wawekezaji.

Sehemu ya Sita ya Muswada inapendekeza kurekebisha Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura ya 148, ambapo maboresho yanapendekezwa katika kifungu cha 6 ili kujumuisha uwekezaji mahiri ulioidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji katika wigo wa maeneo ambayo Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha anaweza kutoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani. Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kuwianisha masharti ya Sheria hii na masharti ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania ili kuboresha utekelezaji wa vivutio vitakavyotolewa kwa wawekezaji.

Aidha, kifungu kipya cha 55A kinapendekezwa kuongezwa ili kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwa kiwango cha 0 kwa mbolea inayozalishwa ndani ya nchi. Lengo la marekebisho haya ni kuleta unafuu kwa wakulima na watumiaji wa mbolea kwa kupunguza gharama za uzalishaji kwa viwanda vinavyozalisha mbolea hapa nchini. Inapendekezwa pia kurekebisha Jedwali ili kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwa magunia ya mkonge yanayotengenzwa nchini na malighafi nyingine zinazotumika kutengeneza mitungi ya gesi. Lengo la kusamehe kodi kwenye magunia ya mkonge ni kuongeza uzalishaji wa magunia hayo kwa viwanda vya ndani na kuchochea kilimo cha mkonge nchini.


19.09.2022_14.58.43_REC.png


19.09.2022_15.00.02_REC.png
 
Sehemu ya Pili ya Muswada inapendekeza kurekebisha Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura ya 147, ambapo kifungu cha 128 kinapendekezwa kurekebishwa ili kumuwezesha Waziri kusamehe ushuru kwenye bidhaa zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi ya uwekezaji mahiri na mahiri maalumu itakayoidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji.
Hapa ndipo makorokocho ya TAKUKURU yataibuka kama uyoga endapo Waziri hatakuwa mzalendo na mwenye msimamo!
 
Muswada wa sheria kandamizi za habari ziko wapi au tusubiri mpaka tufike burundi
 
Babu Tale,Jah People na Kibajaji mnawaonea bure kwenye miswaca hii hawawezi kuchangia lolote
 
Back
Top Bottom